Mauaji ya visasi

Ukijipa muda utagundua kuwa mtu anaekukosea kwa makusudi na bila kujali hisia zako akiwa na dhamira mbaya huwa anaishia pabaya pia. Hakuna mwanadamu mwenye jeuri kuliko nguvu za ulimwengu ambazo zinasimamiwa na MUNGU.

So ni vema kujipa muda, mtu amekufanyia ubaya kwa kusudi then kubali yaishe kisasi muachie MUNGU. Unaweza dhania kumkata na panga au kumchoma kisu itakuwa ni adhabu kali kwake kumbe wala ile sio kitu ila mkabidhi kwa aliyemuumba atawajibishwa huko.

Aiseeee maisha yanapoanza kumnyoosha mtu aliyekukosea na kukuumiza kiasi kwamba unakaa chini unajiuliza hivi MUNGU anaona ukorofi unaofanyiwa ama la? Kazi ya kunyooshwa ikianza utatamani kumpigia MUNGU magoti amuonee huruma. Wewe kaa kimya mwache ajifanye mjanja. Mkalie mbali na kata nae mazoea na mawasiliano basi. Dunia ikianza kumfunza mtu wa hivyo aiseee hakuna wa kuamulia. Maana ukishika panga ukataka kumkata watu wanaweza ingilia akatetewa, au ukisema umtumie wajuba wamdhuru still anaweza escape au ukajagundulika msala ukakurudia, au ukamwekea figisu watu wanaokuheshimu wakakusihi umsamehe. Ila Maisha sasa yakianza kumnyoosha mtajikuta ni ninyi wawili tu ndio mkitazamana mnajua kuwa sasa muda wa malipo umefika na nani analipia hesabu yake ya madhambi aliyomkosea mwenzake.

Hii kitu hata katika mahusiano ipo sana. Mwanaume au mwanamke anamuacha mwenzake kipindi ambacho hakukuwa na sababu yoyote ya msingi na kulikuwa na utulivu tu au anamfanyia mwenzake matukio ya kuvunja moyo na kuumiza hisia kwa makusudi kabisa then anategemea mwenzake ataelewa tu na kupuuzia maisha yaendelee. Watu wa hivi huko wanakokwenda MUNGU huwa anawapa wanachotaka ila anawanyima wanachostahili sababu unachostahili ndicho kitakupa furaha ila unachotaka kitakufanya ujiskie vizuri kwa muda tu then baadae balaa linaanza.


S
 
Mzee akitukanwa sana kwakweli... Ilihitaji uvumilivu wa kiwango cha juu mno kutofanya alichofanya mzee
Ila me nadhani miaka hiyo hakukuwa na mawakili wazuri, huyu mzee amekosea sana kwa namna huyo marehemu RC alivyomkosea heshima eneo lake. Huwezi kwenda eneo la mtu na kuanza kumtusi mbele ya familia yake hata mimi ningemzabua makofi.

Kimsingi hapo huyo mzee alitakiwa kupewa mvua ya miaka kadhaa kama sio maisha. Ila kumnyonga ni kumtendea dhambi kubwa sana huko anapokwenda roho yake imefunga kwa huzuni anaonekana ni mtu mbaya kwa kosa la kusababishiwa. Kuna muda hawa viongozi au watu fulani wenye mamlaka huwa wanatafuta kuadhibiwa kwa makusudi.
 
Uko sahihi sana, hivi ndugu hawawezi kuifufua hii kesi na kukata rufaa?
 
Webale sana sana 🙏🙏🙏👍👍
 
Imetusikitisha sana ni jirani yangu kiboshoroad apa.inatia hasira sana
 
Rip Prof. Chachange S. Chachange; Makuwadi wa soko huria
 
Mamandenyi kaingizwa Chaka vibaya Sana na yey kaenda kichwa kichwa Google kitu gani yaani kuamini kila kitu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu sijona nyumba ya kleru

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
sio kweli ukiua bila kutumia akili ndio lazima ukamatwe tu...lakini wapo wauaji ambao wanaua kwa kupanga mauaji hao bwana hawakamatwi...ng'oooo
 
Kaini kumuua mdogo wake, kisa kikuu siyo sadaka but ni mwanamke aliyepaswa kuolewa na mdogo wake


Kaini siyo mtoto wa Adam ?

Visa vya mauaji ni vingi na miaka hii vimezidi

Just go ...
Aise! Kuna Bible version ya shetani ishatoka ama?
 
Issue sio kutokuwa na mawakili,bali ni mfumo wa katiba iliyopo,ulioupa mhimili mmoja madaraka zaidi( deep state)
Hivi hujui kuwa Rais wa wakati huo aliwaita majaji wote na kuwapa maelekezo ya kufanya dhidi ya kesi zote dhidi ya serikali kuhusu operation vijiji? Na ilikuwa Mwamwindi lazima anyongwe? Kiasi Cha jaji mmoja kujiuzulu,kwa kutotaka kuinajisi taaluma yake?
Mimi hushangaa kwa baadhi ya watu kudai magufuli alikuwa dikteta hivi wangekuwepo kipindi Cha awamu ya Kwanza wangesemaje?
 
Uko sahihi sana, hivi ndugu hawawezi kuifufua hii kesi na kukata rufaa?
Ukate rufaa miaka hamsini baada ya mtu kunyongwa? Ili iweje? Ingekuwa wanasiasa Kama sugu na lema ambao walifungwa kwa maelekezo kutoka juu Kama ilivyokuwa kwa Mwamwindi pia aliyehukumiwa kunyongwa pia kwa maelekezo ya Rais wa wakati huo na kusaini hati ya kunyongwa harakaharaka ingekuwa sawa,ukate rufaa ili mtu afufuliwe au?
 
Hilo ni kosa la kuua bila kukusudia(manslaughter) baada ya mtu kuwa provoked lakini kwa maelekezo kutoka juu likawa kosa la kuua kwa kukusudia ili kuufavor utawala wa wakati huo
 
Hapana familia ipate fidia ya haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…