Mawaziri wa afya kutoka katika nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wana mikakati ipi ya pamoja katika kuhakikisha wanakabiliana na Corona?

View attachment 1380780

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu wa mwisho (last born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu;

Mawaziri wa afya kutoka katika nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) wamekuja na mikakati ipi ya pamoja katika kuhakikisha wanakabiliana ipasavyo na janga hili kubwa la mlipuko wa virusi vya Corona?

Au ndio tuseme urafiki huu wa nchi hizi sita (Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, South Sudan) ni katika wakati wa raha tu, ila kwenye shida kila mtu anapambana na hali yake?

Kama kuna mtu anataarifa juu ya mkutano wa viongozi (mawaziri) hawa ninaomba anijuze walikutania wapi na lini?

Je, Kuna hospitali yoyote ya pamoja (Designated Hospital) iliyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia watu watakaobainika kuonesha dalili za ugonjwa huu huko maeneo ya mipakani kama Namanga?

Je, kuna timu yoyote ya pamoja ya wataalam wa afya iliyowekwa (on standby) huko mipakani katika kukabiliana na hili?

Mwenye taarifa sahihi ninaomba anijuze tafadhali ndugu zangu.

KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Rais Mama Samia yupo Kenya leo hii
 
Back
Top Bottom