Maumivu makali

Hvi haya madingi huku makazini tunayaona yana busara,kumbe behind the scene ndio yanafanya upuuzi hvo?
 
Ushauri mzuri sana ila umesahau kumwambia kuwa kazi ya mchungaji ni kuhakikisha hakuna hata kondoo mmoja anayepotea. Ajitahidi sana kumwokoa huyo kondoo (mume) hata kama mambo mengine yanasababishwa na uzembe wake!

Naam, umenena vyema mkuu. Nashukuru kwa kunikumbusha hilo.
 
Mmh hongera na pole. Aisee jf ina wife materials khaa, ngoja niendelee na course. Ila yote tu mipango ya Mungu mpendwa, likuepukalo lina kheri nawe

Me nina principle moja, hakuna privacy linapokuja suala la simu. Kama tutaweka password ni sawa, but kila mtu atajua password ya mwenzie. Sina haja ya kuvizia uende chooni ndo nishike simu yako nope, naishika tu muda wowote nikijisikia. Sio kwamba hayanikutagi, yashanikuta mnooo, ila Nipo tuuu.

Umeongelea kwenye ndoa, me nakupa mfano wangu kwenye urafiki wangu. Nilikuwaga na bf wangu mmoja, Kila mtu yupo free na simu ya mwenzie. Lakini ukiwa na hamu ya tumaumivu shika simu yake. Sikuwahi kukuta texts chafu but unakuta zile convo labda anamsarandia binti huko au zingine zile za kupewa taarifa, Ntalala kwa fulani au kuna jina likipiga simu kama nipo anamute etc. Tulikuwa tunagombana mwee, na ndugu yako Najua kulianzisha eeeeh. Aah baadaye nikamwambia tu abadili password zake zote Sitaki tena kuwa na access na mawasiliano yake. Basi tukaendelea kwa raha zetyuuuu.

kufupisha tu story, ni simu ile ile ndo ilivunja trust yangu mazima. Cha kufurahisha zaidi kosa likageuziwa kwangu, sio kwa kile kichambo nilichompa. Baadaye nikajitahidi kupotezea tu tuendelee but I couldn't trust him again na nililose upendo na interest kwake, mwishoni ikabaki historia.

Kwa akili zangu hizi nusu na robo, nikajifunza tu naweza nikaignore kushika simu ya mtu, but hiyo sio guarantee ya kuwa sitoumia kama anacheat kweli. Unapostpone tu tarehe za maumivu, ila maumivu yapo pale pale. Ni bora nigundue leo mapema kabla madhara hayajawa makubwa. Coz ntachukulia poa leo, nakuja kushangaa watoto wamefata ada ya chuo kwa baba yao teh au ashaanza kutumia na dozi mwenzangu. So simu ntaendelea tu kushika hadi kwenye ndoa, yakinikuta ntajua huko huko ndoani. Tena bora awe free na simu yake, akiwa anaificha ficha ndo kabisaaa
 
me bado kidogo sana babu
Na ww kwa umri huo umeshamaliza vibarua vyako vyote au unamsumbua bb dc
 
huyo mzee nuksi ''eti mi siku ile sikumaliza..''

pole sana dada... kaza moyo check afya..
 
Ilikuwaje huyu mumeo akuachie usome message kama hizo kwenye simu yake? Haweki password? Ndio madhara yake hayo.mweleze tu muongee labda moyo wako utatulia.
Pole sana shemeji.

Kwa iyo password zinawekwa ili kusudi mmoja asisome yaliyomo kwenye simu.Kiukweli mimi walau mwezi haukatiki sijashika simu ya mme wangu, uzuri wenyewe sina presha kwa iyo nashika tu.
 
chanzo cha wewe kuumia ni kujua kusoma, laiti ungekuwa haujui kusoma yote hayo usingeyafahamu!!!!!!!
 

Endapo na wewe utachepuka na kuzalishwa nje kama alivyofanya mmeo
hapo ndipo utapona hicho kinachokusumbua.
 
Kwangu siyo marufuku ila sitaki na huwasichokonoi simu ya Bibi...

Hii ni kwa usalama wangu....wakati mwingine unaweza kujifia kumbe sms zilikuwa utani..

Pensheni yangu bado ni tamu sana aisee!

Hahaa kweli aisee ila mimi ya mjukuu wako nachokonoa ili nisije nikauvaa mkenge
 
Kwa iyo password zinawekwa ili kusudi mmoja asisome yaliyomo kwenye simu.Kiukweli mimi walau mwezi haukatiki sijashika simu ya mme wangu, uzuri wenyewe sina presha kwa iyo nashika tu.

Kushika simu si tatizo.tatizo yaliyomo.alitakiwa kuhakikisha inbox nyeupe kama theluji unaacha vimeseji tuwili tutatu vya wandugu vya kuzugia. Aah huyo mume wake kachemka sana.unajuwa dadangu hizi ndoa bila kuwa msiri kidogo mnaachana au unamkwaza mwenzi wako.
 
Hee kwahyo unaumia kwa kuwa hatumii cobdom, akiitumia cheating inakuwa ok kwako? MAKUBWA

mwenzako she is just being realistic bwana...wewe wataka kujidanganya kuwa mwanaume wako peke yako
 


dah pole sana...yaani kaa ukijua kabisa kuwa mume/mke akitoka je ya ndoa atagegedana kavu kavu tuu. sasa ndio maana kabla ya kuingia kwenye ndoa inabidi utambue kuwa umesha sign death warrant
 
Siku Zote Tambua kuwa Mwanaume Anapatikana Popote lakini Uhai haupatkani Hata Kwa Kiasi gani Cha Pesa... Kutokujali kwa mumeo hasa anapokuwa mbali na wewe inaonyesha ni Rahisi Kukuletea Magonjwa Ya Zinaa likiwemo la Ukimwi. Unadhani Ukipata Ukimwi nani Atakuwa Ameharibu Maisha Yake?

Machozi Hayawezi kukuondolea Hali hii wala hayataitibu Tabia Ya Mumeo bali Machozi Yako Yanaweza kuwa ni Silaha Ya Mwisho kukuua.

Wafikirie Watoto Wako Kisha Jifikirie Wewe, Waonee huruma Wao na Jionee Huruma Wewe. Kulia na kulalama Sio Suluhisho la Hilo tatizo...

Chakufanya Muweke Chini na Mueleze Ukweli Juu Ya kile Ulichokikuta kwenye simu. Usimuogope kwa kuwa ni Mumeo na usimuogope kwa kuwa Unaona Mtagombana unachotakiwa ni Kuipigania ndoa Yako na watoto wako..

Ukiona Hasikii muitie Wazee Au Viongozi wa DINI na iwapo Itashindikana Unaweza kutoa Msimamo wako katika suala hilo.
 

katika mahusiano yote niliyopitia nilikuwa nikiponzwa na Upole na Ile Hali ya kumuamini mtu kupita Uwezo. Kipindi nipo CBE niliingia katika Mahusiano na Binti mmoja ambaye nilikuwa nikimpenda na Kumthamini kuliko Hata Mama Yangu Mzazi..

Kila alichokuwa Akinieleza nilikuwa nikikubali na kuamini.. Nilimuonyesha kila aina Ya mapenzi, nilimuonyesha ni Jinsi gani Mwanamke Anatakiwa kupendwa... Alikuwa Huru kushika na Kuangalia Chochote.. Iwe Simu; lap top na Vingine vingine kibao. Na hata Yeye alinipa Uhuru Huo kitu Ambacho kiliongeza Upendo Wangu kwake.

Kumbe nilikuwa nikifanywa Mjinga, Mpumbavu na Limbukeni.. Kumbe wakati nikiamini nipo mimi kama mimi kumbe mwenzangu Alikuwa na Mtu wa Pembeni. Na ili mimi nisigundue Akanunua Simu ambayo Ilikuwa Akiificha na kuchati na watu wake akiwa kwao ama mbali na Wewe.

MUNGU hakutaka kumficha mnafiki, Mungu hakutaka niendelee kudanganywa. Ilikuwa Siku ambayo nilikuwa katika Maandalizi Ya Semister nikiwa Nimejiinamia Simu Yangu Ikaingia Sms Upande Wa WhatsAp... Sijui ni kitu gani kilinipata lakini Nilijikuta nikiogopa kuifungua Ile Sms.. Wakati Nikiendelea kujifikiria zikaanza kuingia sms Mfululizo nikaona Bora Nizisome....

Nikaifungua Sms Ya kwanza Ambayo Ilionekana kutumwa na Namba Ngeni.... Hapo nikakutana na Picha Ya mwanamke niliyempenda Akiwa Uchi tena Huku Amekumbatiwa kwa nyuma.. Sijawahi kuumia, kulia kama Nilivyoumia Siku Hiyo..

Bahati Mbaya Nikaharibu Masomo Yangu.. Ibrah Nikadisco na Hata niliporudia mwaka bado nikaangukia pua.. Ingawa ni Mtu Mwenye jina kwasasa Lakini Namchukia mpaka naingia kaburini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…