Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,917
- 30,259
MAULID YA SHARIFF IDARUS STAND YA MBOYA MOSHI USIKU HUU
Hivi punde nimepokea picha za kupendeza kutoka za Maulid ya Shariff Idarus kutoka kwa rafiki yangu.
Maulid haya yanayosomwa Moshi Stand ya Mboya na huyu rafiki yangu kutoka Moshi.
Yeye katokea Mombasa leo kupitia mpaka wa Holili akiongozana na nduguye.
Nduguye kakaribishwa kwa kupewa kusoma Mlango wa Pili.
Maashaallah.
Taarifa hizi zimenifurahisha kupita kiasi nikataza ma nyuma wakati naandika kitabu,''Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama.''
Ibrahim Kirama ndiye aliyeingiza Uislam Kilimanjaro katika miaka ya
1930.
Katika kitabu hiki kinachoeleza maisha yake kilichochapwa mwaka wa 2020 kuna sura nimeeleza Maulid ilivyoingia Uchaggani sasa zaidi ya miaka 100 iliyopita.
Wakati natafiti kutafuta habari zaidi ya maulid nikitumia Nyaraza za Mzee Rajabu Kirama zenye umri wa miaka 100 nilivutiwa na Maulid moja iliyosomwa Moshi Mjini mwaka wa 1952 ambayo ilihudhuriwa na Chief Thomas Marealle ambae mwaka huo alichaguliwakuwa Mangi Mkuu.
Katika Maulid haya alikuwapo pia Mangi wa Machame, Chief Abdiel Shangali.
Lakini kabla ya kufika katika hali ya kuwa Maulid inasomwa Uchaggani ilibidi nitafute historia ya walimu wa mwazno kusomesha Uislam Kilimanjaro sehemu ijulikanayo kama Machame Nkuu.
Nakuwekea kipande kifupi hapo chini:
Sheikh Abdallah Minhaj asili ya wazee wake ilikuwa Ngazija ingaawa yeye na walimu wenzake watatu walitokea Zanzibar na wakaletwa Kilimanjaro na Upare na Sheikh Hassan bin Ameir kwa kuombwa na Mzee Rajabu Kirama kuja kusomesha dini.
Haukupita muda mrefu akisomesha matunda yake yakaanza kuonekana pale Nkuu na vijiji vya jirani kwa watoto kuanza kusoma Qura’an vyema na kufunzwa vitabu vingine vidogo vya kufundisha akida nyingine za Kiislam.
Vijiji vyote vya jirani vya Lyamungo, Masama, Mudio, Kibosho, Mkoanju na Uswaa vikaleta wanafunzi kuja kusoma Nkuu chuo cha Sheikh Abdallah Minhaj.
Haya yalikuwa maendeleo makubwa sana ukitazama nyuma na kuangalia wapi Waislam wa Machame walikotokea.
Wanafunzi wa Muslim School, Machame Nkuu wakawa kila mwaka wanashiriki katika Maulidi ya Mfungo Sita Moshi mjini wao pamoja na walimu wao.
Pamoja na haya pakawa panasomwa pia kisa cha Miraj kila mwaka.''
Maulid haya yamenikumbusha hiyo maulid ya mwaka 1952 miaka 70 iliyopita, Maulid ambayo Mangi Mkuu Thomaa Marealle na Chief Abdiel Shangali walihudhuria.
Leo ndugu zetu wanasheherekea mazazi ya Mtume SAW hapo Moshi Mjini tuchukue fursa hii kuwaombea dua wale wote waliosimama kueneza Uislam sehemu ambazo haukupata kuwapo kabisa na leo upo na unashamiri.
PICHA: Kitabu na picha ya Mzee Rajabu Ibrahim Kirama, Sheikh Abdallah Minhaj, Mangi Mkuu Thomas Marealle, Chief Abdiel Shangali wa Machame na Maulid ya Sharif Idarus, Moshi Mjini.