Mavazi ya dada zetu kwenye nyumba za ibada

babajnr

Member
Joined
Mar 6, 2013
Posts
98
Reaction score
13
Nimehudhuria kanisani leo, nashangaa baadhi ya mabinti wanavaa nguo za aibu hadi uongozi wa kanisa ninako sali wamepitIsha azimio la kuwavika kanga wanawake watakaokuja na nguo zisizo na staha kanisani....,
maswali yangu ni kwamba mwanamke anapovaa nguo isiyo na staha kanisani huwa anamfurahisha nani? Pia huwa najiuliza hata kwenye bendi za muziki ukitazama wacheza shoo wa kiume na wa kike utashangaa tofauti ya uvaaji wao, maana utakuta wanaume wamevaa kiheshima sometimes suti kabisa lkn kwa dada zetu daaaaaaaaahhh wanavaa nguo za kubanaaa na vitovu vikiwa nje, halafu wanaharakati wa haki za kijinsia wapo kimyaaa. Big up kwa wanawake wote wanaovaa nguo za heshimu kwa maadili ya ki-tz.
 
i have done this for the good-will my friends,so plz don't shot towards my thread...
 
Waliumbwa ivo maskin wasemehe, hebu fikilia historia yao kuanzia bustanini....4giv women!
 
dah muda wa kuangalia nguo mnapataga wapi mkiwa kwa church?
 
Mwanamke au mwanaume ukishajua kwanini unaenda kanisani na unaenda kwenye nyumba ya Mungu wa aina gani utaweza kuchanganua pia uende na nguo ya aina gani na kwa muonekano wa aina gani. Tatizo ni kwamba tunaenda kanisani kimtindo na hatujamuelewa aina ya Mungu tunayemuabudu kwamba ni wa kuheshimiwa na hivyo tunapaswa kumheshimu pia. Kama malaika watakatifu wanamuheshimu huyu Mungu wakimsujudia masaa 24 je sie viumbe wadhambi tusio fikia hata kiwango cha robo cha hao malaika kwanini tusimuheshimu?? tunaenda na viguo vyetu vya ajabu ajabu ambavyo hata watu wa duniani wasiomjua Mungu wakituona wanatushangaa, kanisani tuko busy na simu, minong'ono na mengine mengi. Kama tutaendela na utaratibu huu wa ibada ya mtindo ni heri tusiende kusali kabisa kwani haina maana yoyote ni kupoteza muda tu.

Kwa namna moja au nyingine mimi pia nimehusika ila tunahitaji neema ya Mungu.
 
Waliumbwa ivo maskin wasemehe, hebu fikilia historia yao kuanzia bustanini....4giv women!
una uhakika kuwa mungu aliwaumba hivyo??? acha kupotosha. ni binaadamu wenyewe ndio wanajidhalilisha
 
Mwanamke au mwanaume ukishajua kwanini unaenda kanisani na unaenda kwenye nyumba ya Mungu wa aina gani utaweza kuchanganua pia uende na nguo ya aina gani na kwa muonekano wa aina gani. Tatizo ni kwamba tunaenda kanisani kimtindo na hatujamuelewa aina ya Mungu tunayemuabudu kwamba ni wa kuheshimiwa na hivyo tunapaswa kumheshimu pia. Kama malaika watakatifu wanamuheshimu huyu Mungu wakimsujudia masaa 24 je sie viumbe wadhambi tusio fikia hata kiwango cha robo cha hao malaika kwanini tusimuheshimu?? tunaenda na viguo vyetu vya ajabu ajabu ambavyo hata watu wa duniani wasiomjua Mungu wakituona wanatushangaa, kanisani tuko busy na simu, minong'ono na mengine mengi. Kama tutaendela na utaratibu huu wa ibada ya mtindo ni heri tusiende kusali kabisa kwani haina maana yoyote ni kupoteza muda tu.

Kwa namna moja au nyingine mimi pia nimehusika ila tunahitaji neema ya Mungu.
Malaika wa Mungu wana nguo???
Mungu alituumba na nguo???
Mungu hakwaziki (not embarrassed) na nini tunavaa nje ni binadamu ambao wapo mabarabarani, maofisini, kanisani na misikitini ndio wanaokwazika.
 
Kama wote tungekuwa tunawaza chanya namna hii tusingekuwa hapa tulipo. Thanks 4 this quote
 
Malaika wa Mungu wana nguo???
Mungu alituumba na nguo???
Mungu hakwaziki (not embarrassed) na nini tunavaa nje ni binadamu ambao wapo mabarabarani, maofisini, kanisani na misikitini ndio wanaokwazika.

Soma biblia kitabu cha ufunuo habari ya maserufi kwamba wamejifunika nyuso zao kwa mbawa zao kuonesha heshima kama wewe ni msomaji wa biblia. Lingine sijasema malaika wanavaa nguo, nimesema hata sisi katika ubinadamu wetu lazima tuoneshe heshima kwa Mungu aliyetuumba kwa mavazi yetu na mionekano yetu hasa tuwapo ibadani kama duniani tumeshindwa. Mungu anakwazika na ndio maana aliangamiza sodoma na gomora, aliangamiza kwa gharika .

Baada ya dhambi nguo zilitafutwa kumbuka adam na hawa walitafuta magamba ya miti kujifunika ili kuficha aibu zao. All in all heshima kwa mungu inasisitizwa katika biblia.

Hata huko kwenye mazingira tunayoishi twapaswa kuwa mfano biblia inasema Muwe mfano kwa mavazi na mienendo yenu; Ni mavazi gani basi yanayozungumziwa ya sisi kuwa mfano kwayo kama tuliumbwa uchi na hivyo mavazi hayana maana as per your question??

Ninajua binadamu anapoamua kuhalalisha upumbavu au dhambi yake anaipindisha biblia hiyo hyo ili apate uhalali wa kufanya akifanyacho. Sawa umehalalisha kibiblia je ni inakubalika kitamaduni zetu kuvaa nguo za kubana na kuonesha matiti na mapaja yetu????

Btw siko hapa kukuridhisha as sijawahi kutoa jibu ukaridhika.
 
Malaika wa Mungu wana nguo???
Mungu alituumba na nguo???
Mungu hakwaziki (not embarrassed) na nini tunavaa nje ni binadamu ambao wapo mabarabarani, maofisini, kanisani na misikitini ndio wanaokwazika.

Duuu Kaunga hata huogopi? kwamba Mungu hakwaziki na nini tunavaa? Umenukuu wapi hiyo? Si maandiko matakatifu (Biblia)yanasema wanawake wavae nguo za heshima (modestly). Soma Biblia 1 timotheo 2:9 (In like manner also, that women adorn themselves in modest apparel, with shamefacedness and sobriety; not with broided hair, or gold, or pearls, or costly array). Ni kujidanganya na ni mawazo kutoka kuzimu kwa shetani kwamba Mungu hakwaziki na kile binadamu anafanya. Kumbuka usemayo na ufanyayo ndiyo yaliyokujaa moyoni.
 
Kanisa lenyewe limegeuka kama club, sehemu ya mawindo.

Usitake kutibu TB kwa Cofta.

Swali limezama mpaka kwenye subconscious wewe unaliangalia juu juu tu.

Hao wote wanakataa utakayifu wa kanisa. Hiyo ni vote of no confidence.

You can force a donkey to the stream, but you can't force it to drink the water.
 
Hiviii; Mungu yupo kanisani tu? Bafuni kwangu hayupo? Wakati namanua nikiwa natotoa dume langu pale maternity ward hakuwepo? Zaidi ya kuona mapaja yangu, Mungu anakuwa embarrassed na roho yangu inayokuwa nzito kuwasaidia wenye shida, roho yangu inayotamani mali za wengine, roho yangu inayo sengenya na ya kinafiki kama yawayahudi ambao siku ya leo wamemshangilia Yesu na kumsulubu next week.
Duuu Kaunga hata huogopi? kwamba Mungu hakwaziki na nini tunavaa? Umenukuu wapi hiyo? Si maandiko matakatifu (Biblia)yanasema wanawake wavae nguo za heshima (modestly). Soma Biblia 1 timotheo 2:9 (In like manner also, that women adorn themselves in modest apparel, with shamefacedness and sobriety; not with broided hair, or gold, or pearls, or costly array). Ni kujidanganya na ni mawazo kutoka kuzimu kwa shetani kwamba Mungu hakwaziki na kile binadamu anafanya. Kumbuka usemayo na ufanyayo ndiyo yaliyokujaa moyoni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom