Mavazi ya uchi kwa dada zetu

Kivia

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
278
32
Mavazi ya uchi na kubana limekuwa tatizo kubwa sasa hapa tz . Tabia hii ya mmomonyoko wa maadili, ilianza kidogokidogo na sasa imekuwa kama kawaida kwani mpaka kwenye nyumba za ibada wanakwenda na hivi vijisuruali mmbano[big G] bila hata ya woga. Swali langu. 1. TUFANYEJE ILI KUKOMESHA TATIZO LA KIMAADILI ? 2. NANI ALAUMIWE- serikali/jamii yenyewe.?
 
Uchi huwa hauvaliwi ila tatizo ni pale tu mtu anapokuwa amavaa nguo zinazoonesha maumbo ya siri hapo ndio tunasema kuwa mtu kavaa nusu uchi au mavazi ya Uchi kiasi mwili wote haufunikwi kwa mavazi hasa zile sehemu ambazo tuanaita uchi
Hivi uchi huwa unavaliwa?
 
Uchi huwa hauvaliwi ila tatizo ni pale tu mtu anapokuwa amavaa nguo zinazoonesha maumbo ya siri hapo ndio tunasema kuwa mtu kavaa nusu uchi au mavazi ya Uchi kiasi mwili wote haufunikwi kwa mavazi hasa zile sehemu ambazo tuanaita uchi
nashukuru kwa ufafanuzi,ubarikiwe sana.
 
Ndio mambo ya maendeleo hayo.
Si unajua kila kitu waafrika tunaiga tu?
Hata nguo ndefu na pana tuliletewa na wakoloni....
vyote tu ni mwendo wa kuiga tu.
Wazungu wakianzisha fashion ya nguo pana na ndefu waafrika tutaiga tena...
 
Tatizo sio uvaaji uchi, tatizo ni malezi yako ulio lelewa ndio yanakupeleka uwaze ngona kula ukiona dada kavaa nguo za kubana.
 
Mfano ni hako katoto hapo
nashukuru kwa ufafanuzi,ubarikiwe sana.

12.+MASHABIKI.JPG
 
Mavazi ya uchi na kubana limekuwa tatizo kubwa sasa hapa tz . Tabia hii ya mmomonyoko wa maadili, ilianza kidogokidogo na sasa imekuwa kama kawaida kwani mpaka kwenye nyumba za ibada wanakwenda na hivi vijisuruali mmbano[big G] bila hata ya woga. Swali langu. 1. TUFANYEJE ILI KUKOMESHA TATIZO LA KIMAADILI ? 2. NANI ALAUMIWE- serikali/jamii yenyewe.?

Kuzuia hizo nguo zitokako!
 
Hivi dunia iige dini au dini iige dunia???
Hivi kati ya mfuasi wa Yesu na mfuasi wa shetani nani wa kuvuta mwenzake kwenda kwake?
Hivi kati ya mfuasi wa Mohamad (s.a.w) na mfuasi wa ibilisi nani wa kumvuta mwenzake kwenda kwake?
 
mtakapoacha kuwashobokea na hasa kwa kuwasifia kwa unafiki kuwa wanapendeza hata kama ni demu wako ndipo watabadilika na kuvaa mavazi ya heshima.
 
biashara matangazo; zinatafutwa hela za mafuta ya gari hapo....

mjasiri haachi hasiri,ukimwangalia huyu kiumbe utaligundua hilo ya kwamba hyo ndo hasiri yake ya kuvua eti kisa pesa ya mafuta kumbe hata kula kwenyewe mawazo
 
Mavazi ya uchi na kubana limekuwa tatizo kubwa sasa hapa tz . Tabia hii ya mmomonyoko wa maadili, ilianza kidogokidogo na sasa imekuwa kama kawaida kwani mpaka kwenye nyumba za ibada wanakwenda na hivi vijisuruali mmbano[big G] bila hata ya woga. Swali langu. 1. TUFANYEJE ILI KUKOMESHA TATIZO LA KIMAADILI ? 2. NANI ALAUMIWE- serikali/jamii yenyewe.?

Hapa Jamii na Serikali wote wanahitaji kulaumiwa maana katika jamii kuna wazazi ambao hata watoto wao wakivaa hivyo wanaona ni sawa kabisa kwa sababu wanahusika kuwaninulia nguo kama hizo. Kwa kasi hii wazazi na Walezi wengi wanahusika na wanadai ni kwenda na wakati. Kwa upande wa pili Serikali nayo inahusika kwa sababu haikemei hii tabia na raia wakithubutu kuwashughulikia watu kama hao serikali inawachukulia hatua. Mfano, kipindi Mh Jakaya Kikwete ameshinda urais October 2010 nilikuwa mwanza halafu raia wakaanza kuwashughulikia wanaovaa nusu uchi kwa kuwavua kabisa nguo hizo. Mfano wengine walikuwa wakifunga kanga na ndani yake kuna chupi tu na wengine ni kanga bila chupi. Sasa serikali ilipoona hivyo ilipiga marufuku lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na serikali kuwakabili hao akina dada zetu. Kwa hali hii bila serikali kutoa tamko kuwa ni marufuku kuvaa mavazi kama hayo na atakayebainika anachukuliwa hatua kali basi watatembea uchi kabisa maana wamefikia hatua mbaya ya kuingia makanisani na nguo za ajabu sana. SERIKALI ITOE TAMKO NA LITAISHA.
 
Last edited by a moderator:
Mi nashangaaga sana nikiona mtu anahangaika na yasiyomuhusu. As long as mtu hanikeri, hajaingilia utaratibu wangu wa maisha, na sio mwanangu? I dont freaking care what and how they dress up
 
Mi nashangaaga sana nikiona mtu anahangaika na yasiyomuhusu. As long as mtu hanikeri, hajaingilia utaratibu wangu wa maisha, na sio mwanangu? I dont freaking care what and how they dress up

King'asti Zima moto kwa jirani kabla hujafika kwako.....hili ni tatizo lipo kwenye jamii tusipochukua hatua sasa kuna siku litafika mpaka hapo kwa mwanao!
 
Back
Top Bottom