Mavunde: Tusiichezee amani, ni jambo la kudumu

Mavunde: Tusiichezee amani, ni jambo la kudumu

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Peter Mavunde ametoa wito kwa watanzania wote kuitunza amani iliyopo, na kutotumia sababu za muda mfupi kuvuruga amani ambayo ni jambo la kudumu.

"Tukumbuka maneno ya Baba wa Taifa aliyowahi kusema, tusitumie sababu za muda mfupi kwa jambo la kudumu, amani ni jambo la kudumu halina mbadala. Kwa hiyo mtu yeyote asiichezee amani ya nchi," amesema Mavunde.

Soma pia: Haji Manara: Hii nchi ina utawala Octoba 29 hatoki mtu kuandamana

Akizungumza leo Oktoba 07, 2025 katika Kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1, Mavunde ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu na kutoingia kwenye mitego ya baadhi ya watu wenye nia ovu ya kutaka kuivuruga amani iliyopo nchini.
 
Back
Top Bottom