Mavuno ya mahindi mwaka huu wa 2018 siyo mazuri

T-money

Member
Nov 1, 2010
22
10
Tujiandae kupanda kwa bei ya mahindi..mavuno mwaka huu yamesuasua. Zambia production zimeshuka by 34 %. Tanzania bado sijaona taarifa zao. Mahindi sasa yapo mikononi kwa wafanya biashara...nimejaribu kutafuta kwa wakulima sipati...
 
Mbona juzi tuu walikua wanalalamika bei ya mahindi shambani imeshuka sana na imekua hasara kwa wakulima
 
nna mpango wa kuchukua gunia mbili za mahindi mbili za mpunga muda c mrefu kabla mambo ya kufichaficha hayajaanza
 
Mbona juzi tuu walikua wanalalamika bei ya mahindi shambani imeshuka sana na imekua hasara kwa wakulima
Mimi nimetahadharisha tu mkuu kutokana na dalili zilizoko huku Sumbawanga. Huko kwingine sijui.
 
KuadimikA kwa mahindi ni kweli ilA suala la kupanda bei kwa mwaka huu sidhani.......
 
Kwamba yapo maeneo mahindi hayakumea vizuri ni kweli ila habari ya kutafuta mahindi halafu hayapatikani ni uongo.

Nazungumza kama mdau wa nafaka ambae ninaozoefu na karibia maeneo mengi ya nchi hii sio habari yakusikiasikia.

Unasema mahindi hayapatikani wakati masoko ya mahindi kama tandale 1kg=370,Dodoma 315 kwa kg,kiteto gunia la plastiki sits ni 30,000,tunduma/sumbawanga/mbeya haizidi 28000.Tanga kwa mkulima gunia la plastiki sita 24,000 kwa madalali 30,000.

Hitimisho,
Ni kweli Mahindi yataadimika lakini si Leo.
 
Tujiandae kupanda kwa bei ya mahindi..mavuno mwaka huu yamesuasua. Zambia production zimeshuka by 34 %. Tanzania bado sijaona taarifa zao. Mahindi sasa yapo mikononi kwa wafanya biashara...nimejaribu kutafuta kwa wakulima sipati...
Kama unahitaji mahindi tutafutane mkuu,yapo pwani nauza 40,000 kwa gunia kwasasa...
 
Nimeanza kupokea simu nyingi kuulizia mahindi. Wakati wa mahindi kupanda umewadia. Congo, Zimbabwe, Zambia, Malawi wameanza kuja katafuta mahindi hapa Sumbawanga...
 
UWEZEKANO NI MKUBWA NDUGU NA ZINAWEZA KUPANDA ZAIDI MWAKANI KUTOKANA NA WAKULIMA KUKATISHWA TAMAA NA BEI ZA MWAKA HUU.

NAUZA MAHINDI SAFI YA NJANO, NINA TANI 29. NIPO MKOA WA RUVUMA 0758- 25 36 02 AU 0625- 22 80 30.
 
Nimeanza kupokea simu nyingi kuulizia mahindi. Wakati wa mahindi kupanda umewadia. Congo, Zimbabwe, Zambia, Malawi wameanza kuja katafuta mahindi hapa Sumbawanga...
Vip bei ya mpunga kwa gunia imefikia ngapi kwa sas?
 
Mahindi kwa sasa yapo ya kutosha kwa wafanyabiashara na wakulima, kwa lugha rahisi ni kuwa hatuna uhaba wa mahindi kwa sasa ila mbeleni itategemea na maamuzi ya wakulima ( kama wataamua kuendelea kulima kwa wingi ama watapunguza uzalishaji) hivyo tuzidi kuvuta subira huku tukiwa na taadhari zote..
 
Bora yapande bei, tena yapande Kweli Kweli ili Mkulima aweze kunufaika na jasho lake Mwenyewe.
Mkulima anufaike vipi na wewe, mkulima kauza bei ya hasara kwa mlanguzi (mlanguzi kayahifadhi) huyo ndo atakayenufaika.

Chain ya biashara iliharibiwa baada ya serikali kuzuia kuuzwa mahindi nje, hapo ndo mahindi mengi yakawa ndani ya nchi kupelekea kushuka bei kutoka mashambani kwenda kwa mnunuaji (mchuuzi).

Sasa kinachofanyika hapa wafanyabiashara wameweka stock , uhaba ukitokea wanayatoa kuuza kwa walaji kwa bei kubwa huku mkulima akiwa keshakula hasara kitambo tu (nieleweke wengine wanakopa benk kugharamia shughuli za kilimo).

Mwisho wa siku serikali isifanye vitu bila kufikiria maana mkulima akipa hasara mwakani akashindwa kulima tegemea uhaba mkubwa wa mahindi baadae ambao watumiaji pia wataumia, wakulima hali mbaya na wafanyabiashara hawatafanya trade..

Uchumi! Uchumi ! Uchumi ! Wa viwanda (kati).
 
Back
Top Bottom