Nimemuona rafiki yangu leo anaumwa gego la juu aisee kwa jinsi nilivyosimuliwa Ni hatari.
Halali Wala hali vizuri hata kuongea anashindwa yaani mpaka kichwa kimevimba maumivu Ni ya mwili mzima.haya meno we yaone tu hivihivi Ni noma jamaa kapelekwa nyumbani kwao mwanza amekaa miezi sita jino linamsumbua Dawa za asili zimeshindikana kashauriwa akatolewe hospital ya rufaa na asitolewe na mtalaam ambaye Hana historia nzuri kwani jino amesikia linaweza hata kusababisha kifo.
Analia Kama mtoto asee sikuwahi kutegemea Kama jino linasumbua namna hii.
Meno yalipo kuna mishipa mingi ya fahamu, hii hupelekwa maumivu ya meno kuwa makali sana. Ni muhimu kumuona mtaalamu mwenye ujuzi akupe matibabu, uvimbe ni dalili ya maambukizi kwenye jino kitu ambacho ni hatari kwa mgonjwa.