Mauza uza: Maalim bado anatumia Huduma za Serikali ya Zanzibar

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
485
Mwanadamu ameumbwa na milango ya fahamu. Milango hiyo ya utambuzi humsaidia mtu kuelewa kitu au jambo liliopo. Huweza kutambua kitu kwa kukishika, kukisia, kufikiria au kudhani. Lakini kwa vile milango hiyo ni mingi, binadamu anao uwezo wa kugusa, kuonja, kunusa au kusikia. Hata hivyo, mwanadamu huweza kumghilibu binadamu mwingine au kumdanganya kwa kutumia milango hiyo ya utambuzi na hatimaye kumpotosha. Upo uwezo wa kudanganya macho ili yaone mambo kinyume na yalivyo. Mtindo huo huitwa ?mauzauza? au ?kiinimacho?. Katika Bunge la Tanzania, hivi majuzi kambi ya upinzani walionesha mchezo huo wa ?mauzauza? au ?kiinimacho? mbele ya Rais wetu na viongozi kadha wa kitaifa.

Na kwa vile vyombo vya habari vilitangaza na kuonesha vituko na viroja vyao, hali ilikuwa dhahiri shahiri. Viongozi wa genge la upinzani walisimama na kutaka Rais halali wa Zanzibar Dkt. Shein eti asiingiye Bungeni kwa kudai kuwa si Rais halali wa Zanzibar na muda wake wa uongozi umekwisha. Kama hilo halitoshi, walionesha ujinga wao na ushenzi wao kwa kuzomea Bungeni na kufanya fujo. Nia yao ni ilikuwa kumtetea Maalim kuwa ndiye aliyeshinda wakati Tume ya Uchaguzi chombo halali hakijamtangaza. Maalim alifanya makosa makubwa kwa kujitangazia ushindi wa Urais wa Zanzibar.

Nilidhani kambi ya upinzani wakati wanasema Dkt. Shein siyo Rais halali wa Zanzibar basi na wakati huo huo mshirika wao wa UKAWA Maalim naye angeandika barua rasmi ya kujiuzulu nafasi yake ya Umakamo wa Kwanza wa Rais kwani na yeye muda wake umekwisha. Hawawezi wapinzani kumtaka Dkt. Shein Rais wa Zanzibar aondoke Ikulu lakini UKAWA wanapata kigugumizi cha kumwambia Makamo wa Kwanza na yeye atoke Ikulu! Nilikuwa Zanzibar juzi, nilishtuka na kushangaa nilipomwona Maalim amepanda gari yenye nembo ya serikali ya Zanzibar pembeni mwa gari hiyo ipo bendera inapepea ya SMZ. Mbele ya gari ya Maalim ipo pikipiki ya polisi na gari za polisi za Serikali ya Muungano. Nyuma ya gari yake wapo askari na sare zao wameshika silaha za ulinzi.

Niliambiwa kuwa gari ile ilikuwa inatokea ofisini pake Migombani ambayo imeandikwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mlangoni hapo ofisini pake walinzi wake wakampa saluti ya nguvu ya heshima. Naye bila kuchelewa huku akikenya akaipokea. Baada ya udadisi wangu nikaambiwa bado anaishi katika jengo linalolipiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hata huduma za nyumbani kwake bado zinabebwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hata safari zake; za kwenda nje ya Unguja kama Pemba na Dar es Salaam, ndege aitumiayo hulipwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Sina hakika kama mshahara wa mwezi wa Novemba kama atapokea au la! Ni dhahiri bado anahudumiwa kiofisi na kimasilahi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Analindwa na Serikali ya Muungano.

Nini tunajifunza? Wanayoyasema UKAWA siyo wanayoyatenda. Kama bungeni walikataa Dr. Shein asiingiye bungeni kwa sababu siyo Rais halali wa Zanzibar kwa nini hao hao wasimtake Maalim aandike barua ya kujiuzulu umakamo? Kwa nini wasimtake aache kuishi Ikulu, akataye ulinzi, asitumie gari la serikal na bendera? Kwa nini asiache kutumia ndege za serikali na akitaka kwenda Pemba apande jahazi?

Hivi wale wabunge wa kambi ya upinzani waliokuwa Dodoma si wanatakiwa wamwombe radhi Rais Magufuli, Rais Shein na Watanzania kwa utovu wao wa adabu? Waombe radhi kwa kuwadanganya Watanzania kusema kuwa Rais Shein siyo Rais halali wakati mshirika wao wa UKAWA Maalim bado anang?ang?ania Ikulu na kufaidi huduma za kimasilahi na ulinzi kwa fedha za walipa kodi? UKAWA waungame kuwa walichofanya ni ?mauzauza? na ?kiinimacho? tu.

(Dkt. MUHAMMED SEIF KHATIB)
 
Hapo kwenye Dkt ndo nashindwa kujua we ni dkt wa majip au majip aina ya gari.
 
Dkt. MUHAMMED SEIF KHATIB- Una uhalali gani kuwaambia wabunge wa upinzani washenzi? Wapinzani nao wakimwambia huyo unayemtetea hivyo utakubali?
 
Tungo ndefu sana dokta, hii inaonyesha ww ni mtunzi hodari sana, endelea kutunga na utanufaika. Ila ulizia zaidi kwa hao waliokueleza ni nini kimetokea mpaka maalim akaendelea kutumja hizo facilities? Muulize tu sheni nahakika atakupa jibu
 
Niliambiwa kuwa gari ile ilikuwa inatokea ofisini pake Migombani ambayo imeandikwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mlangoni hapo ofisini pake walinzi wake wakampa saluti ya nguvu ya heshima. Naye bila kuchelewa huku akikenya akaipokea. Baada ya udadisi wangu nikaambiwa bado anaishi katika jengo linalolipiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hata huduma za nyumbani kwake bado zinabebwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hata safari zake; za kwenda nje ya Unguja kama Pemba na Dar es Salaam, ndege aitumiayo hulipwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Sina hakika kama mshahara wa mwezi wa Novemba kama atapokea au la! Ni dhahiri bado anahudumiwa kiofisi na kimasilahi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Analindwa na Serikali ya Muungano.

(Dkt. MUHAMMED SEIF KHATIB)
Hizo ni stahiki zake!, viongozi wote wakuu 6 wa nchi wanastahili hata wakistaafu!.

Hata Lowassa na Sumaye licha ya kuhamia Chadema, malipo, pensheni, gari, dereva, mafuta, walinzi, matibabu, na safari za nje, zinagharimiwa na serikali maisha yao yote!.

Pasco
 
hili nalo ni JIPU KUBWA SANA. magufuli tupia macho huko haiwezekani serikali iendelee kulipa mijitu ambayo inasubiri mshahara wa serikali hiyohiyo wanayosema haijafanya chochote miaka 50. sasa kama haijafanya chochote miaka yote hiyo mnadhani pesa ya kulipa mishahara yao inatoka wapi. wanailazimisha serikali kuwalipa kwa kukopa mabenki ya nje na kuongeza bure deni la taifa. nawashauri wakilipwa mshahara warudishe serikalini. kwa sababu wanatuongezea madeni buree
 
Mkuu usishangae, wanasiasa karibia wote (99%) wa TZ, cha kwanza kabisa ni maslahi binafsi vingine vyote visingizio tu!!

Hiyo asilimia moja ni ya Nyerere na Magufuli tu, the rest ni mule mule
 
Hizo ni stahiki zake!, viongozi wote wakuu 6 wa nchi wanastahili hata wakistaafu!.

Hata Lowassa na Sumaye licha ya kuhamia Chadema, malipo, pensheni, gari, dereva, mafuta, walinzi, matibabu, na safari za nje, zinagharimiwa na serikali maisha yao yote!.

Pasco

Vyeo, ofisi, bendera na stahiki za viongozi walioko madarakani i. e. pikipiki haviwahusu. Maalim Seif bado ni makamu wa kwanza wa rais HALALI kabisa
 
Maalim anatumia hi yo vitu kama mshindi halali wa urais Zanzibar
 
Maalim seif ana kila sababu ya kutumia facilities za serikali, ndiye Rais aliyechaguliwa na wazanzibar october 25. Tatizo kuna 'shetani' anamzuia, lakini haijawahi kutokea shetani akamshinda Mungu.

Siyo vizuri kuwaita wenzako eti ni washenzi, siamini kama ni wewe, labda mzimu wako! Hivi kati ya aliyeng'ang'ania madaraka hata baada ya kukataliwa na wananchi na anayedai haki yake ya kuongoza kwa kutii uamzi wa wananchi, nani mshenzi?

Juzi prof kitila mkumbo alisema eti kuna upinzani 'uchwara',ikumbukwe kuwa hata yeye yuko upinzani 'uchwara' wa ACT. Hapa ndipo madokta na maprofesa wa tz huniacha hoi! Kwa nini utumie matusi kufikisha ujumbe? Kama hoja ni nzuri/ina mantiki haihitaji 'kusindikizwa' kwa matusi ili ikubalike. ARGUE, DON'T SHOUT!
 
Hizo ni stahiki zake!, viongozi wote wakuu 6 wa nchi wanastahili hata wakistaafu!.

Hata Lowassa na Sumaye licha ya kuhamia Chadema, malipo, pensheni, gari, dereva, mafuta, walinzi, matibabu, na safari za nje, zinagharimiwa na serikali maisha yao yote!.

Pasco

Labda kama sijamsoma vizuri mtoa mada. Lakini Sumaye, Lowassa na wengine wastaafu uliowataja, sijaona wakiwa na magari ya serikali yenye nembo na alama za nafasi zao za awali. mf Bendera, wakisindikizwa na pikipiki na wakiendelea kuzikalia ofisi za Serikali ati ni stahili yao mpaka wafe!!!
 
Tungo ndefu sana dokta, hii inaonyesha ww ni mtunzi hodari sana, endelea kutunga na utanufaika. Ila ulizia zaidi kwa hao waliokueleza ni nini kimetokea mpaka maalim akaendelea kutumja hizo facilities? Muulize tu sheni nahakika atakupa jibu

Huyu jamaa anasema kweli. Juzi pia nilimuona Maalim Seif akiwa na motorcade kama kawa. Niliuliza kwa watu waliokuwa pale wakasema ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanziba. Niliishiwa pumzi. Nilikuwa natokea GYM pale Colosseum ambapo si mbali sana na anapoishi. Nilimvulia kofia aisee. Tuweni wangalifu sana na wanasiasa wa Kiafrika. Wanaweza kuchoma nchi kwa kitu wasicjokimaanisha.
 
Tungo ndefu sana dokta, hii inaonyesha ww ni mtunzi hodari sana, endelea kutunga na utanufaika. Ila ulizia zaidi kwa hao waliokueleza ni nini kimetokea mpaka maalim akaendelea kutumja hizo facilities? Muulize tu sheni nahakika atakupa jibu

Mkuu unejaribu kumuuliza hizo facilities ni za nani?za ccm au wananchi
 
Kifaurongo maalim ndio rais wa zanzibar sasa mm sikuelewi nn unaongea dunia yote inatambua hivyo na anahaki ya kutembea na vingora hata hivyo in waziri kiongozi mstaafu anahaki kwa mujibu wa sheria za Zanzibar kupata ulinzi na marupu rupu yote samahani kama nimekuudh
 
Hizo ni stahiki zake!, viongozi wote wakuu 6 wa nchi wanastahili hata wakistaafu!.

Hata Lowassa na Sumaye licha ya kuhamia Chadema, malipo, pensheni, gari, dereva, mafuta, walinzi, matibabu, na safari za nje, zinagharimiwa na serikali maisha yao yote!.

Pasco
Mkuu umeambiwa bado yupo ofisini ,kwenye afisi rasmi ya makamu wa kwanza,labda anaenda ku browse internet tu
 
hili nalo ni JIPU KUBWA SANA. magufuli tupia macho huko haiwezekani serikali iendelee kulipa mijitu ambayo inasubiri mshahara wa serikali hiyohiyo wanayosema haijafanya chochote miaka 50. sasa kama haijafanya chochote miaka yote hiyo mnadhani pesa ya kulipa mishahara yao inatoka wapi. wanailazimisha serikali kuwalipa kwa kukopa mabenki ya nje na kuongeza bure deni la taifa. nawashauri wakilipwa mshahara warudishe serikalini. kwa sababu wanatuongezea madeni buree
Ni haki ya kila Mtz kuizodoa serikali, tatizo lenu mna link serikali na chama na ndio maana mtu akiponda serikali macho yanawatoka, usipoiponda serikali yako pale ambapo mambo hayaendi kombo utaiponda serikali ya nchi gani (lengo ni kupiga kelele irekebishe pale ambapo pamekwenda mrama, wale ni viongozi wa kitaifa hata kama waliondoka CCM na wana haki za kikatiba)
 
Yawezekana mtoa mada ni dkt kama alvondka lakn inategemeana ni dkt wa vitu gani!
 
Kama nimemuelewa mtoa mada ameshindwa kutofautisha kati ya chama na serekali,any way maalif seif ni rais mteule wa zanzibar.
 
Back
Top Bottom