Mavazi yanataka kunikosesha mke, nishaurini

Mavazi yanataka kunikosesha mke, nishaurini

Usitake kuaminisha watu kuwa suti ni vazi tu, tambua kuwa suti ni kwa ajili ya class fulani kisha amua kuendana nayo au uwe kenge kwenye msafara.

Live up your standards.[emoji1614][emoji276]
[emoji3][emoji3] dah!
 
Mimi madem wanaonizunguka au naokutana nao kwenye mizunguko ya kazi yangu wqnaogopa kunipiga mizinga...aiseee
 
This is true. Ila kwa upembuzi yakinifu niliokwishaufanya, hapa ofisini sijaona wa kufanana naye.
Angalia na school mates kuanzia primary hadi chuo kama ulifanikiwa,unaweza kupata mnaeendana kidogo
 
Wakuu, habarini za wakati huu na poleni na mabadiliko ya tozo za miamala ya kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.

Kuna nyakati kweli tunafanya mizaha lakini hapa nawashirikisha jambo hili 'on a serious note', comment ukiwiwa kufanya hivyo, usipojisikia soma tu halafu pita, usinikejeli au kunitusi; lakini ukifanya hivyo amini kwamba nimeshakusamehe.

Mimi ni kijana ambaye ndiyo naanza maisha. Kazi ninayoifanya inanilazimisha nivae SUTI kila siku kuanzia j3-Ijumaa, tena kuna wakati nikiwa na kazi maalumu navaa mpaka jumamosi, kwahiyo mara nyingi nakutana na mabinti nikiwa nimevaa vazi hilo, suti zinakuwa za rangi tofauti tofauti; niwe ofisini, mgahawani, mtaani n.k.

Shida ni kwamba mabinti wengi wanapenda muonekano wangu, lakini pili wengi WANAAMINI nina pesa nyingi, so najikuta naombwa pesa sana. Kuna binti mmoja ambaye nilidhani anaweza kuwa mke..huyu tulianza vizuri, hakuomba pesa wala vocha kwa wiki 3 za kwanza, baadaye akaanza kidogokidogo nikawa nam-support, nilikuja kuchoka siku ananiomba milioni 2 za mtaji wa biashara fulani aliyotaka kuifanya, halafu tatizo lingine kubwa akawa hana subira. Nikimwambia asubiri nimtafutie ananuna, anaamini ninayo ila namnyima kumbe kweli sina.

Week end ndiyo navaa casual. Nifanyaje kaka zangu na dada zangu? Ili niwaaminishe suti ni vazi tu. Manake mwingine akikukuta na suti yani hakuelewi ukimwambia huna pesa.

Naombeni msaada wenu. Asanteni.
Tatizo la wavaaji suti wanajiona hii nchi ni mali yao ndio maana mnakuwa victims of the society.
 
Back
Top Bottom