Mawazo mchanganyiko juu ya namna ya kukabili changamoto ya ajira kwa vijana

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Nchi nyingi duniani zinakabiliwa na janga la ukosefu wa ajira kwa vijana, mfano nchi ya Nigeria ambayo nusu ya watu wake ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-35 inakabiliwa na ukosefu wa ajira ya zaidi ya vijana 11.1 milioni. Halikadhalika nchi za Afrika ya Kusini, Kenya, Uganda na zingine nyingi.

Tatizo la ajira kwa Tanzania ni la kihistoria, na serikali ya awamu ya tano inajitahidi kukabiliana nalo kwa njia tofauti.Njia ya kurasimisha shuguli za wajasiria mali kwenye kilimo, ufugaji, na biashara ndogo ndogo kama kuwa na vitambulisho kwa wamachinga, pamoja na shughuli za wasanii zimeleta tija na vijana wengi wanafaidiaka kutokana na mbinu hii ya serikali. Hata hivyo juhudi hizi zimepunguza na sio kumaliza janga la ukosefu wa ajira.

Kukabili janga la ukosefu wa ajira mbinu tatu hutumika, kutengenza hitaji la ajira (labor demand), kutengeneza waajiriwa (labor supply) na kuimarisha mfumo wa ajira (labor market intervention). Tanzania inahitaji mbinu zote tatu kuhakikisha inakabili janga la ajira. Makala hii itajikita katika kuonesha ni wapi serikali na wananchi kwa ujumla wawekeze kutengeneza ajira kama mbinu kuu ya kumaliza tatizo la ajira nchini.

Miradi ya Kilimo na Ufugaji wa Pamoja
Changamoto za mitaji, masoko na teknolojia zinaweza kutatuliwa kwa kuwajumuisha watu pamoja.Kilimo cha pamoja kinaweza kuwawezesha wakulima kupata tija kupitia kilimo na kuifanya kazi ya kilimo kama ajira kama zilivyo ajira zingine.Wataalamu kutoka nyanja mbalimbali wanauwezo wa kukusanya mtaji na kuanza kilimo katika ngazi ya chini na kukua haraka. Mifano ipo ya watu kununua heka tano kwa Tsh 500,000 kwa maana ya heka 100,000 na kulima vitunguu na kukua mpaka kufikia umiliki heka 100 na kuondokana na umaskini.

Miradi ya Viwanda vya Pamoja
Tunarudi pale pale changamoto kubwa ni mtaji, lakini kwenye suala la viwanda changamoto nyingine ni ujuzi. Tunalo tatizo la kundi kubwa la vijana kupitia mfumo wa masomo ambayo kwa namna moja au nyingine yanawapelekea kuwaza kuajiriwa na sio kufungua karakana kwa ajili ya kutoa huduma kutokana na ujuzi alio nao.

Mfumo mzuri wa uanzishaji wa biashara
Mfumo uliopo kwa sasa hivi unahitaji mwananchi kulipa tozo mbalimbali kama vile Brela, Manisapaa, TRA na zingine kabla ya kuanza biashara. Mfumo huu sio rafiki kwani gharama hizi ni sehemu ya kikwazo wa vijana wanaoingia kwenye biashara. Serikali kuwapa vijana wanaomaliza vyuo na kutokuwa na kazi wenye nia ya kuanzisha biashara mfumo mzuri kodi.Tax heaven kuna weza kupunguza idadi ya wahitimu wanaosubiri kuajiriwa.

Mfumo wa Utambuzi wa Vyeti kama dhamana
Tatizo la kifedha au mtaji ni kilio kikubwa kwa vijana, mwanafunzi wa chuo kikuu hutumia gharama kubwa sana kuweza kupata cheti chake. Mwanafunzi huyu hawezi kutambulika popote kama hana hiki cheti, hivyo kutumika cheti kama dhamana kunaweza kukamsaidia mwanafunzi kuweza kupata mtaji na kujikwamua kimaisha.

Miradi mipya ya Kimkakati
Miradi ya Umeme, miradi ya ununuzi wa ndege za mizigo, miradi ya Mwendokasi pamoja na miradi ya SGR

Kusamahe malimbikizo ya kodi kwa kampuni
Zipo kampuni binafsi ambazo zilifanikiwa kupata msamaha wa malimbikizo ya kodi uliotolewa na Raisi 2018.Kutokana na taarifa kutowafikia wenye makampuni ni wazi uwa zipo pia kampuni ambazo hazikuweza kuwasilisha taarifa ili zifaidike na mpango huuu na kuanza tena biashara.

Wakaguzi binafsi (Private Inspectors)
Tasisi za Umma kama EWURA, OSHA, TRA, TAEC, NEMC, na zingine ziweke mfumo wa kuajiri wakaguzi binafsi ambao watapewa kamisheni kwa kazi wanazofanya.Mfumo huu unafanywa na OSHA. Kiwango cha ufanisi katika mfumo huu kiboreshwe.

Kama una wazo au lolote naomba uchangie kwa manufaa ya nchi yetu na vizazi vyetu.
 
Sulihisho mabomu ya nuclear makubwa yaliyopo Duniani kote yalipuke kwa pamoja dunia iwe majivu tukose wote.
 
Back
Top Bottom