Maumivu ya matiti machanga(yanayoanza kuota)

Mine eyes

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
6,464
7,140
Habar wanajamvi...
Nina mtoto wa dada yangu wa kike anatimiza miaka nane mwezi wa kumi na moja, lakini ni mwembamba na utadhani ana miaka sita.
Mara nyingi anasema maziwa yana muuma yakiguswa hata na nguo aliyo vaa....
Mama alipomkagua akakuta viziwa vyake vimeinuka na vina kokwa!
Sasa naomba kujua kamà kuna dawa yoyote na pia mbona yamewahi kikua hayo maziwa au ana tatizo kiafya??

Hii hali inamnyima raha hata kucheza akiruka yanauma, akiguswa kilio na pia anaona kama kaonewa vile maana wenzie hawana.
msaada kwa anayejua tiba
 
Pole sana, mwanao alipata tiba?
Pole sana anti, mwanao alipata tiba?

Hakupata mkuu...
kama unajua chochote tusaidie ndugu yangu..
vikokwa vinakuja tuu na kifuani hapa kati ya maziwa kama panagawanyika!
Inatusumbua sana ni mtoto
 
Ni kawaida. ..yatapona yenyewe. Mtoto wetu yalianza kuota akiwa na 7yrs only. Tulimpeleka mpaka hospital kwa hofu
Ila ni maumbile tu hamna zaidi. Muwekeni sawa tu kisaikolojia akubaliane na hali
 
Ni kawaida. ..yatapona yenyewe. Mtoto wetu yalianza kuota akiwa na 7yrs only. Tulimpeleka mpaka hospital kwa hofu
Ila ni maumbile tu hamna zaidi. Muwekeni sawa tu kisaikolojia akubaliane na hali

Asante kwa ushauri. Tununue sidiria tu!
 
Hiyo ni hali ya kawaida, itaisha...pia mwambie mpwa wako akiona mabadiliko yoyote kwenye mwili wake amwambie mama ake au ndugu wa kike

Mama alifariki kiufupi tunalea sisi na madada wa kazi.... lakini nashukuru kwa ushauri wako kwa sisi ni msaada mkubwa. Mana hospitali walisema itaisha pia lakini mbona kama yanaendelea kukua?!
Si atakuwa na ziwa kubwa kuliko umri,!?
 
Huyo akifikisha 15 zitamfikia magotini
 
Mama alifariki kiufupi tunalea sisi na madada wa kazi.... lakini nashukuru kwa ushauri wako kwa sisi ni msaada mkubwa. Mana hospitali walisema itaisha pia lakini mbona kama yanaendelea kukua?!
Si atakuwa na ziwa kubwa kuliko umri,!?
Khaaaaaa we mjomba wewe.....
Ukubwa wa maziwa inategemea inawezekana akarithi kutoka kwenye family yakawa makubwa, maziwa yakiwa yanaota huwa yanauma Kwahiyo ni kawaida, wewe huna hata dada zako wanaoweza kuongea nae hayo? Au ndo akivunja na ungo wewe ndo utamsaidia?
 
Khaaaaaa we mjomba wewe.....
Ukubwa wa maziwa inategemea inawezekana akarithi kutoka kwenye family yakawa makubwa, maziwa yakiwa yanaota huwa yanauma Kwahiyo ni kawaida, wewe huna hata dada zako wanaoweza kuongea nae hayo? Au ndo akivunja na unga wewe ndo utamsaidia?

Dah! Mpaka nimecheka yaani......
tuko baridi kidogo lakini nitajivua nijichanganye na mabint ili mradi nisaidiwe. Hapa nimekwama mtoto mwenyewe ukikaona ni kamwili kadogo halafu kapole basi kama anaonewa vile!
kuna mtu kani pm eti nipashe moto mwiko halafu unabandika kwenye maziwa... zile kokwa zitayeyuka pole pole!
Aagh!
Bora homa utajua utibu vipi.
 
Mjomba hebu mwache mtoto maziwa yasijekuacha kuota bure, afu ni wewe huyo ndo wakumpashia huo mwiko? We mjomba wewe we mjomba wewe.....
 
Mjomba hebu mwache mtoto maziwa yasijekuacha kuota bure, afu ni wewe huyo ndo wakumpashia huo mwiko? We mjomba wewe we mjomba wewe.....

Kha!
Na wewe popo kama mimi kumbe?!
Halafu ujue mimi si mtu wa kucheka ki vile... lakini leo usiku huu nimecheka tena kwa sauti....
you are realy salt!
To be open... kuna kitu flani nimependa lakini si kwa tafsiri mbaya!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom