Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,652
- 729,711
Tunatambua kuwa milango ya fahamu iko mitano
Macho kuona
Masikio kusikia
Mdomo kuonja
Pua kunusa na
Ngozi kuhisi
Safi sana hii ndio milango yetu mitano ya fahamu tuliyofundishwa mashuleni na katika vitabu vya dini
Lakini una habari kuna milango mingine mitatu isiyosemwa sana ?
Milango ile mitano ya kwanza ni ile inayoonekana kwa macho...lakini baada ya hapo kuna hii mingine mitatu ambayo ni ya kiroho na kiufahamu huwezi kuishika kuinusa wala kuiona kwa macho...hebu tupitie mmoja baada ya mwingine
Mlango wa sita(sixth sense)hiki ni kituo kikuu cha kuchambua matukio yote muhimu yaliyokusanywa kushunghulikiwa na kunyambulishwa na ile milango mitano ,....matukio haya hufanya akili/ufahamu na roho kuwa angavu na makini sana...kwa kiswahili cha kawaida tunaita machale...kutokana na uchambuzi mzuri wa yale matukio yaliyokusanywa na ile milango mitano mlango wa sita huweza kupata mwangaza wa kubashiri nini kinaweza kutokea (wengi wetu akili zimezongwa na mambo ya kidunia kiasi cha kufanya mlango huu usifanye kazi vizuri)
Mlango wa saba...huu unajulikana kama chujio, wafanya tahajudi wengi hunia kufikia hatua hii hii ni hatua ngumu na ya juu mno
Ukiweza kufika hatua hii basi haya yafuatayo ni rahisi kuyafanya kwakuwa akili iko safi na ina mwanga wa kutosha kwakuwa ni matukio muhimu tu ndio huhifadhiwa hapa yakichujwa kwa makini sana
Nitaandika kwa kiingereza. Teleportation telekinesis telepathy cosmo intuition nk nk
Mlango wa nane; hapa ndio mwisho huku ndio hupokea matukio yote yaliyochujwa yakachujika na kuja kukaa hapa milele...huu ni mlango wenye ambao kuna binadamu wachache sana wameufikia huu hauna tofauti na nguvu za majini mizimu mashetani nk nk
Ni hatua ambayo yeyote anayeifikia huweza kufanya miujiza mingi kwakuwa akili na ufahamu wake vimekuwa vyepesi mno..ana uwezo wa kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja kusafiri kwa kutumia mwanga kusoma akili za watu na kucheza nazo kuingia na kutoka popote bila kutumia mlango wala dirisha kuweza kuutangulia muda na kusoma yajayo kwa usahihi nk nk
Hiyo ndio milango mitatu ya mwisho ambayo wengi wetu hatujahi kufundishwa popote
Kwahiyo Tukirudi nyuma kiasili mlango muhimu sana na wa kawaida ukiachana na ile mitano ya kwanza ni huu wa sita huu wa machale huu uwezao kuhisi hatari au utabiri wa jambo japo si kwa usahihi wala kwa uhakika sana
Ni mlango huu wa sita bila wengine kujua ndio ambao hutuchagulia wenza marafiki na hata maadui na mlango huu wa sita ambao hutukumbusha matukio tusiyokumbuka na hata watu pia...unashangaa unamuona mtu lakini ni kama vile hiyo sio mara ya kwanza kumuona haya ni mawasiliano ya kiroho kupitia huo mlango au unakutana na mtu na kumchukia hapo hapo bila sababu si wewe ni nguvu ya mawasiliano ya kiroho
Unapoenda kwa mganga au nabii na mtume akafanya miujiza, wengine si roho ya Kimungu ama kichawi na nguvu ya mlango wa sita na saa nyingine wa saba..ni kitu ambacho kinawezekana hata kwako....waweza jaribu kupitia tahajudi