Mawazo ya mwanadamu

Mawazo ya mwanadamu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,453
Reaction score
872,058
Kama ilivyo kawaida yake, aliamka mapema, akaingia kwenye chumba chake cha mazoezi, akapasha viungo joto.

Baada ya muda kidogo anatoka, akaingia bafuni akaoga.

Baada ya hapo akavaa suruali na shati jepesi, ataenda sebuleni akaketi. Alianza na glasi ya maziwa, ikifuatiliwa na supu, kikombe cha chai ya maziwa, yai na mhogo vya chemsha. Akashushia na glasi ya juice.

Akanyanyuka akaelelekea kwenye meza yake ya kazi, akachukua jalada lenye nyaraka za manunuzi, akazipitia kwa makini, alatingisha kichwa kwa kuridhika akisema "safi sana".

Akachukua jalada la mauzo, ooh, kazi nzuri hali kadhalika. Akapitia hesabu zote, akaona kwamba amepata faida ya kutosha kutoka kwenye kila mradi.

Ilikuwa takribani saa nne asubuhi, mkewe akamletea kikombe cha chai ya rangi na viazi vichache vya kuchemsha.

Baada ya mapumziko hayo mafupi, akachukua jalada wa watu anaowadai, akalipitia kwa makini huku akitafakari jambo.

Wa kwanza ni mama, alikopa ili amudu gharama za matibabu ya mume, bahati mbaya mume alifariki, yule bwana akawaza, huyu ana misiba miwili, wa mume na deni na uwezo wa kulipa hana, akaaigiza aitwe, alipofika akamweleza kwamba amemsamehe deni.

Wa pili ni mwanaume, huyu alikopa ili amudu gharama za masomo ya mwanae, mtoto katoroka shule na sasa ni teja, naye akamsamehe deni.

Watatu ni mfanyabiashara ndogondogo, deni nilamuda na lina roba, akamwita. Kijana akieleza anavyojitahidi na changamoto anazokumbama nazo, akamhimiza alipe kidogokidogo ila alimfitia riba.

Baada ya zoezi hilo mlo wa mchana ukawa utayari. Baada ya chakula akaingia chumbani akajipumzisha.

Jioni, jua likiwa limepunguza makali akatoka akiwa amefuatana na mkewe, wakienda kutembelea miradi yao. Huko mambo ni mazuri, kila mradi ulikuwa unaendelea vyema.

Warudi nyumbani akaketi tena kwenye meza ya kazi, akachukua kalamu na karatasi akaanza kuandika, amabuni mradi mpya. Baada ya muda akamwita mkewe, akamshirikisha mpango huo. Alikuwa ameandaa andiko la mradi vyema na alibakiza tu sehemu ya makisio ya gharama za uendeshaji na mapato.

Ilikuwa kama saa kumi na mbili jioni, akaingia ndani akabadilisha nguo na kutoka kwenda mazoezi.

Baada ya mazoezi akarudi akaoga na kuangalia taarifa ya habari ya jioni.

Mlo wa jioni ulikuwa tayari wakala. Sala ya jioni ilifuata baadae kidogo.

Baada ya sala akawaaga wanawe na wajakazi wake akaenda kulala. Aliwa anavuta usingizi akatafakazi kuhusu mali zake, akaona kwamba anao utajiri wakutosha akajiseme moyoni mwake, "Moyo wangu kula na kunywa, ustarehe, una mali nyingi."

Akitafakari hayo akaona taswira ya mtu mwenye mavazi meupe akimwambia, 'Mpambavu wewe, hujui kwamba leo hii watakuja kuichukua roho yako?"

Kabla hajafanya chochote akajiona anakosa pumzi na mwili na roho yake vikatengana, AMINA.

Kumbe mawazo ya mwanadamu sio mawazo ya Mungu.

Basi tukeshe tukiomba maana hatuijui siku wala saa. JUMAPILI NJEMA
 
Basi tukeshe tukiomba maana hatujui siku wala saa!

Kisa cha huyu tajiri ni kizuri sana kinatukumbusha kufanya hicho kilicho chema.
 
Mshana Jr siku za Sunday anakuwaga tofauti sana; unaambiwa kiama kama itakuwa siku kama hii, pepo ataiona 🙂
 
Kila nafi itaonja mauti

Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
 
Wacha kumchuria jemedari wa Afrika.

Huyu ataishi muda mrefu sana maana amekuja kwa kusudi maalumu la kuwavusha watanzania na Waafrika walio wengi.... Mfano huu unaishi, (jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la kukumbukwa).
 
Wacha kumchuria jemedari wa Afrika.

Huyu ataishi muda mrefu sana maana amekuja kwa kusudi maalumu la kuwavusha watanzania na Waafrika walio wengi.... Mfano huu unaishi, (jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la kukumbukwa).
Leo ni Jumapili na hili sio jukwaa la siasa... BTW sihusiki na tafsiri yako bali nasimamia maandiko yangu
 
Mkuu badili hayo mazingira uliopo leo. Si mazuri kwa afya ya akili.
 
Back
Top Bottom