Mvumbo
JF-Expert Member
- Aug 20, 2015
- 3,485
- 12,108
Takriban mwaka mmoja uliopita kulizuka taharuki kutokana na kuuwawa polisi wetu iwe katika vituo, barabarani au hata katika lindo, pia kukaambatana na matukio ya kigaidi/kijambazi Amboni Tanga, Mwanza, Morogoro na hata maeneo kadhaa ya Dar, Pwani na kwengineko.
Katika hali ambayo haikutarajiwa kukaenea video ya mtu aliyevaa nguo nyeusi na kuziba macho yake akijigamba kwa lugha ya kiswahili kuwa wao ndiyo wanaouwa polisi na kutuma salaam kwa mkuu wa polisi kuwa kazi hiyo itaendelea kwani wanakusanya silaha za kutosha.
Hatukuipa uzito video ile lakini hadi sasa ni muda umepita na alichokisema mtu yule kinazidi kuendelea kama alivyoahidi, najua jeshi letu la polisi linafanya kazi kubwa na nzito kuhakikisha usalama wetu hivyo nawatakia kila la kheri katika mtihani huu na sisi raia tupo nyuma yenu katika juhudi hizo.
Video hiyo hadi sasa ipo YouTube.