Mawazo mgando ndani ya ccm. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawazo mgando ndani ya ccm.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mkute, Apr 14, 2011.

 1. mkute

  mkute Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kama kuna chama cha siasa kilichoshindwa kusoma alama za nyakati kisiasa,basi chama hicho si kingine ila ccm.Chama hiki hivi karibuni tumeshuhudia kamati ya sekrearieti ya chama ikijiuzulu ktk harakati za kile wanachoita kujivua magamba,ili kurudisha mvuto wa chama hasa baada ya kupoteza imani ya watanzania ktk uwezo wao kiutawala.
  Mara nyingi tumeshuhudia ccm inapotokea aidha kuwajibika kwa jambo fulani linalohusiana na viongozi wake kuhusishwa na kashifa mbalimbali kama ambavyo imekuwa kawaida kwao,au kushindwa kutekeleza ahadi zao kwa wananchi, viongozi wazee wa ccm, waliozeeka kwasababu ya unafiki na uwongo tangu siku walipoonjeshwa utamu wa pesa za mafisadi wa nchi hii. Haijalishl umri ktk chama hiki kwani hata vijana mawazo yao huwezi tofautisha na wazee wanaokufa kesho ndani ya ccm.wanafiki!
  Ndio maana mmoja wa uvccm aliwapa ukweli kuwa kama utakuwa mnafiki ukiwa kijana ukizeeka lazima uwe mchawi! nakwambia wazee wengi ndani ya ccm ni wachawi kabisa! Na mchawi si lazima awe yule anaeroga kwa tunguli au kuruka na ungo,hapana hata maneno yanapotumiwa vibaya ni uchawi tosha.
  Mfano mzuri ni uchawi wa mawazo mgando ya tuhuma za makamu wa kwanza wa ccm bara kuwa Jamiiforums ndio wanakibomoa chama chao,hii nadhani hawa wazee wamepoteza uwezo wa kufikiri,ina maana ameshindwa kuelewa website hii inatumiwa na wananchi wenye uchungu na nchi yao? na sio wanasiasa jau chama cha siasa hata yeye anakaribishwa alimradi tu alete hoja za ukombozi wa mtanzania na sio uchawi wake! kwa taarifa yake great thinkers hawalogeki na mapambano yan
  aendelea mpaka kieleweke!
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine msiwalaumu CCM.....Watanzania wenyewe ndio tumewajengea hii ngome imara na kututumia na ujinga wetu kama mtaji wao...

  Angalau tunapowasaidia kujua sasa tuko serious na future yetu na si ujinga wa kijuha wa kujivuna na mavazi ya chama na kadi wakati nyumbani watoto wanakufa njaa ndipo watakapobadilika

  Mahali popote duniani mtaji wa wanasiasa wachafu na vyama vilivyochoka kuongoza kuleta mabadiliko kwa watu wake hubakiwa na mtaji wa ujinga wa wananchi wanaobakiwa na fahari ya chama mfu kwa kuwa tu "ni chetu toka enzi" huku familia haina uhakika wa chakula na watoto shule hawaendi tena

  Kwa kweli pongezi zinastahili kwenda kwa kila mmoja aliewasaidia CCM kugutuka na kufahamu kuwa tayari misumari mi-4 ya jeneza imeshapigiliwa tunasubiri miwili ya mwisho
   
Loading...