Mawakili wavutana kesi ya mwale | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawakili wavutana kesi ya mwale

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by PISTO LERO, May 4, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  MVUTANO mkali wa hoja za kisheria ulizuka juzi mjini hapa kati yamawakili wakuu wa serikali, Fredrick Manyanda na Neema Ringo, na wakili maarufuMediu Mwale.
  Mabishano hayo yalizuka baada ya mawakili hao wa serikali kudai kuwamahakama hiyo ina uwezo kisheria wa kupitia mwenendo na maamuzi yaliyofanyikana mahakama ya mkoa ili iweze kunyoosha pale palipokwenda isivyo na kufanyiamasahihisho huku akirejea maamuzi yaliyofanywa na mahakama ya rufaa nchini.
  Aidha walisema madai kuwa kutumia kipengele cha sheria ambacho hakikonchini kufungua maombi yao mahakamani hapo, ilitokana na makosa ya uchapishajina hawakuweka maneno ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA) huku wakisisitizakuwa sheria hiyo ipo na mahakama ina uwezo wa kufanya marekebisho.
  Wakijibu hoja ya tatu ya pingamizi ya wao kushindwa kuambatanisha nakalaya maamuzi wanayoomba yafanyiwe marejeo, walisema kuwa hakuna mahali sheriainalazimisha kuwekwa kwa nakala hiyo kwa hatua ambayo shauri hilo imefika ilainafanywa hivyo kwa mashauri yanayopelekwa mahakama ya rufaa.
  Wakili wa serikali Manyanda aliieleza mahakama kuwa katika pingamizi lanne lililodai kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hana nguvu kisheriakuiwakilisha Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwani DPP wala TRA hawajashtakimahakamani hapo.
  Aidha alisema kuwa hoja ya hati ya kiapo ya mtumishi wa TRAiliyoambatanishwa kwenye hati ya kufungua maombi hayo kuwa na mapungufukisheria, Manyanda alisema kuwa haina msingi kwani ingepaswa kutaja jina lamahakama endapo ingekuwa inaunga mkono maombi hayo lakini hati hiyo ilipelekwamahakamani hapo kwa ajili ya kuleta taarifa tu.
  Hata hivyo, Wakili Mwale alidai kusikitishwa na majibu ya mawakili waserikali kwani hayana lengo la kuisaidia mahakama kutenda haki.
  Mwale alisema mawakili hao walikosea kufanya rejea kwenye mashauri yamahakama ya rufaa ambayo yameshafanyiwa maamuzi na yanakuwa na amrizisizopungua tatu za mahakama kuu ambayo kwa hatua shauri hili lilipofikiahalihusiki kwani hayo yaliyofanyika ni maamuzi madogo ambayo hayamalizi kesi yamsingi.
  Alidai tatizo la mawakili hao wa serikali hawapendi kusoma kwani hatakwenye hoja zake za pingamizi aliwaambatanishia vifungu vya sheria vinavyoelezajuu ya shauri linalofunguliwa bila kuonyesha kifungu sahihi cha sheria lakinihawakusoma hivyo akaendelea kuisisitiza mahakama kutupa maombi hayo ya kufanyiamarejeo.
  Alisema kuwa haiwezekani kuieleza mahakama kuwa TRA si mdai wakati hatiya kiapo iliyoambatanishwa kwa ajili ya kufungua maombi hayo ya marejeo ni yawakili wa serikali Manyanda na ya mtumishi wa TRA, Andrew Mushi, hivyo sisahihi kusema kuwa TRA haihusiki kufungua maombi hayo.
  “Mheshimiwa jaji hati hiyo si kielelezo bali ni hati ya kiapowaliyotumia kuleta maombi haya mbele yako na hii ndiyo anaitumia mara nyingikuninyima haki,” alisema wakili Mwale.
  Baada ya mabishano hayo ya kisheria, mahakama kuu hiyo imepanga kutoauamuzi Mei 11, juu ya pingamizi zilizowasilishwa mahakamani hapo na wakiliMediun Mwale anayepinga hatua ya serikali ya kutaka mahakama hiyo kupitiauamuzi uliofanywa na mahakama ya mkoa.
  Jaji Kakusulo Sambe alisema atatoa uamuzi huo kuanzia saa 3 asubuhi ilikuwezesha faili la shauri hilo kurudi mahakama ya hakimu mkazi inaposikilizwashauri la msingi.
  Wakili Mwale aliwasilishamahakamani hapo pingamizi tano akiomba mahakama hiyo kutupa maombi ya marejeoya maamuzi madogo ya mahakama ya hakimu mkazi ambayo baada ya kupitia ushahidiwa pande zote iliamuru arejeshewe magari yake saba na simu akidai vilichukuliwana kushikiliwa kinyume cha sheria ya matunda ya uhalifu (Proceeds Crimes Act)pamoja na vifungu namba 41 na 44 vya sheria ya mwenendo wa kesi za jinai hivyokuagiza arejeshewe.
   
 2. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  jamani huyu mwale si yule wakili anayeteteaga majambazi tuu wanaovamiaga mabenki....,,..pamoja na watuhumiwa wa
  mihadarati...?
   
 3. M

  MAKAWANI Senior Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kutetea majambazi siyo hoja. Kutetewa ni haki ya msingi ya kila mtu, soma katiba Ibara ya 13 yote.
   
Loading...