Mawaziri kujibu au kujadili hoja za CAG kabla ya kupitiwa na bunge ni kituko cha awamu ya tano

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,196
Nimeona malumbano yakiendelea Bungeni na mitandaoni kuhusu hatua ya mawaziri kuamua *kujibu* au *kujadili* hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kabla hata taarifa yake haijajadiliwa na Kamati za Bunge za usimamizi (PAC na LAAC).

Baada ya malumbano na matamko kutolewa na wadau mbalimbali, wengi wakipinga na kulaumu hatua hiyo ya mawaziri, jana nimesikia Serikali na kiti cha Spika, kupitia kwa Naibu Spika, wakitetea kwamba mawaziri walikuwa *hawajibu* hoja za CAG bali walikuwa *wanazijadili* tu kama wananchi wengine!

Iwe ni kujibu au kujadili, haya ni maajabu mengine ya awamu hii ya tano.

Kimsingi hapa kilichofanyika na mawaziri ni muendelezo wa dhamira ya Serikali ya awamu ya tano kufifisha uhuru na haki ya wabunge na wananchi kuihoji Serikali kwenye uwajibikaji wake kwa mujibu wa Katiba na sheria.

*Mawaziri kujibu hoja za CAG*

Ni jambo la kushangaza sana kuona mawaziri wanajibu hoja za CAG kwa hesabu za Serikali mara tu baada ya CAG kuziwasilisha Bungeni kwa mujibu wa Kifungu cha 34 (2) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008. Mawaziri hawana mamlaka katika hatua hii kujibu hoja za CAG. Kwa hiyo wenyeviti wa PAC na LAAC, akina Zitto na wadau wengine wako sahihi kusema kwamba walichofanya mawaziri hawa ni kuvunja Sheria tajwa kifungu cha 38(1) na (2) inayotaka Kamati za PAC na LAAC kupitia kwanza taarifa hizo na kuwasilisha Bungeni maoni na mapendekezo yao. Aidha Sheria tajwa katika kifungu Na. 40 inawataka maafisa masuhuli kuandaa majibu ya hoja za CAG na maoni na maelekezo ya Kamati za Bunge na baada ya kuziwasilisha kwa CAG waandae taarifa ya utekelezaji na kuziwasilisha kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali (Katibu Mkuu Hazina) ambaye kwa kupitia kwa waziri wa fedha, atawasilisha majibu na utekelezaji wa hoja hizo Bungeni katika kikao kinachofuata cha Bunge kwa mujibu wa kifungu Na. 40(2)(a). Ni katika hatua hii (Bunge linalofuata) ndipo mawaziri wanaweza kutoa majibu ya utekelezaji wa hoja za CAG kama zilivyoandaliwa na maafisa masuhuli wao.

Kama sheria imeweka utaratibu wa kujibu hoja za CAG (kupitia kwanza kwa maafisa masuhuli) kama nilivyoeleza hapo juu, Serikali ikijibu kwa utaratibu tofauti (kama hivyo kupitia kwa mawaziri) itakuwa imevunja sheria. Nimemwona Ndugu David Kafulila naye kwa makusudi akitumia akili ndogo na kusema ati kwa kuwa sheria haisemi mawaziri wakifanya hivyo ni kosa basi hawakukosea! Sheria haihitaji kusema utaratibu mbaya, inasema tu utaratibu halali, ukifanya vinginevyo umeivunja sheria hiyo. Kwa hiyo mawaziri wanapojinasibu kwamba wamejibu hoja za CAG kuhusu mahesabu ya 2016/17 wamekosea na wamevunja sheria.

*Mawaziri kujadili taarifa ya CAG kabla ya Bunge*

Lakini hata kama watasema kwamba mawaziri hawakujibu hoja bali wamejadili tu kama wananchi wengine wa mitaani kwa mujibu wa kifungu Na. 39 ya sheria ya Ukaguzi, hii nayo itakuwa ni busara ya ajabu sana na kituko cha mwaka kwa mawaziri kujadili hoja za CAG ambazo hazijajadiliwa na Kamati husika za Bunge na Bunge zima na hazijajibiwa na maafisa masuhuli wa wizara zao. Kama walidhani hii ni busara basi ni busara inayopatikana awamu hii ya tano tu! Ati mawaziri wanajadili hoja za CAG kama wananchi wa mitaani? Hoja za wizara zao ambazo kiutaratibu na kisheria zinatakiwa kwanza zijadiliwe na Kamati za Bunge na Bunge zima kisha zijibiwe na maafisa masuhuli wao?

Ndiyo maana nasema kilichofanyika na mawaziri ni muendelezo wa dhamira ya Serikali hii kufifisha uhuru na haki ya wabunge na wananchi kuihoji Serikali kwenye uwajibikaji kwa mujibu wa Katiba na sheria. _It is a continuation of preemption, suppression and intimidation of people's and Parliament's rights to hold government to account._

Lakini hii pia ni kudhalilisha fani ya uhasibu na Ukaguzi na kudhalilisha nafasi na majukumu ya kikatiba na kisheria ya CAG. Hivi hii Serikali na hawa mawaziri wanataka CAG naye ajitokeze kwenye vyombo vya habari na kujibu "majibu" ya mawaziri ambayo hayajafanyiwa kazi na maafisa masuhuli kwa mujibu wa sheria ya Ukaguzi wa Umma kifungu cha 40?

Mimi kama mhasibu mwandamizi (Fellow Certified Public Accountant), kama alivyo CAG Prof. Mussa Juma Assad, ambaye ni kati ya maprofesa wachache sana nchini wa uhasibu (professor in accounting), nimetatizwa sana na dhihaka hii kwa _profession_ ya uhasibu na Ukaguzi. Na kama ningeweza kumshauri Prof. Assad ningemwambia ajiuzulu mara moja arudi UDSM kufundisha.

Dr. Makongoro Mahanga, FCPA.
17/04/2018
 
Kwanza niunge mkono hoja yako pili nami namshauri mwalimu wangu professor assad ajiuzulu tu arudi kufundisha.
Nimeamini asiyekujua hakuthamini kamwe yaani leo hii report yake inakosolewa hadi na akina Livingstone lusinde?? Na akina ummy mwalimu ? Professor assad ana heshimika sana pale udsm kwenye mambo ya accounting ukimkuta darasani anaongea English iliyonyooka lazima utamsikiliza tu
 
Back
Top Bottom