Badala ya kushughulikia mambo muhimu, mnaanza kujadili mavazi? Is it the most burning issue? Mbunge akivaa hivi au vile inachangia nini kwenye maendeleo ya mwananchi. Mbunge badala ya kuzingatia hoja zinazotolewa na wabunge wengine makini ana concentrate kuangalia mavazi ya wanawake na wanawake badala ya kupeleka hoja bungeni wanapeleka vivutio vya maungo yao kwa wanaume Bungeni. Hili ni Taifa la watu wasio makini kabisa. Tutegemee maendeleo gani.
Ndio waseme sasa ili mtu akikiuka iwe issue, sio kujadili sasa wakati hakuna utaratibi maalumu.
Kwani kuna kipimo cha mavazi ya kuendea bungeni? Nchi yenyewe imeshindwa hata kupata vazi la Taifa utaanzaje kumpangia mtu avae mavazi ya wazungu au ya waarabu? Angechaguliwa mrisho mpoto kwenda bungeni angebadilishiwa mavazi?
Kuna nguo mahsusi za kuvaa bungeni,huwezi kuvaa kaptula au jeans au fulana bungeni na ukavumiliwa huenda bunge hili,kwa taarifa aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa kadhaa nchini Nsa Kaisi aliwahi kutolewa bungeni ,baada ya kutinga akiwa amevaa jeans.Bungeni sio bar ,hata baadhi ya hoteli zina miiko ya uvaaji,bungeni si uswazi.
Akili, busara, uelewa, havina uhusiano na urefu wa nguo! Hapa kazi tu, mengine waachie wahusika na masharti au sheria za maandiko yao. Hatuhitaji tena upuuzi wa kuchanganya imani zetu na utanzania wetu!
Habari hio ingenoga sana kama ingeambatana na picha
Sijui nikusaidiaje!!
Kwani we ni mgeni nchi hii?hiyo ni kama zile degree za nguo ya ndani sijui nyie vijana mnaita chupi90% ya wanaovaa robo tatu uchi ni wabunge wa Viti Maalum sijajua mahusiano ya vimini na Ubunge wa Viti Maalum!!
Kwahiyo unaona sawa wao kuvaa vimini kama unavyovaa wewe?