PreGE2025 Mawakili wa Tundu Lissu wawasilisha malalamiko umoja wa mataifa, kushinikiza hatua za kimataifa

PreGE2025 Mawakili wa Tundu Lissu wawasilisha malalamiko umoja wa mataifa, kushinikiza hatua za kimataifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mawakili wa mwanasiasa kigogo wa upinzani nchini Tanzania ambaye yuko gerezani TUNDU LISSU wamewasilisha malalamiko mbele ya Jopo la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia vitendo vya Ukamataji Watu Kiholela.

Wakili wa Lissu, Robert Amsterdam amesema malalamiko hayo ni sehemu ya kampeni pana ya kuongeza shinikizo la kimataifa kwa watawala nchini Tanzania kumwachia huru kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.

Kwa kawaida jopo hilo hutoa maoni yake ya kisheria juu ya mamlalamiko inayopokea lakini halina nguvu ya kuyatekeleza. Hata hivyo Amsterdam amesema kampeni ya kutaka Lissu aachiwe inahusisha pia mwito kwa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani kuwawekea vikwazo wote wanaohusika na kesi ya Lissu ikiwemo waendesha mashtaka, majaji na polisi.

Lissu alikamatwa mwezi uliopita na kufunguliwa kesi ya uhaini kutokana na matamshi anayodaiwa kuyatoa ya kuwataka wafuasi wake kuzuia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini Tanzania mwezi Oktoba.
=======

Amsterdam & Partners LLP Files United Nations Petition on Behalf of Tanzanian Opposition Leader Tundu Lissu


Washington, D.C., May 30, 2025 – Amsterdam & Partners LLP, international counsel to Tanzanian opposition leader Tindu Lissu, has submitted a formal submission to the United Nations Working Group on Arbitrary Detention (UNWGAD), calling for an urgent investigation into his ongoing detention by Tanzanian authorities.

Mr. Lissu, a prominent lawyer, longtime advocate for democratic reform and Chairman of CHADEMA, the country’s largest opposition party, was arrested on 9 April 2025 following a peaceful rally held in the town of Mbinga in southwestern Tanzania, as part of the "No Reforms, No Election" campaign. He has since been charged with treason — a charge which under Tanzanian law carries the death penalty.

"This is not just an attack on one man, but on the democratic aspirations of an entire nation," said Robert Amsterdam, Founder and Managing Partner of Amsterdam & Partners LLP. "We have made this submission to the UN Working Group on Arbitrary Detention because there is little chance for a fair or independent legal outcome for my client in Tanzania. My client's detention violates Tanzania’s obligations under international human rights law, and we are calling for the world to act", he added.

The petition details a range of serious procedural violations and human rights abuses. It highlights the arbitrary nature of Mr. Lissu's arrest, prompt formal charges and the restrictions placed on his access to legal counsel and family members. It also raises grave concerns over the misuse of sedition and treason laws to target peaceful political speech, and underscores the Tanzanian government’s failure to uphold the minimum standards of due process required under its international treaty obligations.

In addition to requesting that the Working Group declare Mr. Lissu's detention arbitrary and in violation of international law, the petition urges the UN body to call for his immediate release and recommend remedies, including compensation and guarantees of non-repetition.

Mr. Lissu's arrest and continued detention have drawn widespread condemnation from international human rights organisations, civil society groups and foreign governments, with which Amsterdam & Partners LLP will continue to engage. The United States, European Union and multiple regional leaders have issued statements of concern.

"Tundu Lissu stood up for electoral reform, transparency and the rule of law. For that, he is being punished," said Amsterdam. "We will not stop until justice is done."

Amsterdam & Partners LLP is an international law firm based in Washington, D.C. and London, with a focus on political cases.
 
Mawakili wa Kiongozi wa Upinzani nchini Tanzania aliyepo mahabusu, Tundu Lissu jana Ijumaa waliwasilisha malalamiko yao kwa Jopo Kazi la Umoja wa Mataifa wakipinga kuendelea kushikiliwa kwake katika jitihada za kuongeza shinikizo la kimataifa la kutaka aachiwe huru, linaripoti shirika la habari la Uingereza Reuters.

Lissu, ambaye ni mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, na mshindi wa pili katika uchaguzi wa rais wa 2020, alikamatwa mwezi uliopita na kushtakiwa kwa uhaini, shitaka ambalo akikutwa na hatia hukumu yake ni kifo, kutokana na kudaiwa kutoa wito kwa wafuasi wake kuzuia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Msemaji wa serikali ya Tanzania hakujibu mara moja ombi la Reuters kutaka maoni yake.

Wakati Rais Samia Suluhu Hassan amepata sifa kwa kupunguza ukandamizaji wa kisiasa hususani kwa vyama vya upinzania na viongozi wao, amekabiliwa na maswali kuhusu utekaji nyara wa wakosoaji wa serikali katika miezi ya hivi karibuni. Utekaji nyara huo haujatolewa maelezo thabiti na viongozi wa serikali.

Rais Samia, ambaye atagombea kiti cha urais katika uchaguzi wa Oktoba, amesema serikali yake inaheshimu haki za binadamu na kuagiza uchunguzi ufanyike kuhusu utekaji nyara unaoripotiwa.

Wakili wa kimataifa wa Lissu, Robert Amsterdam, alisema malalamiko ya siri kwa jopo kazi la Umoja wa Mataifa, ambalo linatoa maoni lakini halina nguvu ya utekelezaji, ni sehemu ya kampeni ya shinikizo kubwa.

Mwezi huu Bunge la Ulaya lilipitisha azimio la kupinga kukamatwa kwa Lissu na kwamba kulichochewa kisiasa, na Amsterdam alisema kwamba ataiomba Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuweka vikwazo.

"Hata kwa waendesha mashtaka, majaji, polisi - watu wote ambao wanahusika katika kesi hii ya uwongo wangefahamu kwamba wanapaswa kulinda maslahi yao nchini Amerika," Amsterdam aliiambia Reuters.

Katika kujibu azimio la Bunge la Ulaya, wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ilisema ukosoaji wa nje kuhusu kesi hiyo ulitokana na "taarifa zisizo kamili au za kuegemea upande fulani".

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni yake.

Lissu, ambaye alipigwa risasi 16 katika shambulio la mwaka Septemba 2017 katika eneo la makazi ya viongozi mjini Dodoma, na ambalo hakuna mtuhumiwa aliyewahi kufunguliwa mashtaka, atafikishwa mahakamani tena Jumatatu Juni 2.

Kabla ya kufikishwa mahakamani wiki iliyopita, mamlaka zilimshikilia mwanaharakati rai awa Kenya na mwanaharakati wa haki za Uganda ambao walikuwa wameingia Tanzania kuhudhuria kusikilizwa kwa shauri dhidi ya Lissu.

Walitelekezwa siku kadhaa baadaye jirani na na mipaka ya nchi zao. Mwanaharakati wa Kenya, Boniface Mwangi, alisema wote wawili waliteswa vibaya wakiwa mahabusu.

Maafisa wa Tanzania hawajajibu maombi ya maoni yao kuhusu madai hayo.

Rais Samia amewaonya watu wa nje dhidi ya "kuvamia na kuingilia mambo yetu"

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa toleo jipya la Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 (Toleo la 2024), Rais Samia alisema kuna mwenendo unaoibuka wa baadhi ya wanaharakati kuvuka mipaka na kuingilia masuala ya ndani ya nchi, hali ambayo haiwezi kuvumiliwa.

"Tusiwe shamba la bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka… Tumeanza kuona mtitiriko au mwenendo wa wanaharakati ndani ya region (kanda) yetu hii, kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku," alisema Rais Samia.

Kauli hiyo ilikuja siku moja baada ya wakili mashuhuri wa Kenya na aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria, Martha Karua, pamoja na Jaji Mkuu wa zamani Willy Mutunga na wanaharakati wengine wawili, kuzuiwa kuingia nchini Tanzania.

Walikuwa wamewasili kushuhudia kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tanzania, Tundu Lissu, ambayo imeendelea leo katika Mahakama ya Kisutu.

Kwa mujibu wa Karua, alifurushwa na kurudishwa Kenya kwa lengo la kumzuia kuhudhuria kesi hiyo. Mutunga na wenzake pia walielezwa kuwa walizuiwa katika uwanja wa ndege kabla ya kurejeshwa nchini kwao.

Kauli ya Rais Samia ilionekana kutoa mwelekeo wa msimamo wa serikali ya Tanzania kuhusu suala hilo.

"Sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia huku. Tusitoe nafasi, walishaharibu kwao, walishavuruga kwao, nchi iliyobaki haijaharibika watu wako na usalama na amani na utulivu ni hapa kwetu, aliongeza Rais Samia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Korir Sing'oei, alisisitiza umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu na ushirikiano wa kikanda.

Hata hivyo, tofauti na ilivyotarajiwa, baada ya kauli hizo hali ya mambo haikupoa badala yake kulitokea kauli zenye lugha kali za baadhi ya wabunge wa Tanzania wakati wakchangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi huku baadhi ya wabunge wa Kenya wakijibu kwa ukali

Nako katika mitandao ya kijamii kulikuwa na mjadala na malumbano makali kwa pande zote mbuli hadi Rais wa Kenya, William Ruto alipoziomba radhi Tanzania na Uganda.
 
hivi si kuna hata maandamano flani hivi ya waropokaji chadema yaliishiaga Umoja wa Mataifa?
Ilisaidiaga nini ile mambo gentleman?🐒
 
Wameyataka, watayapata, alisikika Lissu
1747669820981.jpg
 
Mawakili wa Mwenyekiti wa Chadema aliye gerezani, Tundu Lissu, wamewasilisha malalamiko Ijumaa kwa Kikundi Kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia kunyimwa uhuru kiholela, katika juhudi za kuongeza shinikizo la kimataifa ili aachiliwe.

Lissu, aliyet9mbea urais na kushika nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020, alikamatwa mwezi uliopita na kushtakiwa kwa kosa la uhaini lenye adhabu ya kifo, kutokana na kauli anazodaiwa kuzitoa akiwataka wafuasi wake kuzuia uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba usifanyike.
Pia anatuhumiwa kwa makosa ya kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni.

Msemaji wa Serikali ya Tanzania hakujibu mara moja alipotafutwa na Reuters kuhusu haua hiyo.
Japo Rais Samia Suluhu Hassan amesifiwa kwa kulegeza ukandamizaji wa kisiasa, amekumbwa na maswali kuhusu utekaji nyara wa watu wanaoikosoa serikali katika miezi ya hivi karibuni. Hassan, ambaye anatarajiwa kugombea tena urais mwezi Oktoba, amesema serikali yake inaheshimu haki za binadamu na ameagiza uchunguzi kufanyika kuhusu matukio hayo ya utekaji.

Mwanasheria wa kimataifa wa Lissu, Robert Amsterdam, amesema malalamiko ya siri yaliyowasilishwa kwa kikundi kazi cha Umoja wa Mataifa – ambacho hutoa maoni lakini hakina mamlaka ya utekelezaji – ni sehemu ya kampeni pana ya kushinikiza.

Bunge la Ulaya mwezi huu lilipitisha azimio la kulaani kukamatwa kwa Lissu, likiitaja kama kisiasa, na Amsterdam alisema ataiomba Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuweka vikwazo.

“Kuanzia kwa waendesha mashtaka, majaji, polisi – watu wote waliohusika katika kesi hii ya uongo wanapaswa kufahamu kuwa wanapaswa kulinda mali zao walizonazo Marekani,” Amsterdam ameliambia shirika la habari la Reuters.

Kufuatia azimio la Bunge la Ulaya, wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ilisema ukosoaji wa nje kuhusu kesi hiyo umetokana na “taarifa zisizo kamili au za upendeleo.”

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani haikutoa majibu mara moja kuhusu ombi la kutoa maoni.

Lissu, ambaye alipigwa risasi mara 16 katika shambulio la mwaka 2017 ambalo hadi sasa hakuna mtu aliyeshtakiwa, anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu.

Kabla ya kufikishwa mahakamani wiki iliyopita, mamlaka za Tanzania ziliwakamata wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Kenya na Uganda waliokuwa wamefika kuhudhuria kesi hiyo.

Siku chache baadaye walitelekezwa karibu na mipaka ya nchi zao, na mwanaharakati wa Kenya, Boniface Mwangi, alisema wote waliteswa vibaya wakiwa kizuizini.

Maafisa wa Tanzania hawajajibu maswali kuhusu madai hayo. Hassan ameonya watu wa nje dhidi ya “kuingilia na kuathiri masuala yetu ya ndani.”
 

Attachments

  • Screenshot_20250601_081559_Google.jpg
    Screenshot_20250601_081559_Google.jpg
    722.2 KB · Views: 22
Back
Top Bottom