Mawaziri msaidieni Rais, ndiyo maana amewaamini

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
ELIMU ITOLEWE ZAIDI JUU YA MFUMKO WA BEI NA KATIZO LA UMEME.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kesho macho na masikio yatakuwa Dodoma kwenye mkutano wa CCM. Kabla ya mkutano huu mkubwa ninaomba nitoe changamoto kwa Wizara ya Nishati, Kilimo na Biashara.

Kumekuwa na katizo la umeme. Waziri amejitahidi kutoa ufafanuzi, lakini bado kuna manung'uniko.Hoja ya Mhe Makamba kuwa kuna matengenezo yanafanyika ndiyo maana umeme unakuwa wa mgao mara Kwa mara inawezekana ni kweli. Lakini huku chini wananchi hizi sababu hazieleweki sana, labda aongeze darasa zaidi Kuna siku wataelewa.

Kuna watu wengi wanafanya biashara kwa kutumia umeme. Kwa mfano watu wenye mashine za kusaga na kukoboa nafaka wanategemea umeme ili mashine zao zifanye kazi. Umeme unapokua haupo mashine hazifanyi kazi. TRA wanapokuja kukusanya mapato wanataka hela yao waliyokukadilia. Hawajui kama kuna wakati hukufanya kazi kwa nishati ya umeme kukosekana. Hapa wananchi hawatendewi haki. Ushauri wangu ni kuwa TRA ingetoa punguzo ambalo mtu alikadiliwa, hasa yule ambaye source of income inadepend umeme.

Changamoto nyingine ambayo wananchi wanapaswa kupewa Elimu ya kutosha ni bidhaa kupanda bei. Mawaziri na viongozi wote wanatakiwa kuwapa wananchi majibu yakina yasioacha Mashaka yoyote. Wananchi bado wanaamini pamoja na COVID 19 Bado zipo jitihada ambazo serikali inaweza kufanya.

Vita ya Urusi imeanza mwaka huu, lakini ukiangalia bei ya mbolea toka mwezi wa kumi ilianza kupanda bei. Sawa! Tu assume ni vita ya Urusi na Covid 19, kwa Wananchi wa Songwe na Mbeya wanatakiwa kupata uelewa kuwa kwa nini bei ya Mbolea Malawi na Zambia ipo chini kuliko Tanzania wakati mbolea yote inatokea bandari ya DSM? Kwa nini serikali isiweke ruzuku kwenye sekta hii mhimu? Malawi kwa mfano mbolea ni 85,000/= Tanzania ilifika mpaka 140,000/=

Sukari Kwa Tanzania ni 55000/= lakini Malawi ni 41000/= hata Zambia. Na kwa Bahati nzuri Malawi na Tanzania mzalishaji ni mmoja.

Mafuta ya kupikia Tanzania ukienda Tunduma ni Tshs 120,000/= lakini ng'ambo ya pili upande wa Zambia ni 105,000/=.

Hii ni mifano michache ambayo inatakiwa itusaidie kuibua hoja. Hoja hii ni mhimu sana kwa Wananchi wa kawaida. Wakati wanasiasa wanadai katiba mpya, tunatakiwa kwanza kuwa na mjadala mkubwa juu ya mfumko wa bei.

COVID 19 na Vita ya Russia ina madhara kwa Dunia nzima, lakini serikali inaweza kuchukua hatua za makusudi kama ilivyo Kwa nchi hizi mbili nilizotolea mfano.

Nilishawahi kutoa ushauri, na bado ninaendelea kutoa ushauri. Dunia kote maendeleo yanaletwa na mapinduzi ya kilimo. Kilimo ndicho kinapaswa kuangaliwa Kwa jicho kubwa. Kilimo hakitakiwi kufanyiwa siasa bali uhalisia. Wizara inatakiwa kuwa na kalenda ya kilimo Kwa kila mkoa. Ipo mikoa msimu wa kilimo ni June, unapowapa pembejeo October huwasaidii chochote. Ukisha fanya mapinduzi kwenye kilimo hatua inayofuata ni mapinduzi ya Viwanda. Viwanda huko unahitajika umeme. Ukizalisha Sana, ukawa na viwanda vingi lakini ukawa na umeme wa kukatika bila saa basi unakuwa sawa na hakuna chochote.

Mawaziri wa wizara hizi karibia wote ni vijana. Wanatakiwa kufikiria zaidi ya hapo kumsaidia Mhe Rais ili kutimiza ndoto zake.
 
Umeandika mambo mengi lakini mwisho ni mafisadi yote yamerudi kutafuna nchi
Mafisadi CCM hayajawahi kuisha hata siku 1,yapogo tu.Sikio la kufa
mNLPzh2J9M2Jussf.jpg
 
ELIMU ITOLEWE ZAIDI JUU YA MFUMKO WA BEI NA KATIZO LA UMEME.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kesho macho na masikio yatakuwa Dodoma kwenye mkutano wa CCM. Kabla ya mkutano huu mkubwa ninaomba nitoe changamoto kwa Wizara ya Nishati, Kilimo na Biashara...
Kama rais anakua na kidodomo cha kusema bei za vitu zitapanda, lazima zitapanda maana ana-speculate na yeye ndiye the most powerful....
 
Back
Top Bottom