Mawaziri wanatuficha nini wanapotetea kujitoa kwenye Mpango wa Uendeshaji Serikali kwa uwazi?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Mbunge wa viti Maalum Grace Tendega aihoji serikali kujiondoa kwenye mpango wa uendeshaji kwa uwazi shughuli za serikali akisema jambo hilo lilikuwa ni silaha muhimu katika kupambana na rushwa.

Ripoti zimekuwa zikionyesha vitendo vya rushwa kuongezeka na ripoti ya CAG kutofanyiwa kazi kwa walioshiriki kwenye ubadhirifu wa mali za umma kushughulikiwa, huku serikali ikizidi kujiondoa kwenye kwenye mambo ambayo itawaonesha wananchi na kuwathitishia kuwa ina nia na kufanya mambo kwa uwazi bila kificho.

Je, kwa kufanya hivi serikali haioni kama ina mkono wake kwa sehemu kubwa katika kuchangia vitendo vya rushwa na ufisadi kushamiri?

========

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Grace Tendega amehoji ni kwa nini Serikali iliamua kujiondoa kwenye mpango wa uendeshaji wa Serikali kwa uwazi wakati silaha kubwa ya kupambana na rushwa ni uwazi.
Tendega amehoji leo Jumatano Novemba 8, 2022 wakati akiuliza la msingi bungeni.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndegembi amesema uamuzi wa Serikali kujitoa OGP haujaathiri uendeshaji wa Serikali kwa uwazi.

Amesema kwa kuzingatia ukweli kwamba Serikali inao utaratibu wa ndani wa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi wakati wote kwa kuwa na vyombo na Taasisi zilizokasimiwa majukumu ya kusimamia na kufuatilia Sera ya Uwazi na Uwajibikaji.

Amevitaja vyombo hivyo ni mfano Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Tume ya Utumishi wa Umma.

“Suala la kujiunga na OGP ni hiari kwa nchi mwanachama na vilevile inaweza kujitoa kwa hiari. Kwa msingi huo Serikali iliamua kujitoa kwa hiari,”amesema.

Amesema kwa ngazi za kimataifa, Serikali imeendelea kuwa moja ya nchi zilizoridhia mfumo wa kukaguana wa nchi za kiafrika APRM (African Peer Review Mechanism) ambao ulianzishwa mwaka 2003 na kamati ya wakuu wa nchi za kiafrika.

Mwananchi.
 
Kuna msemo kwenye kabila fulani unatafsirika kama " fumba macho nikuibie"
 
Back
Top Bottom