Mavazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mavazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Haika, Aug 19, 2010.

 1. H

  Haika JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Siku hizi mavazi ni ya aina nyingi sana, hakuna sheria wala mpangilio, kila kitu kinachovaliwa ni ubunifu wa mtu fulani, na lazima kuna watakaokubali na watakaoshangaa au kuchukia.
  Naomba tushee maoni nguo tunazopenda au kushangaa au kuchukia japo bado ni maarufu.

  Mie huwa nakerwa sana na watu wanaoacha bukta, au nguo za ndani zozote kuonekana hadharani, ama wanapotoka wakiwa wamevaa vesti, najisikia kama wanajidhalilisha.
  Kuna ile style ya kuvaa top fupi na low cut trousers au skirt ambapo ukijigusa tu mwili unaonekana, hasa kwenye public transport au mabenchi ha public places.

  jamani mwenzenu nakerwa na viatu vichafu!!!
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ukisema unaambiwa kila mtu ana maamuzi ya kuvaa vile anavyojisikia wengine ndio kwanza wanakuwa hawana habari na wewe wanaona kama unaimba ngonjera kuna siku niko kwenye gari dada wa watu amevaa G STRING kila mtu anaiona watu wakawa wananong'onezana yeye wala hana habari na mtu nikasema sijui nyumbani wakati anatoka hakuna aliyemwambia
   
 3. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli tunaenda kubaya...nadhani umarekani na utandawazi tunaoshabikia utaharibu kizazi hiki cha dotcom...wengine wameolewa kabisa lakini mhh unaona aibu hata kumtazama ila ndio uhuru huo tulionao..majuzi nasikia Erykah Badu kafungwa kwa kutembea uchi nadhani sasa kuonesha za ndani haikutosha so kachojoa zote na kutembea uchi...nadhani maadili yarejewe na wazazi japo ndio watoto wa siku hizi wanaona haana wa kuwazuia si wanaona US na kwingine na kudhani wako kama Ciara,Beyonce au Lil wayne..
  kwa kweli kimaadili tumepiga hatua nyuma coz hawa malil wayne wanajidhalilisha wao na wazazi wao pia kwa mavazi yao ya aibu hasa wanayoiga kwenye TV nk...BET waliifungia video ya Ciara (ride) lakini hapa bongo yapigwa mchana kweupe na wanaoona ni watoto na mahausgel wanaokuwepo home muda huo. Lady GAGA ni mfano wa kituko kingine cha msanii na ndio wanapendwa na watoto na vijana wa kisiku hizi hakika inakera.
  zamani ukikosea unachapwa hata na jirani lakini siku hizi thubutu yako..mtachapana na mzazi mwenzio. so nadhani tatizo hili la maadili tulitazame kwa undani zaidi kwani jamii inazidi kuharibika..majuzi niko na wife tukakuta vibinti vidogo nahisi vya form one kituoni vinangoja usafiri mashati ya shule ni vitop vyeupe yani ukichomekea hata hakichomekeki nikabaki najiuliza walimu shuleni hakuna au ndio wale wa voda fasta walioenda kozi miezi miwili(haihitaji kwenda college wangeiona tu)...nilijiuliza bila majibu.
  hili la mavazi tujitazame vizuri na tutazame watoto wetu,wadogo zetu,dada zetu,kaka zetu na tusikae kimya tuseme hata kama watabishana ila ujumbe umefika na mabadiliko yatakuja tu hata kama mchina nae anachangia kuharibu kwa kuleta style za kimajuu kwa bei chee basi tuwe makini na tuvunje ukimya iwe home,kwenye daladala au ofisini.
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hapo umenena vizuri sana:tea:
   
 5. D

  Dick JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanalonga eti ni maendeleo!
   
 6. H

  Haika JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Haswa!!
  sasa swali langu vizuri ndio aje?
  manake nilisikia kuna hospitali wamekataza wanawake kuingia na suruale, je suruale nayo vazi baya? kwa wengine ni baya?
   
Loading...