Mawaziri wa JK wapeana kavukavu mbele ya wananchi: Ni Mkulo na Magufuli

Sikutaka ku comment hapa hadi nisikie kauli ya TANESCO ama wizara ya nishati na madini.
 
Kweli mkuu kwani magezeti watu tumeisha soma sasa mambo ya kurudia yanini ni vizuri ndani ya JF tukapata habari mpya ambazo bado hazijatoka kwenye magazeti(za leo leo)

Hamtatutendea haki kwa sisi ambao hatuko Tanzania
 
mimi sina tatizo na uamuzi huu wa maghufuli. yawezekana memo zilishaandikwa lakini no action.
 
4 sure, mkulo bonge la mzigo tz, i wish jk atoe tamko ata kesho kuhusu iii mifisadi

Atajitolea je na yeye kauli wakati nae yumo maana asingekuwemo asingeyafumbia macho yote hayo yanayofanyika wazi na mchana kweupeee
 
..huu sasa ni upuuzi.

..i dont care uko kwenye serikali ya CCM au CDM lakini mawaziri hawapaswi kulaumiana kwenye vyombo vya habari.

..huyu Magufuli ni domo kaya, hana nidhamu.

Mbona na akina sita nao walikuwa wakilumbana? inaonyesha ni jambo la kawaida kwa serikali ya magamba na bado tutashuhudia mengi, bado malumbano ya rahisi na mawaziri wake!
 
Ndugu yangu unauliza habari za Ngurudoto? kule wailienda kujifunza udaku, umbea, mipasho na kikubwa zaidi wizi. kwa hayo yanayotokea mi wala sishangai, maana mkuu mwenyewe yupo yupo tu.
 
Tuwe wakweli hata kama mtu ana makando kando yake lakini Pombe Magufuli ni jembe, ni mtendaji haswaa! Wengi wanao mwandama au kumuhujumu, hasa viongozi wenzie, ni hofu juu ya uchapaji kazi wake. Tumwombe Mungu ili Jakaya amrudishe tena katika baraza la mawaziri hasa katika wizara aliyopo sasa au hata uwaziri mkuu.

Kibanga Msese

Ole wake JK asimrudishe Masolex kwa baraza la mawaziri.Tunamjua KJ ana bifu sana na Masolex,kwanza kumpanga kwake kwenye awamu hii inayoishia aliogopa maswali,ile iliyopita alimweka kwenye vitoweo,hivi wtz wenzangu,jembe kama Masolex ni wa kuweka kwenye vitoweo?SHAME ON U KJ,unalikoroga sana ila mwisho wako ni aibu KUUUBWA INAKUSUBIRI.
 
Magufuli ni kiongozi mzuri,ila mara nyingine maadili ya uongozi anayakosea. Sio maadili mema kukaripiana na mwenzako wa kazi hadharani. Ni huyuhuyu Magufuli aliyewaambia wananchi wapige mbizi kama hawataweza kulipa nauli ya sh.200 kwa ajili ya kivuko.
 
Tuwe wakweli hata kama mtu ana makando kando yake lakini Pombe Magufuli ni jembe, ni mtendaji haswaa! Wengi wanao mwandama au kumuhujumu, hasa viongozi wenzie, ni hofu juu ya uchapaji kazi wake. Tumwombe Mungu ili Jakaya amrudishe tena katika baraza la mawaziri hasa katika wizara aliyopo sasa au hata uwaziri mkuu.

Kibanga Msese
Ha ha ha
 
Back
Top Bottom