Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,648
- 75,737
Mawasiliano/communications.
Hili ni jambo tunalolipuuzia saana tunapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi. Aidha ndoa nyingi au mahusiano mengi yamevunjika tu kwa aidha mwanandoa mmoja au wote kupuuzia mawasiliano au kumshirikisha mwenzi wake japo dogo alilonalo moyoni, ambalo lingeweza kumalizwa na mazungumzo.
Unapokuwa na tatizo na mwenza wako ukalificha.. kutomshirikisha kutaleta athari kubwa na hautajua imesababishwa na kutokuwepo kwa mawasiliano kwasababu unayapuuza.
Kwenye mahusiano kuna matatizo ya kuhisi kusalitiwa, matumizi ya pesa, kutokuridhika katika mapenzi, kudharauliwa, kutokushirikishwa katika maamuzi n.k. haya yote njia rahisi ya kuyamaliza ni [mawasiliano] kukaa chini na kuyazungumza na mwenzi wako na sio kuyaweka moyoni siku ukiudhika uyaseme kama malalamiko.
Mawasiliano yanapokuwepo baina ya wapenzi.... yaanasaidia kuaminiana, kuheshimiana, kusikilizana na kuvumiliana. Wewe dada mmeo/mwenza wako alipokukera ulimwambia kwa utaratibu baadae kuwa hubby ulinikera naomba tuyamalize? Au umeliweka moyoni siku akikukanyaga umkumbushie kwa kulia?
Wewe mwanamme mpenzi wako alipohisi unamcheat ulimkalisha chini mkayamaliza kila mmoja akabaki na amani pasipo na hisi hasi?
Tupende kuwasiliana katika mapenzi.... tutaboresha mahusiano yetu kwa ujenzi wa familia bora.
asalaaam.