Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 19,312
- 30,494
Hapo iko sawa... maana bi mkubwa sikumuelewa kabisa...Tatizo wewe mtoa mada hii hukumwelewa Ndalichako unaanza kukurupuka tu na kuanza kuwataja waheshimiwa bila kufanya uchunguzi walisoma mfumo gani wa elimu. Ndalichako kasema kama umefaulu vizuri form four ukaenda kusoma Ordinary Diploma/FTC katika vyuo vya Ufundi kama DIT ,TCA au MTC na ukafaulu vizuri huzuiwi kusoma degree utaratibu ambao unajulikana tangu mwanzo. Maana mtu anaweza pata division one au two aliyesoma Technical Secondary School /au Secondary za kawaida akaamua kwenda kusoma Ordinary Diploma/FTC na baadaye kuendelea Degree au kwenda kufanya kazi. Alichokataa mheshimiwa ni zile shule za kuunga unga kama vile form four failure kapata division four anaanza na foundation course, certificate ,Ordinary Diploma na baadaye Degree.Anachotaka mheshimiwa ni ule utaratibu tuliokuwa nao kama form four combination hazijakubali urudie tena mtihani upate pass za kukuwezesha kuendelea mbele.