Mawaziri kuhamia majengo ya UDOM kwazua mjadala Bungeni. Wizara hazijapata hata viwanja vya kujenga

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Wizara ya katiba na sheria amabayo ilihamia Dodoma na kukaa kwenye majengo ya UDOM kwa kuwa CDA hawajajenga majengo na viwanja havijatafutwa bado majengo kumezua majadala leo bungeni mara baada mbunge Suzan Lymo kuuliza inakuaje miundo mbinu ya chuo inachanganywa na serikali.

Naibu waziri wa elimu Stella Manyanya alisema suala hilo ni la muda mfupi na CDA wanatafuta viwanja vya kujenga majengo ya wizara na kila wizara itakua na eneo lake.
Ila wabunge waliona kutoridhika na jibu kuwa ni ya muda mfupi na kulisikika kauli za kuzomea na kudai wamaepeleka wazee na hawana hata sehemu za kuweka wake zao




Msigwa naye amedai seriakli ilihamia Dodoma kwa kutafuta sifa, wakafanya kwa kukurupuka na ndio maana wanahangaika na majengo ya wanafunzi

 
Huu ni upuuzi wa hali ya juu! Unaacha majengo ya wizara unang'ang'ania kwenda kubanana kwenye majengo ya chuo!!
wapi walikuwa na majengo ambayo wameyaacha unayoyajua wewe.
 
Ni aibu kubwa na pia ni upuuzi wa kupindukia kwa watunga sera wetu, msiogope kumwambia rais kuhamia Dodoma bado na kuanzia sasa hadi 2019 waandae majengo ya kuhamia. Chakushanga eti CDA ndio inatafuta viwanja, kwani tangu ilipotangazwa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi hawakuwahi kutenga maeneo ya kujenga ofisi za serikali na makazi ya watumishi wa serikali?.
Eng. Manyanya anajibu kirahisi hivo, na kama UDOM kuna majengo yanabaki bila matumizi kulikuwa na sababu gani ya uanzishwaji wa utitiri vyuo visivyo na vigezo vya kuridhisha.
 
Wanang'ang'ania kukaa kwenye majengo ya chuo,pengine wanafunzi na walimu wa chuo hicho wanaishi kwa kupanga mitaani.
Sio kukaa mtaani tu, wafanyakazi walio wengi pale UDOM hata ofisi hawana wanabanana kwenye common rooms wkt majengo mengine wamepewa serikali.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Eng. Manyanya anajibu kirahisi hivo, na kama UDOM kuna majengo yanabaki bila matumizi kulikuwa na sababu gani ya uanzishwaji wa utitiri vyuo visivyo na vigezo vya kuridhisha.

May be yalijengwa ili wajanja wapate 10%
 
Imagine Wizara zote karibu nafikiri zina majengo yake Dar.
Wanayaacha majengo yao Dar matupu wanakimbilia Dodoma ambapo wengi wanaenda kujibanza UDOM..
What a shame??
Hizi ni akili au uwendawazimu..!!??
Kweli hii awamu ya mkurupukaji.
Fuatilia kwa ufasaha ndugu, asilimia 90 ya wizara zote hapa dar zimepanga. Ni wizara chache sana zenye majengo yake. Wizara yenye jengo lake mi naijua moja tu, Wizara ya Mali asili na Utalii
 
Fuatilia kwa ufasaha ndugu, asilimia 90 ya wizara zote hapa dar zimepanga. Ni wizara chache sana zenye majengo yake. Wizara yenye jengo lake mi naijua moja tu, Wizara ya Mali asili na Utalii
Sio kweli, Wizara ya Ardhi inajengo lake. Na pia hiyo Wizara ya Maliasili lile mengi ni la Idara ya Wanyamapori
 
Back
Top Bottom