MWANASIASA HURU
Senior Member
- Oct 4, 2012
- 180
- 245
Mimi ni dada wa miaka 38 nina watoto 3 kwenye ndoa nina miaka 13, mume wangu ana umri miaka 52.
Mwaka huu mwanzoni nilifuma sms kwenye simu ya mume wangu akijibu sms ya mchepuko.
Ni hivi mchepuko alimwandikia kwamba ana mimba yake, yeye akajibu kwamba sio mimba yake siku ambayo walikutana yeye akumaliza (sijui alikuwa na mana gani). Hiki kitu kimeniumiza sana moyo.
Nilikuwa nina uhakika kwamba anachepuka lakini nikajipa moyo anatumia condom. Baada ya kufuma hiyo sms ndio nikaamini kwamba ana kwenda bila kinga. Hiki kitu kinaniumiza sana moyo sijui nifanye nini ili nisahau, ukizingatia magojwa yalivyo mengi! Inatisha kwelikweli.
Naomba ushauri nitumia njia gani ili nikifute kwenye mawazo yangu.
Mwathirika.
Usijali shem akeKwahiyo unaponiona naongea vitu ambavyo vinakukwaza tusameheane shem
Usijali shem ake
Aah nilikuwa hoi tangu ile jana usiku, ila namshukuru Mungu Naendelea vizuri nownashukuru kwa hilo shem, vp umzima lakini
Aah nilikuwa hoi tangu ile jana usiku, ila namshukuru Mungu Naendelea vizuri now
tatizo nini tena mpendwa wangu?
Hahahahhahahahah acha nicheke kwanza
Ni hivi niliolewa 2010 na mwanaume niliyempenda kwa moyo wote.
Ndoa ikawa tamuuuuu sanaaa tamu kweli (nilikuwa nawaambia rafiki zangu mume wangu hata aje mwanamke ameumbwa vipi hajavaa nguo hata moja hatamtamani, nilimuamini sana na before marriage tulishakaa kama miaka mitano hivi so nilijiaminisha).
Basi bwana mambo yakabadilika weeee hadi ikafika muda mume nyumbani harudi hata wiki ila kazini yupo muda wote. Iliendelea hivyo hadi tukatengana (nakata story)
Basi baadae tukasuluhishwa pale tukarudiana (simu pia ilichangia hadi tukatengana), basi maisha yakaendelea ila ule upendo ukawa umepungua kwa upande wangu, mume akajitahidi sana kunirudisha kawaida akawa mtulivu kweli kweli taratibu (na wanawake tulivyo) nikajikuta narudisha upendo vile vile japo kuna muda nakuwa na wasi wasi.
(Tuokoe muda), kuna siku nikawa naumwa nimelala nimeshindwa hata kupika nikampigia simu kumwambia, akarudi kama saa 3 usiku kakuta nimelala, tumesalimiana kaniuliza unaendeleaje na vitu kama hivyo, baadae pale kitandani akakaa ila hatazamani na mimi akawa busy na simu hadi saa tano (me nilipitiwa na kausingizi ka homa) nashtuka nakuta mtu yupo busy bado, akaniomba maji ya kuoga ki ukweli sikuwa naweza hivyo nikamuomba ajiandalie alichukia kwa sababu nilimzoesha ni lazima ni muandalie maji na lazima tuoge wote hata kama nimeshaoga ila akaanda akaenda kuoga.
Mimi nikawa naitamani sana ile simu, nikaishika yeye yupo bafuni, yaani kufungua tu kwenye sms nakutana na chatting moja mataa (baby, honey swty darling majina yote yale mazuri mazuri unayoyajua) ila kubwa zaidi ni sms za pitia ofisini nikuone mwanaume ndo anamtumia mwanamke nimekumiss nahitaji kufanya mapenzi na ww, your so sweet na vitu kama hivyo mwisho kabisa wakamalizana na hii, "kesho saa tisa basi tukutane kule kule wewe tangulia ukifika niambie" (nilivyofika hapa nilipona nikawa mzima kabisaa).
Basi mume katoka kuoga nikamuuliza, jibu lake sasa hahahahahahahah "alikwambia ushike simu yangu nani umeyataka" (nililia sana zaidi ya sana haielezeki kumbuka me nilikuwa naumwa nipo kitandani yeye ndo anafanya hayo). Niliumia sana.
Nikajitahidi nijidai mkali nikaishia kupewa maneno ya kuumiza zaidi.
Kweli Mungu yupo. Nilijikuta nawaza niamke nisali tu, basi hivyo hivyo huku nalia nikaingia kuoga nikapata udhu vizuri nikaswali (me ni muslim), niliswali huku machozi yanatoka, niliamua kumlilia Mungu nilitumia muda mrefu sana hadi pale moyo wangu ulivyopoa.
Nilivyoridhika nikapanda kitandani yeye alivyoona ninaswali akalala, basi nikajiandaa kulala ila kabla nikamuamsha nikamshika mkono nikamwambia "nisamehe mume wangu", akaniuliza kwanini nikamjibu "kwa sababu nimeshika simu yako nisingeshika haya yote yasingetokea, nisamehe sana, nakupenda mume wangu".
Mh machozi yakamtoka akaniambia nisamehe pia mke wangu, nikamjibu nimekusamehe na moyo wangu mweupe, sina kinyongo na wewe, akaniambia nakupenda mke wangu hawa nawapotezea muda tu ndio maana nimekuoa wewe, nikamjibu najua mume wangu na nakuahidi sitashika simu yako tena. Baada ya HAPO SIKUSHIKA SIMU YAKE TENA NA SITASHIKA SIMU YA MWANAUME TENA
Ila baadae tuliachana. So kushika simu ya mtu ni kujitafutia matatizo, mwanaume ukigundua hajatulia unaamua tu au kumvumilia (ndo ile kwa shida na raha) au kuachana nae ila kushika simu unajiumiza na ukimuuliza anaweza kukujibu ukahisi dunia nzima inakuona unavyojibiwa
kwenye hii post kuna sehemu nimecheka hadi machoz ila pole aiseee. hawa viumbe wanadamu both ke na me ni shidaaaaa
Hahahahah wapi hapo?
pale ulipojitahid kuwa mkali hahahahah
hiv nikuulize maana ishapita muda; si kuna wakat ukikumbuka huwa unacheka??
maana mie michoz haikukauka mapema
Malaria haikubaliki teh
Teh teh, kuna muda nacheka saaanaaaa
Hata usijali shemNingejua mapema ningekuletea Matunda mpendwa
cheka tu LUV maana hakuna namna. yaan kila nikikumbuka nacheka. nahis ka nakuon Vile ulivyojiandaa gafla ukanyweaaa.
mbavu zangu mieeee
Hata usijali shem
Nilimaanisha kuwa nimekutaarifu late kama naumwa, so usijali. Nashukuru sana shemhuwezi kuacha kujali kwa mtu muhimu kama wewe, wewe ni muhimu kwahiyo kujali ni jukumu langu
huwezi kuacha kujali kwa mtu muhimu kama wewe, wewe ni muhimu kwahiyo kujali ni jukumu langu
Hata usijali shem
Hahaha mama Man U mgonjwa Shurti abembelezwe. Huna ratiba ya BBC leo?Nawachabo tu mnavyobembelezana.....mkalale sasa eboooo!!!......lol
Hahaha mama Man U mgonjwa Shurti abembelezwe. Huna ratiba ya BBC leo?
Hahaha ukute brod darlin hayupo, maana anajua kuazimisha mwiko wake MmhHahahAha yaani nimechokaaa mpka hamu nayo sinaaa.....labda asubuhi nipambazuke na Bwana....lol