Mauaji ya Tanga

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Wakati mauaji ya watu wanane waliochinjwa usiku wa kuamkia juzi mkoani Tanga yakizua maswali lukuki na kuzidisha hofu, imebainika kuwa wauaji waliwachinja wote kuanzia sehemu ya chini ya kisogo.

Watu hao waliuawa kwa kuchinjwa katika kitongoji cha Mabatini, Kata ya Mzimama, Tanga.

Tukio hilo lilifanywa nje ya nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho, ikiwa ni mwendelezo wa mauaji ya uchinjaji yaliyoikumba nchi tangu mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Mauaji hayo yametokea wakati mkoa wa Tanga ukizidi kukumbwa na matukio yanayohisiwa kuwa ni ya kigaidi tangu polisi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walipopambana na watu wasiojulikana kwenye mapango ya Amboni Januari 26 mwaka jana.

Chanzo: Mwananchi
 
Habari haiendani na kichwa cha habari yenyewe...haielezi hayo mazito yenyewe
 
Kwangu mimi hayo ni mazito sana, kumchinja mwanadamu mwenzako kama kuku, sasa polisi tunapoomba vibali vya kununua Silaha au kumiliki Silaha mtoe mapema, ona sasa hapo angekuwepo mmoja tu mwenye bastola sasa hivi ingekuwa habari tofauti
 
China raia hawana silaha na haya hayatokei!

Cha maana ni kupiga marufuku kumiliki silaha..ni Majeshi TU.
 
RPC na RC wa Tanga wafungwe maana wananchi waliripoti na Jamaa wakajitokeza kwenye media na kukanusha akiwemo pia Advero Msemaji wa Jeshi la Polisi aliyesema kuwa nchi iko salama.
Kweli?
 
China raia hawana silaha na haya hayatokei!

Cha maana ni kupiga marufuku kumiliki silaha..ni Majeshi TU.
Jamaa umeandika ugoro. Kwani silaha iliyotumika hapo kuwachinja watu ni silaha gani? Na matumizi na upatikanaji wake ukoje?
 
Tanga kunani? Mbona mauaji yamekithiri hivi!! Au ndo hili Bomba la mafuta?nawaza tu
 
Back
Top Bottom