Mavazi yanataka kunikosesha mke, nishaurini

Mavazi yanataka kunikosesha mke, nishaurini

Kabla hujamtongoza, unaandika sms!.

SUTI NI KASHA TU.
MIMI HALISI NI BILA YA SUTI. PESA PIA SINA, HII NI UNIFORM.

Ahsante ndugu mtongozwaji.

Wa kweli utampata.
[emoji3][emoji3]
 
Wanawake wana Akili sana. Huyo Aliingia Kwa Gear hiyo ili umuone Wa Maana kuliko Wengine. Ila Subiri Moto wake.bora wale wanaojionyesha Mapema
 
Kabla hujamtongoza, unaandika sms!.

SUTI NI KASHA TU.
MIMI HALISI NI BILA YA SUTI. PESA PIA SINA, HII NI UNIFORM.

Ahsante ndugu mtongozwaji.

Wa kweli utampata.
🤣🤣🤣🤣
 
Wakuu, habarini za wakati huu na poleni na mabadiliko ya tozo za miamala ya kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.

Kuna nyakati kweli tunafanya mizaha lakini hapa nawashirikisha jambo hili 'on a serious note', comment ukiwiwa kufanya hivyo, usipojisikia soma tu halafu pita, usinikejeli au kunitusi; lakini ukifanya hivyo amini kwamba nimeshakusamehe.

Mimi ni kijana ambaye ndiyo naanza maisha. Kazi ninayoifanya inanilazimisha nivae SUTI kila siku kuanzia j3-Ijumaa, tena kuna wakati nikiwa na kazi maalumu navaa mpaka jumamosi, kwahiyo mara nyingi nakutana na mabinti nikiwa nimevaa vazi hilo, suti zinakuwa za rangi tofauti tofauti; niwe ofisini, mgahawani, mtaani n.k.

Shida ni kwamba mabinti wengi wanapenda muonekano wangu, lakini pili wengi WANAAMINI nina pesa nyingi, so najikuta naombwa pesa sana. Kuna binti mmoja ambaye nilidhani anaweza kuwa mke..huyu tulianza vizuri, hakuomba pesa wala vocha kwa wiki 3 za kwanza, baadaye akaanza kidogokidogo nikawa nam-support, nilikuja kuchoka siku ananiomba milioni 2 za mtaji wa biashara fulani aliyotaka kuifanya, halafu tatizo lingine kubwa akawa hana subira. Nikimwambia asubiri nimtafutie ananuna, anaamini ninayo ila namnyima kumbe kweli sina.

Week end ndiyo navaa casual. Nifanyaje kaka zangu na dada zangu? Ili niwaaminishe suti ni vazi tu. Manake mwingine akikukuta na suti yani hakuelewi ukimwambia huna pesa.

Naombeni msaada wenu. Asanteni.
Kwanza muweke wazi kuwa vazi lako ni hali tofauti na kipato chako utaokoa mengi
Unadhifu huficha umaskini
 
Wanawake wana Akili sana. Huyo Aliingia Kwa Gear hiyo ili umuone Wa Maana kuliko Wengine. Ila Subiri Moto wake.bora wale wanaojionyesha Mapema
Hakika mkuu. Yani wale wanaonifichaga uhalisia wao mapema ni wabaya kuliko wale waokuwaga wawazi.
 
Back
Top Bottom