Mawaziri Wasukuma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri Wasukuma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gaga, Jan 26, 2011.

 1. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hivi huwa najiuliza kwa nini mawaziri wasukuma wanakuwa waadilifu kwenye kazi zao wakitumikia serikali ipasavyo na kusahau majimbo yao?
  Kwa nini hawatumii nafasi yao kuleta maendeleo majimboni? Utaona kama waziri Ngeleja yupo nishati na madini lakini miaka mitano ishapita kule kwao sengerema hata kusogeza umeme kidogo vijijini ameshindwa? kuna miji inakuwa sana kule mfano kutoka sengerema kuna nyehunge, nzela .katwe , kahunda kwa nini mawaziri wameshindwa kupeleka umeme kule wakati miji imepanuka imekuwa mikubwa kuliko hata sengerema mjini yenyewe?
  Nilienda kikazi huko nilishangaa kama mbunge wao ni waziri wa nishati na madini. na ni hivyohivyo kwa hata aliyepita. hawaoni wenzao wa kilimanjaro umeme mpaka vijijini?
  kwa kweli wana JF naomba kuwakilisha mada
   
 2. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,539
  Trophy Points: 280
  Akishakua waziri under CCM Babylon system,interests za jimbo zinasahaulika,kwani siku zote atataka kutimiza yaliyo mema kwajili ya mabosi zake. Anasahau mabosi wake wa ukweli ambao ni wananchi waliomweka uongozini.

  Ndo mana tunahitaji katiba mpya itakayoweka bayana kua waziri hapaswi kua mbunge. Ili mbunge atimize wajibu wake kamili kama mbunge. Na pia kuepuka muingiliano wa mihimili ya dola (yani serikali,executive,na bunge).
   
 3. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mawaziri wasukuma ni wabinafsi, Chenge et lal, kila kitu nduhu tabu!:disapointed:
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa ila mbona mawaziri wa kilimanjaro na kwingineko wameweza kufanya maendeleo huku wakiendelea kumtumia mwajiri wao. mtu akitoka vijijini moshi akaja mjini hashangai umeme wala bomba la maji ngoja atokee huko mamwanza na masengerema
   
 5. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  kama wasukuma wangekuwa wanakumbuka kwao usukumani kungekuwa mbali saaana hebu hesabu ni mawaziri wangapi wameshika nyadhifa toka uhuru wengine hata nyumba hawajajenga kwao. Mbali na uwaziri pia wasukuma wenye nyadhifa za juu ka ukurugenzi, ukuu wa idara ila nao bure kabisa
   
 6. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Rafiki mimi ni msukuma lakini naomba kutofautiana na wewe kidogo. Mawaziri wasukuma sio wote ambao ni waadilifu. Mfano Chenge huyu ni mwizi na mtovu wa nidhamu wa hali ya juu na wote tunajua hilo. Maghufuli japo si kwa 100 % ana nafuu na kazi zake zinaonekana na huko kwao kawapelekea barabara nzuri sijui mengine. Ngeleja sioni uadilifu wake hata kidogo zaidi ya kuwepo pale wizarani kuendesha miradi ya bosi wake Rostam Azizi aliyempa Ubunge na huo uwaziri. Maige sina data zake kamili.
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kathread haka kananuka kiasi, mhhh!
   
 8. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  bale tu lemba nho!
   
 9. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It is true! Generalization ya Gaga si sahihi, mi nadhani alipaswa kuleta hoja ya kwanini Ngeleja anashindwa kupeleka umeme jimboni mwake? Naamini kwa nafasi yake ni rahisi ku-facilitate hilo huku akitekeleza majukumu ya Taifa!
   
 10. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  halafu kama mnachunguza vizuri sio Ngeleja tu anaharibu hata wenzake waliotangulia! kama Chenge alishiriki kuwapora Wasukuma wenzake ardhi yenye rasilimali ya madini kuwapa wawekezaji kwa mikataba isiyo na manufaa akiwa kama Mwanasheria Mkuu! Pia akiwa kama Waziri wa Miundo Mbinu Chenge huyo huyo alishiriki pia kuiuza TRL kwa kampuni ya kilaghai ya Rites zaidi ya hapo akagonga Wasukuma wenzake na gari sasa hatujui kama alitumwa maana alilipa laki mbili kama faini akaachiliwa! cha ajabu zaidi akashinda Ubunge kwa kishindo! Mbali ya hayo ukiacha ndg zetu Wasukuma hata wenzetu Nshomile hawako nyuma kuna wakina Karamagi pia walileta TICTs na mikataba ya kifisadi ya kusaini hotelini ughaibuni! Ukiachilia mbali ukweli usiofichika kuwa wako kwenye sehemu nyeti sasa katika serikali hii ya Kikwete yaani Ukatibu Mkuu na Ukurugenzi, utendaji wao na elimu zao ni tofauti yaani elimu inawekwa pembeni inabaki kulamba makalio ya mafisadi na kushibisha matumbo!

  Angalia type ya Silver Rweyemamu, na Mkandara hapo UD! Pia watu kama mama Mongela amekuwa Mbunge miaka nenda miaka rudi hamna cha maana alichofanya huko Ukerewe na mavyeo yoote aliyopata kuwa nayo! Mpaka najiuliza hawa watu na kuelimika kote, tatizo ni nini haswa? hawana uchungu na nchi hii? walio wasafi toka mitaa hiyo ni Dr Magufuli na Prof. Tibaijuka (ambaye yeye bado tunampima) tu! Jamani mnatuaibisha! wenzetu wa Kilimanjaro hawana shida kama sisi, isitoshe hata wakiiba huwakumbuka wapiga kura wao (mf. Mramba, pia kumbukeni Msuya, Mama Malecela, Dr Mathayo anasaidia sasa huko Upareni)! pia kumbukeni Mzee wa Kiraracha naskia alipelekaga barabara kwao alipokuwa waziri wa mambo ya ndani ukiachia mbali kuishikisha adabu polisi! Mbali na hayo hata watu wa Mbeya wanatuacha mbaali sana! angalia wakina Prof. Mwakyusa na wenzie walivyopigania mpaka uwanja wa Songwe unajengwa! hospitali ya Mbeya pia imeboreshwa na mambo chungu nzima ya maendeleo! Sie wa lake Victoria tumelogwa!
   
 11. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kwa kweli ni kurogwa na mganga kafariki. nimeshangaa sana, anashindwa nini kutumia madaraka aliyonayo kuweka umeme hasa kwenye miji inayokua kwa kasi vile?
   
 12. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  tatizo pia ni kwa sisi wananchi......we sukumas dont question
   
 13. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mzee Vijisenti na Mapesa ni WANYATUNZU,sio wasukuma!!!!!!!!
   
 14. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii hapa ni kama unaongelea UKATOLIKI na ULUTHERI wote ni WAKRISTO........
   
 15. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Anachowaza ni kulipa deni la Dowans, sasa akishalipa hiyo pesa ya kuleta nguzo Nzela itatoka wapi?
   
 16. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mnuko wa shuzi la ukabila.......
   
 17. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  kwa mtindo huu watu watakuwa hawaongelei under performance ya Wabunge wa eneo flani kwa vile ni kabila flani! acha narrow mindedness!
   
 18. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwani waziri anateuliwa kwa maendeleo ya eneo lake la asili au kwa taifa zima. Kumlalamikia Ngeleja kuwa hajasambaza umeme Sengerema kwa kuwa ni waziri wa nishati, ni kumfanya anuke ukabila au ukanda.
   
 19. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145

  Hivi kila waziri akipeleka huduma zinazotolewa na wizara yake jimboni kwake tu na majimbo yasiyokuwa na mawaziri yatasalimika kweli? serikali ina vipaumbele vyake, inapanga nini kiende wapi na wakati gani, sasa huo ubinafsi wenu eti ngeleja kwakuwa ni waziri wa nishati basi apeleke umeme kwenye vijiji vya kwao hata kama siyo kipaumbele cha serikali. Si unakumbuka mramba alivyozodolewa alipotaka kupeleka barabara huko jimboni kwake bila maelezo ya kutosha?

  Siungi mkono hoja.
   
 20. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndio maana nikasema hoja hii inanuka shuzi la ukabila na watu wakanishambulia. Haiwezekani kuwa na mawaziri wa kanda, labda mpaka itakapokubaliwa Tz iwe na majimbo.
   
Loading...