Mawifi chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika

Mawifi chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2016
Posts
533
Reaction score
741
Hii tabia ya wifi kuingilia ndoa za ndugu zao na kuleta mtafaruku ambao wakati mwingine kupelekea kwa ndoa nyingi kuvunjika inazidi kushamiri kila uchao.

Utakuta hawa mawifi ndo chanzo cha migogoro katika ndoa nyingi na wakati mwingine kuwapangia ndugu zao kipi wawafanyie na kipi wasiwafanyie wake zao na wakati mwingine kuanzisha matabaka kwa kumpenda mke wa ndugu flani na kumtenga mke wa ndugu mwingine kwasababu sisizo za msingi, kwa mfano utakuta wanamchukia mke wa ndugu flani kutokana na either mmewe anampenda sana au kwasababu hapendi kuwaskiliza wao.Utakuta mtu anapendana na anaishi vizuri na mke wake lakini mawifi wanaanza kutafuta maneno kwa ajili ya kuwatenganisha na wakati mwingine mwanaume usipokuwa makini basi utakuta ndoa yako inasambaratika.

Dada zangu chonde chonde hebu badilikeni kama ndugu yako ana mke wake na wanapendana waache waishi kwa amani kwani wamechaguana wao na sio kuanza maneno yasiyo na tija mara sijui huyu hapa kwetu anatujazia tu choo, mara ni mvivu, mara sijui lazima tumkomoe kwa kumchonganisha na mmewe kwasababu tangia aje hapa kwetu upendo wa ndugu yetu umepungua kwetu au yeye ndo anapendwa zaidi na sababu nyingine sisizo na msingi ambazo mwishowe husababisha ndoa kuwa na mgogoro na wakati mwingine hata kuvunjika.

Na sisi wanaume kama umeoa ishi kwa upendo na mkeo mjenge maisha yenu na sio kuanza kusikiliza maneno ya uchonganishi kwa mkeo kutoka kwa baadhi ya ndugu na wazazi maana baadae utajajuta na ikumbukwe kuwa ndoa ni ya wawili na usikubali ndugu au wazazi kuingilia ndoa yenu kwasababu zao binafsi na uwe makini na maneno yanayoweza kukuchonganisha na mwenza wako kutoka either kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na ukumbuke huyo ni mkeo uliyemchagua na ni jukumu lako kumlinda na kumtunza.
 
Sasa wewe ndoa ikushinde usingizie mawifi sijui mama mkwe siamini hivyo hata kidogo.Ndoa ni nyie wanandoa mmavunja wenyewe hata vitabu vitakatifu vinasema mwanamke huvunja ndoa yake mwenyewe na pia inasema mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja sasa hapo mawfi wanatoka wapi!tunzeni ndoa zenu muache kusingizia watu wengine
 
Lkn kama mke wako ni mvivu au mchafu kweli kwa nn watu wasikuambie?kuna vengine vinauma wanavyofanya wake zetu na ukiangalia ata ww mume unaona ni kweli. Kwa nn usimuwache?tupo nayo tunaenda nayo ila yanauma .yamenikutaaaaaaa eeeeeeeee binafasi
 
Sasa wewe mkeo akiwa mvivu dada ako inamhusu nini? Ni mkeo au ni mke wenu??
 
Sasa wewe ndoa ikushinde usingizie mawifi sijui mama mkwe siamini hivyo hata kidogo.Ndoa ni nyie wanandoa mmavunja wenyewe hao mawfi wanatoka wapi!tunzeni ndoa zenu muache kusingizia watu wengine
Hili lina ukweli
 
Kosea pote usikosee kuolewa na mwanaume asiye na msimamo. Kweli kuna mawifi na wakwe vichomi, ila mume akisimama kwenye nafasi yake, watasurrender wenyewe. Sasa upate mume bendera fuata upepo, utajutraaa
 
Lkn kama mke wako ni mvivu au mchafu kweli kwa nn watu wasikuambie?kuna vengine vinauma wanavyofanya wake zetu na ukiangalia ata ww mume unaona ni kweli. Kwa nn usimuwache?tupo nayo tunaenda nayo ila yanauma .yamenikutaaaaaaa eeeeeeeee binafasi
Sasa mkeo kuwa mchafu dada ako yanamuhusu nn uwo uchafu Wa mkeo yaweza kuwa ww mume ndo uliupenda
Kwaiyo kwako ni sahihi dada yako kumwaona mkeo mchafu na sio ww kama mume kuongea na uyo mkeo kuusu swala hilo la uchafu.
Kweli akili zatofautiana
 
Ndugu wa kiume akiwaendekeza hao, hapo ndipo shida uanza na kuendelea bila mawifi kuona aibu. I thank God kuwa, wake wa wadogo zangu wanafuraha na sisi dada za waume wao.
 
Mawifi wengine wazuri ndo wakwanza kujua mimba ni yako au la wanaesabu ad cku ucwaalibie sifa Mawifi wa watu
 
Hii tabia ya wifi kuingilia ndoa za ndugu zao na kuleta mtafaruku ambao wakati mwingine kupelekea kwa ndoa nyingi kuvunjika inazidi kushamiri kila uchao.

Utakuta hawa mawifi ndo chanzo cha migogoro katika ndoa nyingi na wakati mwingine kuwapangia ndugu zao kipi wawafanyie na kipi wasiwafanyie wake zao na wakati mwingine kuanzisha matabaka kwa kumpenda mke wa ndugu flani na kumtenga mke wa ndugu mwingine kwasababu sisizo za msingi, kwa mfano utakuta wanamchukia mke wa ndugu flani kutokana na either mmewe anampenda sana au kwasababu hapendi kuwaskiliza wao.Utakuta mtu anapendana na anaishi vizuri na mke wake lakini mawifi wanaanza kutafuta maneno kwa ajili ya kuwatenganisha na wakati mwingine mwanaume usipokuwa makini basi utakuta ndoa yako inasambaratika.

Dada zangu chonde chonde hebu badilikeni kama ndugu yako ana mke wake na wanapendana waache waishi kwa amani kwani wamechaguana wao na sio kuanza maneno yasiyo na tija mara sijui huyu hapa kwetu anatujazia tu choo, mara ni mvivu, mara sijui lazima tumkomoe kwa kumchonganisha na mmewe kwasababu tangia aje hapa kwetu upendo wa ndugu yetu umepungua kwetu au yeye ndo anapendwa zaidi na sababu nyingine sisizo na msingi ambazo mwishowe husababisha ndoa kuwa na mgogoro na wakati mwingine hata kuvunjika.

Na sisi wanaume kama umeoa ishi kwa upendo na mkeo mjenge maisha yenu na sio kuanza kusikiliza maneno ya uchonganishi kwa mkeo kutoka kwa baadhi ya ndugu na wazazi maana baadae utajajuta na ikumbukwe kuwa ndoa ni ya wawili na usikubali ndugu au wazazi kuingilia ndoa yenu kwasababu zao binafsi na uwe makini na maneno yanayoweza kukuchonganisha na mwenza wako kutoka either kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na ukumbuke huyo ni mkeo uliyemchagua na ni jukumu lako kumlinda na kumtunza.
 
Kosea pote usikosee kuolewa na mwanaume asiye na msimamo. Kweli kuna mawifi na wakwe vichomi, ila mume akisimama kwenye nafasi yake, watasurrender wenyewe. Sasa upate mume bendera fuata upepo, utajutraaa
Mume akiwa hivo inabidi apate mwanamke fyatu kama yule aisha, kuna clip ipo whatsapp Aisha anahojiwa na dida anasema nimekuja kuwachamba mama mkwe, mawifi zangu pamoja na mume wangu ha ha ha ha ha nilicheka sana
 
Tuombe mwenyezi mungu atupe Mume/Mke mwenye kheir na sisi changamoto za wifi,Mama mkwe,Baba mkwe,Shemeji
zitakuwepo tuu,ila wewe mke ndio unatakiwa kutumia akili yako na zidi kumuomba Mwenyezi mungu akupe subra na uvumilivu kwani kila familia utakayo ingia ina majanga yake, unaweza ukakuta mkwe mpole na ma wifi wapole lakini mashemeji ndio balaa,wewe kama mke ndani ya nyumba nilazima ujue kuishi na watu tabia yako kama mbaya usilaumu wifi
Hukuolewa na wifi umeolewa na mumeo wifi anakukera nini? mie kwa upande wangu wifi shemeji sio threat hawajawa na hawatokua tishio kwenye ndoa yangu,huenda mkwe sababu namuheshimu sana Mama na Baba na hawa ni sawa na wazazi wangu,walobakia wakiniheshimu sawa hawakuniheshimu sawa mie shida yangu mume wangu sio mazowea na wao,na wala sipotezi mda wangu kuwa please wao,ntawapa heshima yao kama wifi na kama shemeji lakini wasi cross line...
ukishughulika na wao mume atakushinda....
 
Mume akiwa hivo inabidi apate mwanamke fyatu kama yule aisha, kuna clip ipo whatsapp Aisha anahojiwa na dida anasema nimekuja kuwachamba mama mkwe, mawifi zangu pamoja na mume wangu ha ha ha ha ha nilicheka sana
Ahaha sijaiona. Ila huyo Aisha ni kwamba yamemfika hapa, yupo tayari kwa lolote. Mawifi/wakwe headache, upate na mume headache tena khaa
 
Back
Top Bottom