Mawaziri wa JK wapeana kavukavu mbele ya wananchi: Ni Mkulo na Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wa JK wapeana kavukavu mbele ya wananchi: Ni Mkulo na Magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, May 3, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tanzania Daima

  Mawaziri wa JK watishana


  na Ratifa Baranyikwa

  HALI ya utendaji kazi ndani ya Baraza la mawaziri imeendelea kuwa tete baada ya mmoja wa mawaziri waandamizi kumpa mwenzake muda wa siku saba kutekeleza matakwa yake, vinginevyo watafikishana mbali.

  Akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi, na daraja lililopo eneo la Tangibovu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, alimshambulia hadharani Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo na kutishia kumshitaki kwa Rais Kikwete ikiwa hataruhusu kutolewa kwa vifaa vya ujenzi, mali ya Kampuni ya Strabag ya Ujerumani vilivyozuiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA).

  Lakini Waziri Mkulo aliiponda kauli ya Waziri Magufuli, akidai kuwa amekwenda kinyume cha utaratibu wa kazi kwa kutishana kupitia magazetini, na kwamba namna pekee ilikuwa kufuata taratibu.

  Akizidi kuishutumu Wizara ya Fedha, Magufuli alidai kuwa hawezi kubebeshwa lawama za kuchelewa kwa ujenzi wa barabara hiyo, na hatakubali kuadhibiwa kwa uzembe na makosa ya watendaji wengine wa serikali.

  Kauli ya Magufuli ilikuja baada ya kukuta kazi za ujenzi zimesimama, na ndipo Meneja wa kampuni hiyo ya ujenzi, Frank Rohde, akamweleza kuwa kuna vifaa yakiwamo makatapila vimezuiliwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam, kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo fedha.

  “Hili ni agizo la rais mwenyewe kuhusu upanuzi wa barabara hizi ili foleni ziishe na waziri analifahamu, nitaongea naye kama akishindwa basi nitamchongea kwa rais, Mamlaka ya Mapato (TRA) nayo nitaongea nayo,” alisema.

  Imebainika kuwa kampuni hiyo inaidai serikali fedha nyingi kama gharama za ujenzi, lakini katika namna ya kushangaza wamezuiliwa kuchukua vifaa vyao bandarini kwa madai ya kutolipa ushuru.

  “Kilichobaki sasa ni kuchongeana kwa Rais Kkwete ili mambo yaende vizuri, na ili kufanikisha ujenzi huo ni lazima kila mmoja atimize wajibu wake,” alisema.

  Alisema kampuni hiyo ya Ujerumani inakwenda na muda ili kumaliza mradi kwa wakati, hivyo hawataki kupewa vikwazo vyovyote.

  Kwa mujibu wa waziri, mradi huo unajengwa kwa manufaa ya wakazi wa Dar es Salaam, kwa kuwa utapunguza foleni kwenye jiji, lakini pia utakuwa ni mkombozi kwa taifa, hivyo ni mradi wa wote, hivyo hautakiwi kupewa vikwazo vyovyote vikiwamo vya wizara, Tanesco au TRA.

  Alifafanua kwamba kampuni hiyo inatakiwa kukaa kwenye eneo la ujenzi kwa muda wa miezi 36 na Wajerumani wanajua jinsi ya kujali muda, kwani hatua ya kupewa vikwazo kwa kampuni hiyo, inarudisha nyuma maendeleo ya wananchi wenyewe.

  Magufuli alilipa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) siku saba kun’goa nguzo za umeme kando kando ya barabara hiyo, na endapo watashindwa atazing’oa kwa nguvu.

  Waziri huyo pia aliwataka wananchi waliojenga eneo la barabara kubomoa makazi yao haraka iwezekanavyo, na wasidanganywe na mtu ikiwa ni pamoja na kwenda mahakamani, kwani hata wakichukua hatua hiyo hawana uhakika wa kushinda.

  Alielezea kuwa mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi eneo la Kimara hadi Kivukoni utagharimu sh bilioni 288, ambapo ujenzi wa barabara pekee utagharimu sh bilioni 240 na vituo vyake kugharimu sh bilioni 44.

  Alisema hata kama mabasi hayo yatashindwa kuletwa nchini, barabara hizo zitatumika kwa magari ya wananchi, ambapo mradi huo ukikamilika Barabara ya Morogoro itakuwa na njia nane.

  Mkulo: Sijui kitu

  Akihojiwa na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Waziri Mkulo, alishangazwa na mashambulizi dhidi yake akidai kuwa hajui lolote na kwamba kitendo hicho cha Magufuli ni kinyume cha taratibu za kazi.

  “Si utaratibu kwa waziri kuzungumza kwenye magazeti eti kusema atanishitaki kwa rais, kuna utaratibu wake… huo si utaratibu,” alisema Mkulo.

  Kadhalika alidai kuwa haelewi jambo lolote kuhusiana na kampuni hiyo, na hivyo hawezi kuzuia malipo wala kutolewa kwa mizigo yake bandarini na kwamba anayewajibika kuelewa masuala hayo ni katibu mkuu wa wizara.

  Jitihada za kumpata katibu mkuu wa wizara hiyo zilishindikana, na hata alipotafutwa Msemaji wa Wizara ya Fedha, Namsembaeli Mduma, simu yake ya mkononi iliita bila kupokewa.

  My take:
  Hivi maadili kwa viongozi ya Ngurudoto yaliishia wapi au ndo nini: huku nje twaona haya huko ndani kukoje????????
   
 2. M

  MAKAWANI Senior Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Its ok, but sithani kama kukopi na kupest habari za magazitini kama zilivyo ni sahihi kwenye JF
   
 3. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,654
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha haaaaaaaa kiranja mkuu anapokua msanii tutegemee nini kwa viranja wengine?

  But honestly; Mkulo ni mzigo kwa taifa
   
 4. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Hazina yenyewe imefulia vibaya sasa sijui watatoa wapi za kulipa...nchi hiii kweishneeeee
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  You are right. lakini naona ni starting point na inatuonesha kuwa mawaziri wetu ndio hivyo tena, kila mmoja ana lake, they do not work as government.
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ni sahihi
   
 7. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  aaaah kumbe ngumi hazikupigwa
   
 8. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkulo anajua anaondoka ,ndo maana hana mda wa kutekeleza hayo
   
 9. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kweli Magufuli ameishiwa...:tape:
   
 10. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,407
  Likes Received: 10,450
  Trophy Points: 280
  Huju jamaa anayeitwa Mkulo nilishamchoka siku nyingi sana!!
   
 11. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa hazina imefilisika rais asingekuwa anasafiri na bunge lisingeendelea maana posho ingekata.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Strabag jamaan wanataka kitu kidogo hao TRA na hii ndo bongo na mkiendelea kuleta za kuleta utashangaa migreda yenu wamechomoa tyres
  Hii ndo bongo sio Ujerumani
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160
  Three, two, one, ACTION . . . . , Cut!
   
 14. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  President has no complain on his Ministers ... !! Kwake utendaje wao ni wakutukuka ... kwani ameshawachukulia hatua gani? Kwani nani kawachagua ...!! Give Pez The break!!! ... yote yatapita kama upepo!!
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkullo atakumbuka nini cha kufanya wakati anabadilisha ndege? Vivyo hivyo Kitillya atanyanyuka na kuacha glass yake ya wine?
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  mkulo ana jua hana chake hapo ndio maana anajifanya ajui kinachoendelea.kaisha kula pesa zake hana habari.
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  TRA inashangaza sana ngano na sukari za bakhresa na metl zenye misamaha inapita mara moja,vifaa vya ujenzi wanazuia
   
 18. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Absolutely!
   
 19. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndo bongo hiyo mazee, mimi nilijua wakiingiza vifaa vya ujenzi msamaha moja kwa moja. Kumbe msamaha ni wale wa vifaa na mafuta ya madini, Bulyanhulu, Buzwagi nk
   
 20. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hah hah ... kama ni hivi? Really strange!!
   
Loading...