FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,416
- 7,828
Mawimbi ya redio ya ajabu kutoka anga za juu yagunduliwa na darubini Canada
Picha: Mawimbi hayo huenda yanatoka kwa nyota ya nutroni - au pengine viumbe
wengine anga za juu. (Picha: Getty Images)
Wataalamu wa anga za juu wamefichua kwamba walinasa mawimbi ya redio ya ajabu ambayo yalikuwa yanatoka mbali sana katika anga za juu.
Mawimbi hayo yalinaswa na darubini ya kufuatilia mawimbi ya redio ambayo ipo Canada na yanaaminika kutoka kwenye mfumo wa nyota na sayari ulio mbali sana.
Chanzo halisi cha mawimbi hayo ya redio bado hakijabainika na wala wataalamu hao hawajafahamu sifa kamili za mawimbi hayo.
Miongoni mwa mawimbi hayo ya redio ya kasi sana (yanayofahamika pia kama FRBs kwa maana ya Fast Radio Bursts), ambayo yalinaswa mara 13, kulikuwa na mawimbi yasiyo ya kawaida yaliyokuwa yakijirudia tena na tena. Yanaaminika kutoka kwenye chanzo kimoja umbali wa takriban miaka 1.5 bilioni kwa miaka ya kasi ya mwanga.
Tukio kama hilo limewahi tu kuripotiwa mara moja tu awali, na darubini tofauti.
"Kufahamu kwamba kuna nyingine imepatikana ni jambo linalodokeza kwamba kunaweza kuwa hata na zaidi," amesema Ingrid Stairs, ambaye ni mtaalamu wa fizikia ya anga za juu katika Chuo Kikuu cha British Columbia (UBC).
"Na tukiwa na mitambo zaidi ya kuimarisha nguvu za mawimbi hayo na pia vyanzo vingi, basi tunaweza tukafahamu na kutanzua kitendawili hiki cha anga za juu - tujue mawimbi haya yanatokea wapi na nini chanzo chake."
Kituo cha kutafiti anga za juu cha CHIME, kinachopatikana katika Bonde la Okanagan katika eneo la British Columbia, kina antena nne (waya maalum za kupokelea mawimbi ya sauti) za urefu wa mita 100 ambazo hufuatilia anga ya kaskazini kila siku.
Darubini iliyotumiwa ilianza tu kufanya kazi mwaka jana, na iliyanasa mawimbi hayo 13 ya redio karibu mara moja, pamoja na mawimbi hay ya kujirudia.
Picha: Darubini mpya ya mawimbi ya redio ya CHIME, Canada.
Matokeo ya utafiti huo hamechapishwa katika jarida la Nature. "Tumegundua mawimbi ya pili yanayojirudia ambayo yanafanana na yale ya kwanza," Shriharsh Tendulkar wa Chuo Kikuu cha McGill, Canada amesema.
"Hili linatufahamisha zaidi kuhusu sifa za mawimbi haya ya kujirudia yakiwa kama kundi."
FRBs ni mawimbi mafupi, yenye nguvu sana ya redio ambayo yanaonekana kana kwamba yanatokea katikati ya mwendo nusu wa umbali wote wa vitu vyote vilivyopo (nyota na sayari na anga) kwa makadirio ya wanasayansi.
Kufikia sasa, wanasayansi wamegundua mawimbi takriban 60 ya redio ya pekee yanayokwenda kwa kasi sana, na mawimbi mara mbili yanayojirudia.
Wanaamini kwamba kunaweza kuwa na mawimbi ya redio ya FRBs maelfu yanayopita angani kila siku.
Mawimbi haya yanatolewa na viumbe wa anga za juu?
Kuna nadharia kadha kuhusu nini huenda kikawa chanzo cha mawimbi haya.
Moja ni kwamba huenda kukawa na nyota ya nutroni ambayo ina nguvu nyingi sana za sumaku na ambayo inazunguka yenyewe kwa kasi sana. Nyota za nutroni ni kitu kwenye anga za juu ambacho si kikubwa sana (nusu kipenyo chake ni kilomita 30 hivi) na kina uzani wa juu sana, na kimeundwa na nutroni (neutron) ambazo zimebanana sana).
Picha: Darubini ya VLA katika jimbo la New Mexico, Marekani ilikuwa ya kwanza
kunasa mawimbi ya redio yaendayo kasi kutoka anga za juu yanayojirudia.
Mawimbi haya ya redio yanaweza pia yakawa yanatokana na nyota mbili za nutroni kuungana.
Kuna baadhi ya watu, ingawa wachache, ambao wanasema kuna uwezekano mawimbi hayo yakawa yanatokana na chombo cha anga za juu pengine kutoka kwa viumbe wanaoishi anga za juu, au mawimbi yenyewe yawe ni chombo hicho cha anga za juu.
Chanzo: BBC Swahili