Mawaziri wa rais Magufuli wafutika kiaina!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,906
2,885
kulikua na mazoea ktk utawala wa awamu ya nne kwa baadhi ya mawaziri kuonekana kama mawaziri wenye utendaji uliotukuka kiasi kwamba kuna wakati ccm walipita kwa wananchi kuwanadi wakiwatumia kama mfano wa kuonyesha uhai wa serikali ya awamu ya nne awamu hii hali ni tofauti sana kwani hakuna yeyote anaeonekana kuchomoza akamzidi walau majaliwa ukiachilia mbali rais mwenyewe mawaziri wote chini ya magufuli wanaonekana wa kawaida sana unadhani tatizo lilikua udhaifu wa rais tulie kua nae wamepunguza utendaji changamoto zimepungua au wanafanya kazi ila wamezidiwa!?
 
Mzee wa msoga njoo huku kuna uzi unakuhusu, au tuma Kijana aje akusaidie kujibu najua upo nje ya nchi
 
Waandishi wa habari wamegomea maigizo ya hawa wasanii, kwa hiyo kwa kukosa support ya waandishi wameamua kupiga kimya.
 
Zamu ya wakuu wa wilaya sasa, makonda kishachukua mkoa, sasa sifa zimehamia kwa mkuu wa wilaya ya iringa, sijui anaitwa nani yule, full sifa
 
nguvu kubwa ya jpm ameielekeza kwa wakuu wa mikoa ndo mana mawaziri kama hawapo vile
 
Ndiye yule aliyekuwa anaongea na waziri Huku akiwa amesimama katikati ya dimbwi la maji??
 
Kuchomoza kumzidi mwengine hapo unaongelea "Kiki" na "sifa" which is irrelevant na matarajio ya wananchi, rais au wazir ataibuka kutolea ufafanuzi jambo lililo na msingi na sio mashindano kama unavyoaminisha watu
 
Muingiliano wa kazi za rais na mawaziri ndio unaofanya tusahau kama kuna mawaziri!
Magufili ni Rais pia ni Waziri wa kila Wizara!!Sijapata ona serikali inayo endeshwa kiajabu kama hii yetu!

Head of the State kachukua madaraka yoye toka kuwa mchumi na kiongozi wa bodi za kupanga mishahara ya watumishi kulingana na inflation hadi kuwa Chief Justice kuwafunga wasio na kazi hadi kuwa Waziri Mambo ya ndani kukamata wacheza bao hadi kuwa waziri wa Fedha kukagua bandarini na mengineyo mengi!
 
Back
Top Bottom