GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Najua fika kuwa nyie ndiyo Viongozi wa Sports Departments za vyombo vya habari mnavyovifanyia kazi ambapo Maulid Kitenge yupo E fm wakati Shafii Dauda yupo Clouds fm na tv huku Amri Masare akiwa ITV na Radio One.
Nyie Watangazaji tajwa hapo juu tumeshajua kuwa mpo vizuri na mnafanya pia vyema katika tasnia nzima ya Utangazaji ila naomba tu kuwaulizeni hili swali. HIVI NI LAZIMA KILA ZIARA YA KIKAZI HASA ZA KIMICHEZO ZA NJE YA NCHI KILA MARA MUENDE NYIE TU?
Kwa mfano Kitenge ziara nyingine ukimuachia Ibrahim Masoud au Shafii ukimuachia Alex Luambano au Amri Masare ukimuachia Hemed Kivuyo mtapungukiwa na nini? Kwanini mnakuwa WABINAFSI hivi na hamtaki kuwapa nafasi na Watangazaji wenzenu pia na wao watoe kidogo " matongotongo? " Kwani mnadhani na wao pia hizo allowances hawazitaki ili nao pia waendeleze maisha yao kama yenu yalivyokuwa mazuri? Hii roho ya choyo na ubinafsi mmeitoa wapi?
Basi kupitia UZI huu nawaombeni mjisikie aibu na vibaya halafu ziara zijazo za kimichezo hasa za nje ya nchi Kitenge, Shafii na Masare mbaki mle vumbi hapa Dar na wenzenu pia wasafiri na hii itawajengea sana uhusiano mwema baina yenu kuliko kama ilivyo sasa ambapo mnachekeana tu usoni lakini tukikutana humu mitaani mnasemana na kupigana mno majungu.
Hali nasikia imepelekea sasa baadhi ya Watangazaji wenzenu kuwaendea kwa Waganga kuwaroga ili mpotee hali ambayo ilimtisha Mtangazaji mmoja Mkongwe na maarufu wa " mapacha na miss tanzania media " kukimbia kwenda zake redio ya kimataifa ya Mkoloni wetu wa kwanza kabla ya Muingereza yenye idhaa yake ya Kiswahili mara baada siku moja kupigwa " kipapai " na mwenzie hali iliyopelekea kwa siku takriban tatu ( 3 ) kila akiwasha FEDA sauti yake haitoki lakini akiizima tu inatoka na hali hii ilimtokea kwa hizo siku na akaona isiwe taabu akaamua " kujiongeza " na kuhama na sasa anakula zake tu kipupwe kwa Mama Angel Merkel.
Ni vyema tu Wamiliki wa hivi vyombo vya habari wakalifanyia kazi hili suala vinginevyo kwa jinsi sasa Watangazaji wanavyorogana kwa kuoneana wivu hasa baada ya wao kugundua kuwa nyie Wamiliki mnawapenda sana hao wenzao tajwa hapo juu ipo siku mtakuta mtu amemeza kipaza sauti studioni halafu kafariki dunia au wakapofuana ili mwenzao asisome script aliyoiandaa kwa kipindi chake.
Naomba kuwasilisha............