Maumivu ya mahusiano! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maumivu ya mahusiano!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Jul 23, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kwa siku za hivi karibuni, tumekuwa tukishuhudia sehemu kubwa ya mahusiano yanayo wahusisha vijana hatima yake huwa ni machozi yanayoambatana na maumivu ya majuto.

  Je, tunakuwaa hatuufahamu ukweli tunapoingia ktk mahusiano? Tatizo ni nini? Tunaweza kufanya nini tuepukane na hii hali?

  Naomba Maoni yako kuhusiana na hili tatizo!
   
 2. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Wengi wanakua wanaingia kwenye mahusiano kwa maslahi yao,wakikuona mambo safi mtu anaingia na maneno matamu,
  baby na darling kwa wingi,na wala haoni tabu kumchukua bwana na hata mdogo wake..
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Mmh, HP moyo ni msaliti sana wakati mwingine.

  Kuna saa ukweli unakuwa shubiri unaamua kujifurahisha na uongo japo kwa muda.
  Hapa mwisho wake lazima yawe machozi

  Kuna saa unapenda wakati unaona mbele kiza na unajua/hisi kabisa hakuna future.
  Kama ni mtu 'realistic' unaamua kukwepa ila ukishindwa unajisemea liwalo na liwe

  Na kumbuka, wakati mwingine kadiri unavyokaa na mtu ndivyo upendo unazidi
   
 4. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,322
  Likes Received: 2,300
  Trophy Points: 280
  1. Tumekuwa wasanii mno (tunaigiza tunachokiwaza) hatutaki kuwa realistic na kuukubali ukweli

  2. Kipato pia ni tatizo......wapenzi wanataka kupendeza (pesa), kula vizuri (pesa), simu na voucher (pesa), kutoka out (pesa).......Kwa hiyo utaona hivyo vionjo vyote vipya vilivyoingizwa kwenye mapenzi vinaenda kwa nguvu ya chapaa na kama mmojawapo hana basiii.

  3. Tuna-expect mengi sana kutoka kwa wenzi wetu kana kwamba wao ni viumbe wa ajabu sana au malaika kwa mfano: sexy (unataka perfect), uzuri (perfect) , maongezi na (perfect) n.k

  4. Kutokuwa waaminifu kwenye mahusiano....ambayo pia inaweza kuchangiwa na sababu hizo hapo juu
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Mambo safi ni nini?
  Na maslahi mazuri yanaaznia sh. ngapi?

  Basi, tena penzi linapokuwa la maslahi haliumi hata tone moja
  Wenye mafao mazuri ya kimaslahi ni wengi tena wanono tu
  Ni marketing strategy tu inahitajika, hapa huwa anashuka mtu anapanda mtu.

  But, when it's 'real' hapo ndio huwa kuna maumivu.

   
 6. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Wifi dongo hilo....
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nini kifanyike kama lengo ni maslahi? Majeruhi wa mapenzi wanaongezeka siku hadi siku na hii inatishia uaminifu katika mahusiano!
   
 8. unknown animal

  unknown animal JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tatizo unatakiwa kulijua wewe na huyo mpendwa wako coz mapenz hayana formula kwamba fulan alifanya hivi bac uige,so lazima ujipime wewe kama ni mkal wa kuhandle situations,enjoy...........
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Hata kama ilikuwa real, ulifanya maamuzi sahihi au ndio uliamua kuufumbia macho 'ukweli' sababu hukuwa tayari kuukubali? Mfano falling for a 'player' ni wazi hawezi badilika saa akija cheat unaanza kupasuka kichwa, why?

  Ukijiona uko kwenye mahusiano ambayo huwezi beba mapungufu ya mwenzio, jichunguze kwanza je 'was it real?'
  Ukicheat au sijui kuwa na kidumu sababu ya pesa, sex, n.k jiulize, was it real?

  Love conquers all -source: MwanajamiiOne

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hapo penye bold nakubaliana na wewe Kongosho lakini kuna changamoto moja kuwa kama mmoja yupo kimaslahi na mwingine ndo keshafika, aliyoko kimaslahi ndiye ambaye hawezi kuumia, lakini yule aliyejiona ameshafika ndiye anayekumbwa na mkasa wa majeruhi wa mapenzi .....


  Swali: Tunakuwa hatufahamu ukweli tunapoingia ktk mahusiano? Kuna namna ya kuepukana na hii hali? Nini cha kuzingatia tunapoanzisha mahusiano yanayoweza kutupeleka kwenye ndoa?
   
 11. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,322
  Likes Received: 2,300
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana nikasema kwenye namba moja hatutaki kuwa "realistic"......Kwamba sijidanganyi na najua huyu mtu ni player kwa hiyo kama naingia lazima niukubali 'utata" wake na nijue namna ya kukabiliana nao au kuumia nao ama niangalie future kwa uhalisia wake vilevile na si kujidanganya kwa jambo ambalo huna hakika nalo (kwa mfano atabadilika baadaye)
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Mie naaamini kabla ya kuingia kwenye mahusiano unajua kabisa
  Huyu mtu ni wa aina gani
  Kuna viashiria vidogo vidogo viiingi
  Lakini mara nyingine tunakataa kuukubali ukweli maana kwa wakati huo unakuwa mchungu kwetu
  Inabidi kujidanganya mtu unayeingia naye kwenye mahusiano na yeye 'kapeeenda' huku wazi kabisa 'conscious' au 'six sense' yako inakuambia anataka 'pesa' yako tu anataka kuingia kwenye 'sketi' yako tu

  Mbona hili liko wazi from day 1?

  Mtu anayekupanda 'genuinely' unamfahamu kabisa.

   
 13. mangulumbwisi

  mangulumbwisi Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mi nionavyo , wengi wetu tunakuwa siyo waaminifu na wakweli, kwani utakuta mmoja kati yenu anajua kabisa hapa mimi huyu na mdanganya tu nataka starehe,

  Upande wa pili mwezio anakuwa gizani kabisaaa kajiachia full anajua ndo amefika, Kusema za kweli wanaume mara nyingi huwa wanakuwa wanajua kabisa huyu binti nipo naye tu lakini sina mpango nae na hamwambiii chochote,

  wengine wapo radhi hata kumzalisha msichana then baadae anakwambia mimi sijapanga kuishi nae, HAPA TATIZO NI KUTOKUA MKWELI/KUTOKUWA MWAMINIFU
   
 14. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kama watu huingia kwenye mahusiano na mtu wangali wakitambua kuwa huyo mpenziwe ni 'player', tunaweza kusema kwa kiasi vijana wa karne hii ni wazembe au watu wasio na huruma na afya zao au maisha yao? Inazekenaje kunywa asali yenye utamu sana ambayo imewekewa sumu hali ukijua itakudhuru baadaye?

  Kwa nini tumefikia huku tofauti na wenzetu wa miaka ile ya sitini na sabini ambapo maumivu ya mapenzi yalikuwa ni ya nadra sana? Hatuwezi kufuatilia tujue wenzetu walifanyaje/waliishije? Au kwa kufanya hivyo na kuyarudia ya zamani tutaonekana tumepitwa na wakati, na hivyo kujipotezea wapenzi? loh!?
   
 15. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Aaaah eeeee kichwa kinauma eeeeeh
   
 16. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,322
  Likes Received: 2,300
  Trophy Points: 280
  Umeongea kama mama.....i wish unge.............!!
   
 17. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Yaani kama kweli mtu ungeweza kujua toka siku ya kwanza sidhani kama ungeweza kuendelea na kuwa na muuaji hata kama ni pesa ndio imekupeleka hapo. Ina maana ukishajua huyu anaweza kuniua,utadiriki kweli kuendelea nae mpaka ndoa??!!!sidhani bana.
  Tukubaliane kwamba kuna watu ni wataalamu waku pretend........
   
 18. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naona hawajionei huruma,cha muhimu kwao ni starehe kwanza! HorsePower tumefika huku sababu ya tamaa, binaadamu hawaridhiki jamani sijui kwanini, inasikitisha sanaaa......huruma inanijia zaidi kwa watoto wetu daaah sijui hali itakuaje huko mbeleni.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Yummy hapo penye bold ndipo paliponilazimisha kuandika uzi huu. Nafikiria huko mbeleni tunatengeneza taifa lililojaa majeruhi wa Mapenzi. Taifa lenye watu wenye pressure na kutokuaminiana. Taifa la watu wenye vidonda vya tumbo na frustrations nzito za mahusiano! Mwisho wa siku taifa lijalo la watoto wetu litakuwa ni ma-expert cheaters, watu waliojaa mioyo yenye usugu wa mapenzi, kutokuaminiana na kutokuwa na huruma ya mapenzi kwa wengine wala upendo wa kweli! Sijui hali itakuwaje!
   
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  cacico, kuona viashiria ni A, na kuukubali ukweli ni B

  Siamini kuwa kuna watu hawawezi kabisa kuona viashiria au kuna watu wanaweza kupretyend saaaana kiasi kwamza usiweze ona ukweli.Kinachotuumiza ni 'denial' kwa sababu ushavutiwa sana na mtu huyo.

  Jamani kila kitu huiongea, maneno, matendo, macho.Usiniambie wee huna 'six senses'? hata kama ziko five senses mtu anayekupenda kiukweli kabisa unamjua

  Cha kwanza huwa hana 'mysteries' unaweza msoma kila kitu.Ukiona uko na mtu afu kila siku kuna vitu 'dots' haziconnect afu bado useme hukujua kama ni real ama lahBasi anza fuata utabiri hata wa hali ya kewa.

  Simaanishi kuwa kuanzia mwanzo utajua mikiki mikiki yte kuwa labda atakuua au atakuwa anakupiga 2*3 kwa siku 4Lakini utajua kabisa huyu mtu chochote chaweza tokea so expect some 'Disappointments'

   
Loading...