Kama ni Muislam, hakikisha sala zako za faradhi (tano kwa siku) hazikupiti na hakikisha unakuwa udhu saa zote na unapoingia kulala hakikisha una udhu na unasoma Qur'an japo sura tatu ndogo za mwisho kila moja mara tatu.
Yaani kama ningepata dawa ya kumuona na kumgandiha akiwa anafanya mambo yake hiyo ingekua evidence kubwa sana...
ukwe wenza wa mama ako na mama ako wa kambo wewe haukuhusu. mama ako na gurupu lake la marafiki majirani muachie wamsaidie kulilia wivu sio wewe mtoto wa kiume wa kutegemewa kuitwa baba unamsaidia mama ako na marafiki zake kuwa na wivu.
aisee hiyo ni aibu kwa mtoto wa kiume sio siri, yaani umetiwa kasumba chuki barabara ya kumchukia mke wa baba ako na wewe kwa akili zako fupi umeyabeba na ukayajaza tele akilini, na kumwita mama ako wa kambo mchawi.
Acha kuwa na akili changa zako na za kuchangiwa.possibility kubwa kuwa wewe hufanyi kazi kabisaa, kwa hiyo kijana fikiria maisha yako yatakuwaje na vipi utaweza kupata pesa za halali kwa ajili ya maisha yako mwenyewe kuliko kuendelea kukaa nyumbani mpaka saivi wakati ullitakiwa uwe na maisha yako na mkeo na wanao.Fikra potofu za uke wenza achana nazo na umwambie mama " wivu utakuja kukutia maradhi hii baba ni haki yake kisheria najua inauma lakini VUMILIA"
Paw please,mada hii ni ya mmu!Usiku huu wa saa nane kasoro nipo macho sina hata usingizi na huko nje ya nyumba nasikia vishindo ila watu hawaonekani...
Ni hivi... baba yangu ana wake wawili ambao ni mama yangu na ma mdogo na wote anaishi nao nyumba moja (na mi naishi hapa nyumbani maana sijaanza kujitegemea)
Sasa tatizo kubwa ni mauzauza ya nyumba hii... 90% ya watu mtaani kwetu wanajua kabisa huyu mama yangu mdogo ni mchawi. Kuna watu hapa mtaani washawahi kugombana nae wakimwambia aache kuwawangia.
Mi mwenyewe alishawahi kunitokea ndotoni na wenzake wakiwa wamevaa kaniki, nilishtuka usingizini na kupiga kelele sana, but nkaamua kupotezea tu sikuwahi kumwambia mtu.
Baba nae kahisi karogwa na kapewa limbwata juu maana yupo ka zuzu, inshort katekwa sana akili. Ukimwambia mkewe mchawi ugomvi unaanzia hapo..
Maelewano ya familia ya mama mdogo na familia yetu ni madogo sana maana tunajua dhahiri pasi na shaka kuwa huyo maza anaturoga na kutufanyia mauzauza na shida yake kubwa sie tupotee hapa ili ye atawale.
Kiukweli maisha haya ya kurogana na kuwangiana daily mimi binafsi nimeyachoka sana. Natamani nihame hapa home ila tatizo sina kazi itayoniwezesha kujitegemea.
Yaani sasa hivi akili ishachanganyikiwa kabisa, natamani hata kumuua huyu mama ili tuishi kwa amani.
Nipeni mawazo maana nahisi nishadata na ntapoelekea ntakuja kumtoa roho huyu mtu. Au kama kuna mtu anajua dawa ya kukomesha uchawi (apart from maombi au kwenda kwa waganga) anisaidie jamani
NB: Nishaomba na kusali sana ila mauzazuza ya usiku yapo vile vile.
Msaada wenu wakuu
Ndugu mi nshaomba sana... ila huyu mama ni kiboko,kila siku afadhali ya jana
Faiza Foxy nakukubali. somo tosha kwa sisi wote. ulipitia madrasa ya baba ake Sheikh Yahya Hussein pale Kinondoni nn??!!Kama ni Muislam, hakikisha sala zako za faradhi (tano kwa siku) hazikupiti na hakikisha unakuwa udhu saa zote na unapoingia kulala hakikisha una udhu na unasoma Qur'an japo sura tatu ndogo za mwisho kila moja mara tatu.
Kama husomi hama hapo kwa baba yako, nenda kajitegemee hayo mambo ya wake za baba yako mwachie mwenyewe , wewe hayakuhusu.
Tafuta chumba cha bei rahisi panga Anza kujitegemea mambo ya kukaa kwa wazazi utakuwa unakosoa kila kitu,kila kitu utakuwa unaona hakiendi sawa.
Kama ni Muislam, hakikisha sala zako za faradhi (tano kwa siku) hazikupiti na hakikisha unakuwa udhu saa zote na unapoingia kulala hakikisha una udhu na unasoma Qur'an japo sura tatu ndogo za mwisho kila moja mara tatu.