Mawazo kuhusu familia/Ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawazo kuhusu familia/Ndoa

Discussion in 'Great Thinkers' started by Shayu, Dec 8, 2016.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Dec 8, 2016
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 502
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 180
  Haijalishi ukubwa wa harusi uliyofanya kitu cha muhimu ni unachokwenda kukijenga baada ya harusi, baada ya watu wote kuondoka na kuwaacha peke yenu mwende nyumbani, mkaanzishe maisha yenu. hiko ndicho cha muhimu na ndicho kinachotakiwa kupewa umakini mkubwa. Usisahau hilo jua kwamba una kazi kubwa mbele yako, na usichukulie harusi kwa ukubwa usiostahili zaidi ya kile unachoenda kukijenga. "Familia"

  Harusi ni ya siku moja, lakini unachokwenda kukijenga huenda kikaishi muda, zaidi ya uhai wako. Kwakuwa misingi utakayo wajengea watoto wako ndio misingi hiyo hiyo watakayo wajengea watoto wao. Ubora wa familia yako huenda ukawa pia ubora wa familia zao.

  Inategemea ulivyolelewa na wewe utawalea hivyo hivyo. Kwahiyo kwa mwanamume hana haja ya kufurahia sana harusi bali kufikiri kazi iliyo mbele yake. Kulea watoto katika maadili na nidhamu.

  Kulea watoto kama simba walio nyikani, ili wakabiliane na changamoto zote za duniani. Kwasababu maisha ya duniani sio rahisi sana yanahitaji busara kukabiliana nayo. Unawezaje kufanya harusi kubwa na kujenga baadae kisicho na thamani? Ewe kichwa cha familia?
   
Loading...