Maudhui ya Kitanzania kwenye tovuti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maudhui ya Kitanzania kwenye tovuti

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Aug 26, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  ASILIMIA kubwa ya kile kinachopatikana katika intaneti kimebuniwa na kuandaliwa na watu binafsi, kampuni na serikali za nchi zilizoendelea. Katika hali kama hii nguvu za utandawazi zinaelemea nchi masikini na kuhatarisha uhuru wao wa kiutamaduni na kiuchumi kwa kiasi kikubwa zaidi.
  Mtandao usipoangaliwa kama ilivyo kwa lugha za kigeni na athari za kasumba zake kuwalemeza wale waliotawaliwa na nchi kongwe duniani ndivyo ilivyo pia kwa TEKNOHAMA. Kama tusipoangalia tutajikuta sisi ni watumiaji na kazi ya kubadili maudhui katika tovuti sio kwa kiasi fulani ni kazi ya mtu mmoja mmoja lakini kazi hiyo itakuwa ngumu kama serikali isipokuwa na mchango wake na isipotoa msaada wake kwa watu na makampuni binafsi.
  Kitu cha kwanza kinachohitajika kufanywa na serikali ni yenyewe kuchangamkia suala la kuwa na maudhui za Kitanzania kwenye tovuti. Kweli ipo tovuti ya taifa lakini inavyoonekana hivi sasa ni kuwa wizara zimeweka oroddha tu ya vitu fualni lakini hakuna maelezo na habari muhimu za kumsaidia na kufanya kazi au majukumu ya Watanzania na wageni kuwa marahisi zaidi.
  Je, kwanini kila wizara isiwe na tovuti yake yenye maelezo yenye manufaa kwa mtuamiaji ndani au nje ya nchi. Kwa namna hii shughuli za maulizo/malezo, kuomba visa au vibali vya serikali, kujua fursa za uwekezaji, biashara na Tanzania na kadhalika vitakuwa rahisi kuliko ilivyo sasa.
  Hivi sasa wawekezaji huko nje wanajua machache sana kuhusu fursa za uwekezejai zilizopo katika mikoa na wilaya mbalimbali Tanzania, je, upo uwezekano wa kila mkoa na kila wilaya kuwa na tovuti yake yenye maelezo ya kina juu ya vitu hivyo.
  Katika miaka hii ya sasa tovuti hiyo itakuwa na uwezo wa kuwa na picha zinazofanana na ukweli; maelezo kwa sauti; ramani ya mkoa au wilaya na njia za kuwasiliana kupitia mtandao ili kurahisisha kazi kwa mwekezaji mtarajiwa.
  Kuna majumba ya makumbusho machache tu nchini kuweza kuhifadhi kwa dhati mila na utamaduni wa Mtanzania. Ujio wa intaneti unafanya iwe rahisi kwa kila kabila Tanzania kuwa na makumbusho yake kwenye intaneti. Tovuti kama hiyo inaweza kuwa na nyumba za asili; vifaa mbalimbali vilivyotumika na makabila husika; mitindo ya nguo, mavazi, nywele ya wakati huo; maelezo muhimu kuhusu maisha-uzazi, ndoa, vifo, elimu na mahusiano ya kijamii na kadhalika. Bila kusahau historia ya kila kabila.
  Kinachotakiwa hapa ni kwa kila kabila kuwatumia vijana wake na kuwekeza kitu kidogo ili utamaduni ikiwa ni pamoja na lugha ya kila kabila visifutike kabisa kutokana na kasi ya usambaratishaji kutokana na utandawazi. Baadhi ya vyombo vya habari hivi sasa vinautajirisha mchango wa Tanzania kwenye intaneti kila siku lakini bado vingi tu havijaona ndani katika suala hili la kutoa mchango wa kile Tanzania inachozalisha kihabari na kiutamaduni kwenye mtandao ili watu wengine duniani nao wafaidi.
  Hata kwa wale walio na tovuti bado kuna mambo mengi tu yanayopaswa kufanyika ili tovuti ziwe na vitu vingi na mbalimbali vinavyomfaa zaidi Mtanzania na mtu wa nje. Kampuni nyingi bado zimelala kuhusiana na kuwepo kwao kwenye mtandao. Miaka imebadilika kwa kasi sana hivi sasa kiasi kwamba kama hauonekani kwenye intaneti basi ni sawa na haupo.
  Biashara inakuwa ngumu sana na nchi za nje kama usipoonyesha kuwa una e-mail na tovuti yake mwenyewe. E-mail za watu kama yahoo au hotmail sio rahisi kukubalika kibiashara. Ili biashara na uchumi Tanzania ukue lazima makampuni mengi zaidi yawe na tovuti na hivyo kujulikana kuwa zipo lakini pia kutoa mchango wao katika kuneemesha maudhui za Kitanzania zinazopatikana katika mtandao
   
Loading...