Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
Kwenu,
Kiutendaji, wizara huendeshwa na Katibu Mkuu wa wizara husika akisaidiana na makamishna na wakurugenzi. Hawa ndiyo engine.
Kazi ya mawaziri ni kusimamia sera.
Kwa siku za karibuni,mawaziri hawafanyi kazi kwa programu walizojiwekea. Wanasubiri maelekezo ya Rais. Wanasubiri mwangwi. Kila waziri amebaki kutangaza viwanda na reli ya standard gauge.
Hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi.
Hata hivyo kuna mawaziri wanaojituma sana kufanya kazi; Prof Makame Mbarawa wa Miundombinu, William Lukuvi wa Ardhi, Selemani Jafo wa TAMISEMI na Luhaga Mpina wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira. Hawa huzunguka nchi nzima kukagua miradi, kusikiliza kero, kutoa maelekezo na kufanya maamuzi.
Wengi wa mawaziri waliobaki ukiacha Waziri Mkuu, kama akina 'Dakta' Mwigulu Nchemba wanasogeza siku tu. Ni mizigo halisi. Kinana uko wapi?Waandame hawa.