Mawazo ya watu wachache yanavyokandamiza madaktari na taaluma ya Udaktari. Toa maoni yako

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari WanaJF, naomba nisiwapotezee muda sana .Jambo la msingi kama Title inavyojieleza ni kuhusiana na Watu wachache wanavyo haribu Kada ya Afya Tanzania. Hivyo basi kwa leo ntagususia na Kushauri mambo Mawili ambayo Yanaumiza vichwa sana Madaktari wetu kwa Sasa .

1.CPD
Baraza La Madaktari Tanganyika lilikuja na wazo zuri sana la CPD- continuous proffessional development ili kuhakikisha madaktari wetu hawasahau vitu na wanapata elimu mpya yote hayo ikiwa ni kuboresha huduma ya Afya .Na kwa umuhimu wake MCT wakaona ni bora hawa Madaktari wasirenew leseni zao bila kuwa pointi 5 kwa 2022 na pointi 20 kwa miaka inayoendelea .

Ni Jambo Zuri tatizo ni namna hizo points zinavyopatikana kunakuwa na Changamoto zifuatazo:
A.CPD providers wamefanya kama njia ya kujiingizia kipato ,Sasa kila mwaka Madaktari wanalipia pesa ya Kurenew leseni na bado mtu alipie pesa ya kushiriki presentations ili apate points za kupata hiyo leseni sio sawa ,atarudi na nini nyumbani mwisho wa mwezi ?

B.Muda na Mazingira ya kazi ,Madaktari wengi wanabanwa sana na muda kulingana na uchache wao hivyo wanakuwa bize sana lakini pia maeneo waliyopo inakuwa ngumu sana kuaccess huduma ya internet kushiriki hasa Online .

Hivyo Basi kufuatia sababu tajwa hapo Juu yafutayo ni mapendekezo ili kuweza kufanikisha zoezi la CPD

i. Viwepo vyanzo mbalimbali za kupata points kama Vile MAHUNDURIO YA VIKAO VYA MAPITIO YA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI NA WATOTO WACHANGA -MPDRSR kitu ambacho huwa hayaridhishi ,CLINICAL MEETINGS na CME- continuing medical education.

ii. CPD providers inabidi watoe huduma for free Washiriki watakao hitaji wajigharamie au wagharamiwe na vituo vyao.

iii. MCT na MAT ni vitu viwili tofauti ,Baraza na chama cha madaktari ni vitu viwili tofauti sasa MAT inabidi ijitahidi kufanye vizuri na kujitangaza ili ipate wanachama sio kupitia Mgongo wa MCT na CPD kwa maana kumekuwa na presentations zenye favour kwa MAT members .

iv . MCT inabidi ijitanue either iwe na ofisi kila mkoa au ichague baadhi ya Madaktari wawe wajumbe kwa ajiri ya ufuatiliaji wa hilo zoezi la Continuos Proffessional Development huku mikoani na wilayani .

2. PRE AND POST INTERNSHIP EXAMINATION ,Hili suala linahitaji liangaliwe kwa jicho la Pekee ni kweli kwamba kuna incompetent graduates lakini Haiwezekani mtu asome toka mwaka wa kwanza mpaka wa Tano kisha aje azuiliwe baada ya kumaliza intern au apimwe kwa mtihani mmoja .Hivyo wizara na MCT waunde bodi ya madaktari iwe inaanda mitihani ya Vyuo vyote na externals kwa ajili ya clinicals ingawa shule ya udaktari itazidi kuwa Ngumu lakini tupate watu competent kama lilivyo lengo la huo Mtihani.

Lakini pia vyuo visipewe usajiri tu vifuatiliwe kwa kina ,Daktari ni mtu muhimu sana akikosea kidogo anaweza matokeo ambayo sio mazuri .

WanaJF hayo ni mawazo yangu kama mdau wa afya na ni mawazo ya madaktari wengi ,kama Daktari,Mtumishi wa Afya ,Mwananchi mzalendo mchango wako ni muhimu katika hili na ni hakika kwamba hili suala halipo kwa madaktari tu .Karibuni
 
Back
Top Bottom