Kikubwa, kabla huaoa piga goti vya kutosha na ukishaoa piga goti pia vya kutosha ... heshima na adabu ya ndoa ni kitu cha pande mbili, kabla hujaheshimiwa na mke kukutii cha kwanza jiheshimu na uwe mtii, jinsi ulivyoandika mada yako kwanza inaonesha hujaoa and like MKE ni kitu tu umekileta nyumbani kwa ajili ya matumizi yako.
Kumbuka, unapopiga goti kwa ajili ya kumuomba MUNGU mke wa kufanana nawe, mke naye at the same time amekuwa akimuomba MUNGU mume wa kumfaa na kufanana naye so si lazima yeye tu ndo afuate tabia zako bali wewe pia unatakiwa ufuate tabia zake. Usisahau kanuni hii : Stranger+Rafiki+Uhusiano+Uchumba+Ndoa=Mke so kama huko kote ulipita mwisho wa siku ukaamua kujitwisha then hilo lako ... wanaume tupunguze kulalamika na tu deal na changamoto zetu za kwenye ndoa.
Mke ni binadamu kama binadamu wengine, tofauti ni jinsia tu, so kama wewe unakosea yeye pia anayo nafasi ya kufanya makosa tena kumbuka wao wana disadvantage in mood swing due to the monthly hormonal changes so weka room kwa ajili ya hiyo kitu. Kikubwa, kama couples msisahau kurekebishana kwa heshima na upendo na kusamehe, coz kwangu asiyesamehe ndiye anayepata hasara zaidi kuliko hata yule asiyesamehewa.