Young Dee: Mimi situmii unga, ila ni cha-pombe mkubwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,504
d7b249edf38e5ba2e9bc100efc26346a.jpg

Young Dee amekanusha tena uvumi ulioenea mitandaoni kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea kwenye kipindi cha Harakati cha Clouds FM kinachoendeshwa na Kalapina, rapper huyo amesema tokea akiwa mdogo amekutana na mambo mengi ya kuzushiwa.

“Hata mimi nasikia sana,” alijibu alipoulizwa kuhusu tetesi za kutumia unga.

“Unajua mimi nimekuwa kwenye muziki tokea niko mdogo maana tokea nipo shule nimekutana na mengi sana. Nina imani mti wenye matunda ndio hupigwa mawe, unajua sometimes wanavyosema ukifuatisha ndio unaweza kukuta kweli unaingia huko. Lakini situmii madawa ya kulevya, mimi ndio najua maisha yangu, mimi najua natumia pombe tu,” alisema Young Dee.

Alipoulizwa kwanini aliamua kuandika ujumbe kuhusu Babutale kumsaidia Chid Benz na kama hakukubaliana na Tale haya ndio yalikuwa majibu yake:

“Mimi nilihisi kitu tofauti kabisa maana Chid ni msanii mkubwa sana na haikutakiwa kumweka vile, ilitakiwa umchukue umweke sawa kimya kimya na sio vile kila mtu aone. Kama unamsaidia huo ndio ulikuwa mtazamo wangu wa tofauti, hayo mambo mengine yaliyotokea na mimi ni binadamu.
 
asigwa we subiri tu uzuri wa unga unadevera tutamuona tu maana hata chidi mwanzo alikataa
teh teh teh
Mkuu hawa wanakanaga sana mwanzoni, ila mwisho wa siku wanaanza kutembeza bakuli wakiomba jamii iwasaidie kupelekwa sober house.

Bora hata mtu avute mabangi misokoto mia kwa siku, lakini si madawa yao haya aiseee..
 
Huyu mtoto anaonekana kabisa anabwia unga, then kwa umri wake sikutaraji Ingekuwa hata pombe awe anakunywa to the extreme kama anavyodai
 
Sasa hata kama hatumii "unga" Je hiyo pombe watawezana na WCB ??? (kuna tetesi atasainiwa WCB)
 
d7b249edf38e5ba2e9bc100efc26346a.jpg

Young Dee amekanusha tena uvumi ulioenea mitandaoni kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea kwenye kipindi cha Harakati cha Clouds FM kinachoendeshwa na Kalapina, rapper huyo amesema tokea akiwa mdogo amekutana na mambo mengi ya kuzushiwa.

“Hata mimi nasikia sana,” alijibu alipoulizwa kuhusu tetesi za kutumia unga.

“Unajua mimi nimekuwa kwenye muziki tokea niko mdogo maana tokea nipo shule nimekutana na mengi sana. Nina imani mti wenye matunda ndio hupigwa mawe, unajua sometimes wanavyosema ukifuatisha ndio unaweza kukuta kweli unaingia huko. Lakini situmii madawa ya kulevya, mimi ndio najua maisha yangu, mimi najua natumia pombe tu,” alisema Young Dee.

Alipoulizwa kwanini aliamua kuandika ujumbe kuhusu Babutale kumsaidia Chid Benz na kama hakukubaliana na Tale haya ndio yalikuwa majibu yake:

“Mimi nilihisi kitu tofauti kabisa maana Chid ni msanii mkubwa sana na haikutakiwa kumweka vile, ilitakiwa umchukue umweke sawa kimya kimya na sio vile kila mtu aone. Kama unamsaidia huo ndio ulikuwa mtazamo wangu wa tofauti, hayo mambo mengine yaliyotokea na mimi ni binadamu.
"Mimi sili mineli,
Wala sivuti Kubeli,
Ila i use Ndumu,
this is ghetto baby,
Nilipompoteza Father,
Pata Hopes kwa Mother,
........"

Nimeukumbuka huu mstari wa wimbo wa Swahili remix ya All the Above - Tpain na maino
 
mbona hata chidi alikua anabisha sana akiulizwa, ngoja uanze kudebweda tu
 
Wabongo hatutakiani mema ndio maana kila siku tunasingiziana mambo ya ajabu ajabu tu. Sio vizuri kuandika mitandaoni kuwa Fulani anapumuliwa Kama mnauhakika. Kupumuliwa sio jambo zuri.
 
Wabongo hatutakiani mema ndio maana kila siku tunasingiziana mambo ya ajabu ajabu tu. Sio vizuri kuandika mitandaoni kuwa Fulani anapumuliwa Kama mnauhakika. Kupumuliwa sio mambo zuri.
vp mkuuu hlo povu au unafrahia mwenzio kupumuliwaaa
 
Kukataa kinachoonekana na watu ni kama kupanda mnazi chooni utastawi kwa mbolea ya kinyessi na maji machafu na huitakuwa siri Tena. Dogo anapeng'a unga huyu dalili zinaonekana japo hio pichani anapiga weedah kama vile sheria imemruhusu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom