Mawakala wa UKAWA vs Ulinzi wa kura za Rais

Mawakala wa UKAWA vs Ulinzi wa kura za Rais

tanken

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2014
Posts
224
Reaction score
53
Nahisi ni vema tuwekane sawa kuhusu hawa mawakala wa UKAWA. Hapa ndiko kete letu wanamabadiliko.

Nashauri hawa waapishwe na wakili wa UKAWA kusaini mkataba, wapewe simu maalum iliona uwezo wakurekodi 24 hours, watakiwe warekodi tukio lote wakati wa kuhesabu KURA, kamera aina ya spy kamera. Watume picha baada ya dakika 10. Watume data ya kituo hasa picha ya matokeo kuyatuma ilio bandikwa kwa Tallying center ya UKAWA. Ikiwezekana hawa mawakala watumwe na makao makuu, ofisi za UKAWA, wawe ni watu wasionunulika kamwe.
 
Mawakala wapelekwe mafunzo maalum MAHALI pasipojulikana,wawekwe sawa,wafundishwe uzalendo,kuhusu malengo ya MABADILIKO. Wakae SIKU mzima.
 
wakala atangia kwenye chumba cha kuhesabia kura kama wairaq walivo ingia kumsikiliza Bush enzi hizo alipotembelea baghdad.

labada watakuwa na fursa ya kurusha viatu vyao tu, si kingine.
 
Nahisi ni Vema tuwekane sawa kuhusu hawa mawakala wa UKAWA. Hapa ndiko kete letu wanamabadiliko. Nashauri hawa waapishwe na wakili wa UKAWA kusaini mkataba,wapewe simu maalum iliona uwezo wakurekodi 24 hours,watakiwe warekodi tukio lote wakati wa kuhesabu KURA,kamera aina ya spy kamera.watume picha baada ya dk 10.watume data ya kituo hasa picha ya matokeo kuyatuma ilio bandikwa kwa Tallying center ya UKAWA. Ikiwezekana hawa mawakala watumwe na makao makuu,ofisi za UKAWA, wawe ni watu wasionunulika kamwe.
Hofu ya kuibiwa inawamaliza, mnaanza kuwa watunzi wa movie za James Bond. Kweli mafuriko ya lowassa yamebeba akili za watu.
 
Umetoa binge la wazo, yaani inabidi mawakala hao wawe kwanza wamejitoa kiroho safi kabisa
 
ni kipindi mawakala kuwa matajiri kama diamond mkata viuno analipwa milioni 100 je wakala ambae ndio mwamuzi mkuu unafikiri atapewa ngapi? kweli kazi tunayo tumwombe Mungu
 
Kuna taarifa kwamba ccm wameanda hela feki zakuwahonga mawakala Wa ukawa ili kurahisisha goli la mkono wakishawapa hizo hela wasimamizi Wa ccm wataita polisi watawaambia wawasachi mawakala Wa ukawa wakikutwa na hizo hela feki watachukuliwa na polisi hivyo bao la mkono litakuwa halali ya ccm, mawakala waliangalie sn jambo hili pia raia wote wakumbuke kuja na kalamu zao
 
Mkuu,
Tatizo ninaloliona hapa ni huo mnao usema ati ni uzalendo. Yaani umfanye mtu kuwa mzalendo kwa siku moja tuu?? Hili lilitakiwa liwe ndio kipaumbele chetu tangu mwanzo. Tungalikaa nao kwenye makambi mbalimbali na kuwachunguza na kuwachuja. Majimbo 266 sio mengi kama tungedhamiria.
Hofu yangu, mihela inayomwagwa na ccm. Usipime!!! Yaani wanafanya kufuru. Sasa huu uzalendo upo tena Tz hii kweli?? Mtu atoke home hana mlo wa siku hiyo. Pengine kawaacha watoto hawana mlo. Amekuja tangu asubuhi mpaka asubuhi nyingine. Ushauri wangu, Wapeni posho nzuri wala si sh 20.000/=, mpo?? Walipeni vizuri, waapisheni watalinda. Kinyume cha hapo, tumeumia kwani goli la mkono hiloooo. Ile tofauti ya milion 6 alio isema m/kiti wao ni hapo inakuja kujumlishiwa tu.
Ni mawazo yangu tu, ila sijauona uzalendo huu hapa kwetu mbele ya mshiko unaomwagwa na ccm. Nakuambia ni kufuruuuu
 
Badala ya kutushawishi tuwapigie kura mnawaza kulinda nanikawaambia tutawapa hizo kura mnazo taka kulinda kura zetu kwa magufuli nyie jihangaisheni tu
 
Hofu ya kuibiwa inawamaliza, mnaanza kuwa watunzi wa movie za James Bond. Kweli mafuriko ya lowassa yamebeba akili za watu.

Hapo unapazungumziaje wewe gamba!?
 

Attachments

  • 1445023661709.jpg
    1445023661709.jpg
    54.3 KB · Views: 560
Japokua Imani zinaingiliana...mimi nashauri mawakala wote wakasomewe kurani takatifu,na mda wakala anaapa,amalizie kwa kusema nikiujumu ukawa NIFE KIFO KIBAYA.
 
Marufuku kuingia na simu katika chumba cha kuhesabia kura! by NEC
 
ni kipindi mawakala kuwa matajiri kama diamond mkata viuno analipwa milioni 100 je wakala ambae ndio mwamuzi mkuu unafikiri atapewa ngapi? kweli kazi tunayo tumwombe Mungu

Kweli ndugu YANGU.ni Mungu. Hawa mawakala hasa wa UKAWA wanapaswa wawe ni watu wa pekee
 
Mkuu,
Tatizo ninaloliona hapa ni huo mnao usema ati ni uzalendo. Yaani umfanye mtu kuwa mzalendo kwa siku moja tuu?? Hili lilitakiwa liwe ndio kipaumbele chetu tangu mwanzo. Tungalikaa nao kwenye makambi mbalimbali na kuwachunguza na kuwachuja. Majimbo 266 sio mengi kama tungedhamiria.
Hofu yangu, mihela inayomwagwa na ccm. Usipime!!! Yaani wanafanya kufuru. Sasa huu uzalendo upo tena Tz hii kweli?? Mtu atoke home hana mlo wa siku hiyo. Pengine kawaacha watoto hawana mlo. Amekuja tangu asubuhi mpaka asubuhi nyingine. Ushauri wangu, Wapeni posho nzuri wala si sh 20.000/=, mpo?? Walipeni vizuri, waapisheni watalinda. Kinyume cha hapo, tumeumia kwani goli la mkono hiloooo. Ile tofauti ya milion 6 alio isema m/kiti wao ni hapo inakuja kujumlishiwa tu.
Ni mawazo yangu tu, ila sijauona uzalendo huu hapa kwetu mbele ya mshiko unaomwagwa na ccm. Nakuambia ni kufuruuuu

Huu ni Ukweli. Kuanzia sasa UKAWA naamini wameeanda tayari mawakala, kama bado,waandaliwe sasa,watengewe bajet yao haijalishi ni chama kipi,KILA chama nda ya UKAWA waje na mkakati maalum hasa kuwa identify hawa wakala. Nakuunga mkono
 
Back
Top Bottom