Mawaziri Khamis Kagasheki na Thereza Huviza wagongana

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,961
2,138
na Asha Bani

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ametofautiana na Waziri mwenzake wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Thereza Huviza, akipinga hatua yake ya kuzifungia hoteli mbili za kitalii jijini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita, Waziri Huviza alizifunga hoteli za Double Tree iliyoko Masaki na Giraffe Ocean View iliyoko Kunduchi kutokana na kutotekeleza maelekzo ya wizara pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEC) na hivyo kuendelea kutiririsha maji taka baharini.

Akizungumza na Tanzania Daima, Waziri Kagasheki alisema kama wizara wameshtushwa na hatua hiyo ambayo aliita kuwa haikuzingatia sheria wala haki ya wawekezaji wa hoteli hizo. Balozi Kagasheki alifafanua kuwa, hatua ya kufunga hoteli hizo haraka kiasi hicho haina maslahi kwa taifa. Aliongeza kuwa, Waziri Huviza kabla ya kuchukua hatua, alipaswa kuwashirikisha Wizara ya Utalii, lakini cha kushangaza uamuzi huo ameufanya peke yake bila kujali kuwa kuna madhara gani kwa sekta ya utalii nchini. "Unajua ni uamuzi hatari sana na finyu wenye haraka, kwanza alitakiwa kuangalia ni wakati gani ambao anafanya uamuzi huo. Hiki ni kipindi cha likizo, ameshindwa kujua kweli kwamba wageni wengi wanapaswa kuja nchini?" alihoji.

Waziri Kagasheki alisisitiza kuwa, uamuzi huo hauungi mkono hata kidogo, kwamba waziri mwenzake ameshindwa kuzingatia kuwa hoteli zile ni za kitaifa ambapo katika kipindi hiki cha likizo wageni wengi wanatarajia kuingia nchini.
Aliongeza kuwa, hata mataifa ya nje na kwenye mitandao yao suala hilo limeingizwa na yanasomwa, na watalii wengi waliopanga kuja kutembelea Tanzania watashindwa kuja.

Alisema mikakati ya wizara ni kuhakikisha kuwa wanafanya kampeni za kuongeza watalii nchini, lakini endapo kutakuwa na mambo yanayokinzana, ni lazima watashindwa kufanikiwa kwa hilo. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Giraffe Ocean View, Nicholas Rabilo, alisema tayari wameanza kupata madhara kwani watalii kutoka Ujerumani waliokuwa wameomba nafasi ya kukaa hapo kwa mapunziko kwa wiki mbili, sasa wameahirisha.

Alisema hasara nyingine ni watu wa Kampuni ya simu ya TTCL waliokuwa na sikukuu ya familia kwa watu 100 ambao wameahirisha pamoja na Fair Competition wenye watu 50 na vile vile wameahirisha.

Bravo dada Dr Theresia Huvisa
Mh. Dkt Terezya Huvisa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - (Mazingira).JPG r

Kwa maoni yangu huyu Waziri Kagashekia kumbe hana huruma na afya za Watanzania, yeye interest zake ni wawekezaji na hao wageni (wazungu). Miaka 50 ya uhuru bado tunaabudu wawekezaji na wazungu? Shame!!!
 
Huyu Kagasheki atakuwa amechanganyikiwa kwa alitaka hoteli iwe wazi kipindi cha sikukuu ili wageni wamwage mavi kwa wingi baharini?

Hata hao watalii ambao hawajari usafi wa mazingira katika hoteli wanazofikia watakuwa na mapunguani basi.

Shame on you Kagasheki
 
Ee Mungu mrehemu mtu huyu, Kagasheki shame on you, hivi huwezi hata kuwaonea hata huruma watanzania wanaoathirika na uchafu huo? Kwani dsm ina hotel mbili tu? inaonyesha nn hii, au una hisa kwenye hzo hotel, na huko ndo vinakofanyika vikao vya kuiba twiga wetu. umeonekana mtupu kwenye mwanga wa jua!
 
Leo nimesoma kwenye magazeti Waziri wa Maliasili na Utalii akimpinga mwenzake wa Mazingira kuhusu ufungaji wa Mahotel kwamba ilikua ni makosa kuyafungia Mahotel yanayochafua Mazigira...mimi kwa mtazamo wangu nadhani Kagasheki amekosea sana sio tu kumpinga mwenzake ila pia kusema na kutetea uvunjifu wa sheria za nchi..
 
Na bado.... Kagasheki ataendelea kuleta matatizo sana. Ni suala la muda tu Makubwa na maovu ya ajabu yaja
 
Kagasheki hakupaswa kwenda public kumpinga mwenzake. Haya yangefanyika kiofisi bila sisi kuona wanapingana. Kiutendaji inakuwa ngumu sana kama kiongozi mwenzako anakupinga hadharani.

Sijui walisomea shule gani uongozi wa umma unavyokwenda. Kila mtu anasema kupitia kipaza sauti....
 
huyu babu kweli kaoza akili,, anafurahii watoto wetu wangeendelea kumeza vinyesi vya wazungu xmas wanapoogelea pwani ya bahari ya hindi.................... hii wizara ya maliasi naibu waziri na waziri wake wote wanamaslahii sana katika mambo mengi.......
 
kaza buti MAMA na kweli kina mama wanawezaa.. achana na hawa mafisadi wa maliasili zetu.... funga hoteli zote zinazotoa mavi baharini ....mana kipindi cha mpito wa kufungia hotel inaonekana alipokea posho huyo sa imemgeuka
 
Kagasheki ametia aibu sana ni wa kumfukuza kazi mara moja yaani yeye anatetea maovu haya mambo ya kienyeji sana, sisi tunamwambia Waziri Huvisa fanya kazi wala usiogope hao wenye njaa wasikutishe, wananchi tulishakua tunaona mawaziri kama Huvisa, Mwakymbe Magufuli wanafanya kazi sasa tena wenzao wanawahujumu aibu sana..
 
Kagasheki ametia aibu sana ni wa kumfukuza kazi mara moja yaani yeye anatetea maovu haya mambo ya kienyeji sana, sisi tunamwambia Waziri Huvisa fanya kazi wala usiogope hao wenye njaa wasikutishe, wananchi tulishakua tunaona mawaziri kama Huvisa, Mwakymbe Magufuli wanafanya kazi sasa tena wenzao wanawahujumu aibu sana..
Mkuu ni nani atakayemfukuza kazi?
 
Kwa hiyo kwa sababu ya utalii na maslahi ya uwekezaji ndio madhara yanayowapata watanzania yasifanyiwe kazi?
Si ndi haya mambo ya kutaka kuunda kamati ya kuua nyoka aliyekwenye eneo lako? Kwani kuandikwa kwenye magazeti tumeanza leo Kagasheki? hata kama hoteli zisingefungwa tutaendelea tu kuandikwa, cha msingi ni kama mambo tunayoandikwa yana tija.

Nimeshawahi personally kugombana na wafanyakazi wa double tree hotel kuhusu suala la maji machafu.

Naomba ufafanuzi wa hili, hivi lile bomba kubwa linaloingiza maji machafu baharini maeneo ya ocean road karibu na ikulu limekaaje kimazingira?
 
Utalii unaoharibu mazingira yetu hatuuhitaji hata kidogo.kama kagasheki anautaka atafute pa kuupeleka
 
Kagasheki anapaswa kutambua seniority! Waziri wa mazingira yuko ofisi ya Makamu wa Rais na hivyo maamuzi yake ni final kwa mujibu wa sheria na hana sababu ya kufanya mawasiliano naye. Aidha sheria ya mazigira ndiyo inayotumika kama sheria mama endapo kuna mgongano wa sheria zilizopo katika kusimamia maswala ya mazingira kama maji, misitu, makazi nk.
 
Sakata zima la hoteli za Double Tree na zingine linaonyesha upeo mdogo walionao viongozi wa serikali hii isiyokubali kuitwa 'dhaifu'. Katika mambo mengi sana kumetokea kutoeleweka nani anapaswa kufanya nini na/au kusema nini na wakati gani, si kwa hili tu. Hata hao NEMC wamevunja nyumba za watu kadhaa wenyewe waliwaita 'vigogo' zilizojengwa kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi kinyume cha sheria, lakini mpaka leo hii lile hekalu la Mch Gertrude Lwakatare halijaguswa (?!) Hii ni dhahiri ya kuwa hao walioko madarakani katika jumla yao hawajui wanaruhusiwa kufanya nini na hawaruhusiwi kufanya nini kisheria. Ni dhahiri ya kuwa kuna sheria mbili Tanzania, kwa watu wa kawaida, na kwa 'waheshimiwa'.

Matokeo yake ni watendaji wa chini kutojua kipi cha kufanya maana hakuna mwelekezaji, au waelekezaji wana viwango tofauti kulingana na mtu anayeguswa (double standards).

Nafikiri sasa ni wakati mzuri kwa watakaoweza kushiriki kwenye kutunga katiba mpya kuliweka hili bayana.

Mawaziri na watendaji wote wakuu serikalini lazima wawe na 'job description' na iwekwe wazi hadharani ili kila mtanzania ajue waziri fulani mipaka yake iko wapi. Huenda hili litawafanya watu kama kina Kagasheki kuacha kutuchafua watanzania na vinyesi vya wazungu na kukubali maamuzi ya kina Huvizya kuwa yanakubalika kisheria.

Wanaoumia ni wewe na mimi... ni muda muafaka wa kuamua tunataka watu kama hawa waendelee kuwa madarakani ama hapana!

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kagasheki hakupaswa kwenda public kumpinga mwenzake. Haya yangefanyika kiofisi bila sisi kuona wanapingana. Kiutendaji inakuwa ngumu sana kama kiongozi mwenzako anakupinga hadharani.

Kwani mkuu hujui hii serikali imechanganyikiwa?
 
Kagasheki ameathiriwa na ugomvi wake na Meya wake kuhusu soko jimboni kwake analega na huku hasira zake. Katatue mambo katika baraza la mawaziri na si kupingana na mwenzako hadharani.

Kagasheki akumbuke kilichofanya baraza lililopita kuvunjwa, ilikuwa ni pampoja na mawaziri kupingana hadharani, haya ndo mambo ya mwamba ngoma!
 
Back
Top Bottom