Mawaziri Wasukuma

Mawaziri Wasukuma

Jamani mnatuaibisha! wenzetu wa Kilimanjaro hawana shida kama sisi, isitoshe hata wakiiba huwakumbuka wapiga kura wao (mf. Mramba, pia kumbukeni Msuya, Mama Malecela, Dr Mathayo anasaidia sasa huko Upareni)! pia kumbukeni Mzee wa Kiraracha naskia alipelekaga barabara kwao alipokuwa waziri wa mambo ya ndani ukiachia mbali kuishikisha adabu polisi!

toka lini mwizi akawa na huruma kwa watu wa kwao?ebu nielezeni huyo mramba ni kipi hasa amekifanya huko kwao kiasi kwamba ROMBO watampenda daima? kumbukeni MRAMBA amefutwa kazi na wanarombo kwa kosa la UFISADI, angelikuwa amewakumbuka kwao leo ungekuta bado ni mbunge. Hongera wana rombo kwa kutuondolea huyu fisadi waacheni WASUKUMA wamkumbatie Chenge na Ngeleja.
 
Kwani waziri anateuliwa kwa maendeleo ya eneo lake la asili au kwa taifa zima. Kumlalamikia Ngeleja kuwa hajasambaza umeme Sengerema kwa kuwa ni waziri wa nishati, ni kumfanya anuke ukabila au ukanda.

Noana tunapotelea ndani ya tafsiri ya ukabila. Hawezi endeleza taifa zima kwa mpigo, ni kitu cha kawaida kuanzia kwenu. Angalia sasa na kimbelembele chake kutaka kuilipa DOWANS, sote sasa tunamjua kwa hilo na wala tusimgemlaumu kwa ukabila angepeleka hizo pesa kwenye jimbo lake kwani lipo TZ.
 
Ndio maana nikasema hoja hii inanuka shuzi la ukabila na watu wakanishambulia. Haiwezekani kuwa na mawaziri wa kanda, labda mpaka itakapokubaliwa Tz iwe na majimbo.
mie sikubaliani na mambo ya kabila fulani likishika wizara basi faida ya hiyo wilwizara inahamia kabila hilo, huu ni upuuzi. Cha msingi hapa resources zinazopatikana eneo fulani angalau ndo zitumike kuleta maendeleo yale. Ngeleja atumie madini kuleta maendeleo ya kanda ya ziwa siyo kujipendelea kwa umeme. Kwanza thread hii ifutwe hatutaki ukabila hapa japo hautakaa ufanyekazi kwa tz.
 
toka lini mwizi akawa na huruma kwa watu wa kwao?ebu nielezeni huyo mramba ni kipi hasa amekifanya huko kwao kiasi kwamba ROMBO watampenda daima? kumbukeni MRAMBA amefutwa kazi na wanarombo kwa kosa la UFISADI, angelikuwa amewakumbuka kwao leo ungekuta bado ni mbunge. Hongera wana rombo kwa kutuondolea huyu fisadi waacheni WASUKUMA wamkumbatie Chenge na Ngeleja.

Marytina, kauli nzito hiyo!! Unajaribu kusema kwamba wapiga kura wa Chenge na Ngeleja ni mafisadi? Au unajaribu kusema ni mambumbumbu hawajui madhara ya ufisadi? Unajuaje kama kura hazikuchakachuliwa, na kwamba siyo kosa lao?
 
Hivi huwa najiuliza kwa nini mawaziri wasukuma wanakuwa waadilifu kwenye kazi zao wakitumikia serikali ipasavyo na kusahau majimbo yao?
Kwa nini hawatumii nafasi yao kuleta maendeleo majimboni? Utaona kama waziri Ngeleja yupo nishati na madini lakini miaka mitano ishapita kule kwao sengerema hata kusogeza umeme kidogo vijijini ameshindwa? kuna miji inakuwa sana kule mfano kutoka sengerema kuna nyehunge, nzela .katwe , kahunda kwa nini mawaziri wameshindwa kupeleka umeme kule wakati miji imepanuka imekuwa mikubwa kuliko hata sengerema mjini yenyewe?
Nilienda kikazi huko nilishangaa kama mbunge wao ni waziri wa nishati na madini. na ni hivyohivyo kwa hata aliyepita. hawaoni wenzao wa kilimanjaro umeme mpaka vijijini?
kwa kweli wana JF naomba kuwakilisha mada

Mkuu, naunga mkono hoja yako kwamba ili maendeleo yapatikane nchi nzima kwa usawa basi wabunge wote wawe mawaziri ili wapate fursa ya kupeleka rasilimali za taifa kwenye majimbo yao. Reshuffle ifanyike kila baada ya muda fulani ili kuhakikisha kwamba mbunge husika anashika wizara zote kabla ya kumaliza kipindi chake. Ili jimbo lake lipate huduma zote, yaani maji, barabara, afya, elimu, kilimo, etc.

Hivi kwa nini mikoa ya kusini bado ni maskini zaidi ya mikoa ya kaskazini wakati Mkapa alikuwa rais kwa miaka kumi? Hivi Umeme wa kilimanjaro uliletwa na wabunge mawaziri au zao la kahawa na makanisa? Hivi mashule kilimanjaro yamejengwa na serikali au wamisionari, makanisa, na kipato cha kahawa? Orodha ndefu kidogo, endeleza.

Kwa hiyo, waziri fulani akiingia kwenye wizara akakuta aliyemtangulia alitumia kila kitu kuendeleza jimbo lake na huyu mpya akakosa rasilimali za kupeleka jimboni kwake, basi wananchi wa jimbo lilokosa rasilimali waanzishe chuki na mapigano na wananchi waliopata! Wafipa wafunge safari wakazipige na wasambaa. Njiani wapishane na wapogoro wanakwenda kuzipiga na wanyaturu. Hivyo hivyo nchi nzima.

Naam, kila waziri aendeleze kwao?
 
ACHA UTANI WEWE HAKUNA VIONGOZI WALIOFAIDI NCHI HII KWA KUJICHUKULIA MALI NA KUTETEA UFISADI KAMA WANYANTUZU NA WAKWE ZAO WASUKUMA
-ANDREW CHENGE
-WILLIUM NGELEJA
-CHEYO (WAZIRI YULE)
-EDWARD HOSEA
-nk
 
Tuache unafiki hapa wa ukabila. Magufuli kapeleka barabara kwao..na inatusaidia wengi sana tukiwa tunaenda vijijini kwetu. I care less..hiyo barabara ingestahili kwenda wapi..cha muhimu iko Tanzania na inawasaidia watanzania! Maendeleo hayawezi kuja kwa mpigo. Lazima tuanze na sehemu moja moja..ndo maana nawakubali wakenya..unakuwa fisadi lakini una invest nyumbani! Hivi unadhani kama hizi billions za DOWANS wangekwapua hazina harafu wakazidumbukiza kwenye uchumi kwa kutengeneza miradi ya ajira..tungekuwa wachungu kiasi hiki? Tatizo la akina Ngeleja and co. ni kuiba na kupeleka nje kuwaneemesha wengine. Ndo maana tunawaona viongozi wa TANZANIA kama criminal network fulani hivi...

Mi siyo Mchagga, but I give these people maximum respect! wanajua maisha ni nini...ndo maana hata kama ana ghorofa Masaki..atajitahidi hilo ghorofa alijenge pia kijijini....na trickle down effect ndo inaanzia hapo..mana atavuta umeme, maji..nk..na wananchi majirani..watavuta maana kuunganisha nguzo itakuwa nafuu sana kwa ukaribu! You dont need kusoma economics kujua hivi vitu.

Ushauri wangu: Kama unaweza kajenge nyumba nzuri kijijini (siyo Dar tuu-maana wengine hata likizo wanaogopa kwenda kwao maana hawana pa kufikia..))..vuta umeme, maji..pitisha harambee..mjenge barabara...hata kama haupo wananchi wanatoka kiuchumi namna hiyo. Usisubiri kila kitu eti serikali ya CCM!

Masanja
 
. I care less..hiyo barabara ingestahili kwenda wapi..cha muhimu iko Tanzania na inawasaidia watanzania! Maendeleo hayawezi kuja kwa mpigo. Lazima tuanze na sehemu moja moja..
Masanja

Nakubali kuwa maendeleo hayawezi kuja kwa mpigo, lazima yaanzie sehemu moja...lakini sehemu hiyo siyo lazima iwe nyumbani kwa waziri. Kufanya hivyo ni dalili ya taifa kukosa maeneo ya kuyapa kipaumbele. Tabia ya mawaziri kupendelea kwao ndio inapelekea taifa kukosa mabilioni kwa sababu tu hakuna barabara ya kueleweka toka Dar hadi Kigoma, ambapo mizigo yote ya Burundi, Congo (mashariki) ingepitia kwetu. Kisha faida ambayo ingepatikana ndiyo wangechota kujengea kwao.
 
ACHA UTANI WEWE HAKUNA VIONGOZI WALIOFAIDI NCHI HII KWA KUJICHUKULIA MALI NA KUTETEA UFISADI KAMA WANYANTUZU NA WAKWE ZAO WASUKUMA
-ANDREW CHENGE
-WILLIUM NGELEJA
-CHEYO (WAZIRI YULE)
-EDWARD HOSEA
-nk

Kama una maanisha Gideon Cheyo aliyekuwa waziri wa ardhi... Huyu si msukuma.
Ni mndali na alikuwa mbunge wa Ileje, Mbeya.
 
Mtu yeyote aliyesoma hii si hoja ya kujadili. Huu ni ukabila. Kwanini ngeleja hakuleta umeme kama Mbunge na si kama Waziri.Maana hata singida na Manyara wanamsubiri yeye apeleke umeme kule.
Mbona Hanang mpaka leo haina umeme wa kutosha bara bara ndo usiseme.Sumaye alikuwa waziri mkuu miaka kumi. Sisi hatulalamiki?
 
Thread imekaa kimtego kweli hii!

Ila kwa vile hapa ndani huwa tunaweza kujadili hulka za watu kwa mfano wanawake wa kirangi, kihaya n.k naomba kusema wasukuma wanahulka moja MBAYA.
Ile ya kuwa carefree, msukuma hata kama anapelekwa gerezani ukimwuliza Kinehe (vipi?) atasema Nduhu Tabu (shwari tu).
Sasa kama kwenda Butimba wasema ni shwari ujue tatizo ni kubwa kuliko linaloonekana.

Kazi ya mbunge ni kusimamia serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi. Sasa kama mbunge ni Waziri watu wanamtarajia afanye zaidi ya mbunge wa kawaida.

Likija swala la national priorities ni nani atabishi kwamba kanda ya ziwa na Dar es salaam zina mchango mkubwa sana kwa pato la taifa lakini Dar Mwanza hazikuwa linked na barabara ya lami mpaka miaka 49 baada ya uhuru.

Inaweza kuwa si ukabila lakini something is wrong somewhere!!
 
Mzee Vijisenti na Mapesa ni WANYATUNZU,sio wasukuma!!!!!!!!

Mmakonde, nadhani huwajui wasukuma wewe! Ungefanya uchunguzi kabla ya kuandika. Wanyantuzu ndio wasukuma halisi katika nchi ya usukuma. Hawa asili yao ni Ethiopia, walikuja zamani sana na kuanza kutapakaa katika maeneo mbalimbali huko kanda ya ziwa. Baadae walikuja kuchanganyikana na Wanyankore kutoka Uganda, lakini lugha ya kisukuma ikawa dominant.

Kwasasa wasukuma ni kabila kubwa lenye maeneo yanayojulikana rasmi kama Ntutsu, Kabila, Usimao, Nera nk Mimi nimekaa huko kwa miaka mingi na nikawa nazungumza na wasee wa kisukuma ndio nikaanza kuwafahamu zaidi. Sehemu za Mwanza kuna mchanganyiko mkubwa wa Wakerewe, Wazinza, Wasumbwa na kwa kiasi Wakuria, Waruli, na Wakara. Upande wa Shinyanga kuna mchanganyiko wa Wagadzabe, Masai, Wanyiramba na Wanyaturu.

Tukija kwenye maendeleo, ni kweli wasukuma wako nyuma kwasababu walikuwa wafugaji na hawakupenda kwenda shule. Kutokana na mabadiriko ya ufugaji sasa tunaona wasukuma wameanza kwenda shule. Sasa kuna wasukuma wameanza kupata PhD na kuitwa Dr Magufuli, Dr Hosea, Dr Pius Ng'wandu, Dr W Shija, nk
 
Mzee Vijisenti na Mapesa ni WANYATUNZU,sio wasukuma!!!!!!!!

Mramba si mchaga ni mrombo,Mzee wa Kiraracha si mchaga ni mmarangu,Mbowe si mchaga ni mmachame,C Chami si mchaga ni Kibosho duh list ni ndefu.

Mkuu mmakonde ndani ya kabila moja kunakuwepo na vijikabila vidogo vidogo vinavyounda kabila kubwa.Mfano kabila la wapare utakuta kuna wagweno ambao hata lugha yao ni tofauti na mpare wa Same bado wate wataitwa wapare.Wachaga wapo wamarangu,wamachame,wahuru,warombo,wakibosho wote hawa wana lugha zao lakini bado wataitwa wachaga.
 
Na kwa wahaya kuna wanyambo........
 
Mzee Vijisenti na Mapesa ni WANYATUNZU,sio wasukuma!!!!!!!!

Bebhe nang'ho! Hao wote ni wasukuma. They all speak sukuma. Ila matamshi yanatofautiana kidogo. Ni kama American English na British English.
 
Hili la Wabunge kuteuliwa kuwa Mawaziri, manaibu au Wakuu wa Mikoa ni moja ya mambo ambayo KATIBA yetu MPYA lazima iyapige marufuku haraka. Hili suala la mtu kuendeleza "kwao" wakati yeye ni waziri wa serikali ya Tanzania nzima halitoi picha nzuri.
 
sasa kama Mawaziri ni Wabunge unategemea nini? ila mie ninadhani hata kama wasipokuwa Mawaziri ndg zetu wa Kilimanjaro watasaidia tu majimbo yao kama kazi zao zinavyowatuma! angalia mama Malecela na kiwanda cha tangawizi!
 
Naungana mkono na CHADEMA katika kuleta serikali za majimbo!!!!!
 
mh mtoa mada! umesahau mkapa na lile daraja eee, umesahau msuya na umeme mpaka kwenye miti eee na unaendelea kusahau kikweye na bandari kule bagamoyoo?? hawa wenzetu wamezubaa tu bana

Back
Top Bottom