Mauaji ya Mwangosi: Ushahidi zaidi wa picha

Mauaji ya Mwangosi: Ushahidi zaidi wa picha

wanajukwaa kwenye hizo picha kuna ushahidi tosha! Marehemu amefia mikononi mwa maaskari wenye vyeo kwani jaribuni kuchunguza hizo kofia za maaskari.mlipuaji ni mmoja waliobaki ni wale viongozi wa wale maaskari waliokuwa wanapiga mabomu
 
Hivi wakati haya yanatokea kina Slaa walikuwa wapi? Mbona hakuna picha hata moja wanayoonekana kina Slaa?
hawakuwepo iringa wakati huu kwa sababu haya hayakuwa maandamano ila ulikuwa uzinduzi mdogo tu wa tawi hata uchache wa watu pichani unaonesha kwamba hii haikuwa shughuli kubwa kihivyo zaidi ya kukamilisha tu uhalifu wa kipolisi.
 
attachment.php.jpg


Hii picha backgroud yake inaonyesha wazi kuwa siyo ya pale kwenye tukio.
Kwanza hata ukiangalia rangi ya ardhi inatofautiana na zile za kwanza, pili hii nyumba ina bati juu wakati zile za kwanza ni kama tiles vile, then hapakuwa na Polisi mwenye uniform hizi za huyo anayeonekana nyuma yake kwenye picha za mwanzo, wote walikuwa wamevalia zaidi za FFU. Aina ya miti na majani ni pia ni tofauti sana.
Chunguzeni zaidi mtaona kuwa mwenye kuileta hii picha hapa anataka kupotosha ukweli tu Jambo ambalo si zuri.
 
Dah! Sijui watafungwa na nani? Tuombe MUNGU, baada ya muda tutasikia hili swala liko mahakamani hakuna kulizungumzia.
watwanyamazisha watu kusema lakini hawatawatia ububu ndipo pale sauti iliyokuwa imezuiliwa itakapotoka kwa kasi ya mshale.wangapi waliyafanya miaka dahali yakaja kuwaumbua wakati wakiamini yalishapita.
 
Doh! kwanini alietoa amri au mkuu wa kikosi hicho maarumu cha kuzuia mikutano ya chadema au wizara husika, wachuliwe hatua na haki zabinadam. kwani itakuwa kama mchezo askari kuuwa watu.
 
Kwanini nahisi huu unyama aliofanyiwa huyu mwandishi na kushangaza kuwa si bure lazima illikuwa inatokana na mlipuko wa hasira za hawa jamaa ambao walikuwa wametumwa kuwamaliza viongozi wa juu wa Chadema, sitaki kutaja majina tu. Lakini inavyoonekana huenda walihisi kuwa Mwangosi ndiye aliyevujisha habari kwa waliotakiwa kuuwawa wakawa wameshaondoka kwenye tukio au wakachelewa kufika kwenye mkutano. Sasa walipofika wakawakosa basi wakamchukulia kama msaliti wao? Je inawezekna ndiye aliyetakiwa kuwapa habari kuwa wako wapi viongozi wa chadema kwa wakati huo? Jambo ambalo huenda aliwapotosha kwa makusudi ili wasifanikiwe kutekeleza unyama wao?

Kuna mazito zaidi ya kujiuliza hapa haswa ukiunganisha na kauli zinazotolewa hivi karibuni.
 
Mtiririko wa matukio kabla polisi hawajautoa uhai wa marehemu Mwangosi (RIP)












Picha zaidi zinakuja (mtandao upo slow)

attachment.php









attachment.php


Wakuu hizi picha mkiangalia kwa makini kuna nyuso zinajitokeza. Katika picha hii ya mwisho kuna shahidi muhimu ambaye amevaa kiraia, amejitokeza kwenye picha ya sita kutoka juu. Huyu haiyumkiniki ameshuhudia mlipuko na msambaratiko wa mwili wa marehemu...

Hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe hadi ukweli uanikwe

ATIMAE MAJINA YA WAHUSIKA YAANZA KUMIMINIKA

JAMAA MWENYE KOFIA HAPO JUU KWENYE GARI NA MWENYE KUONEKANA NA NGUO ZA KIRAIA KATIKA PICHA HIYO WANAPO MSHAMBULIA MWANGOSI IMEBAINIKA KUA ANATAMBULIKA KWA JINA LA GABRIEL

NA ALIE KUWA AKIWAKATAZA WENZAKE WASIMSHAMBULIE MAREHEMU AMETAMBULIKA KUA ANAITWA MWAMPAMBA
Habari zaidi zinasema askari watatu wapo rumande MUFINDI IRINGA...
SOURCE. Tanzania Daima
 
Slaa alikuwa amekimbia na kuwaacha wanachama wenzake wapigwe na mabomu km yeye kidume angekaa pale mbn kakimbia hahahahahhahahaah CDM bana
 
huyo aliyevaa kiraia amejitokeza mara mbili akiwa na askari mmoja kwenye gari karibu na ofisi ya chadema na pale eneo la tukio! Huyu anajua kabisa huo mlipuko ulitokeaje!

huyo ni mtu wao,huoni kwenye picha ya pili kanyosha cha moto juu.? Hao ni watu wa upelelezi, nakumbuka enzi za maandamano chuoni tulikuwa tunakutana sana na hao wa kiraia ndo huwa wanatangulia.
 
Labda si Tanzania niijuayo mimi kwani wangapi wamefungwa toka wakutwe na makosa?!?labda mimi na wewe ambao hatuna hata BIBI na BABU waliowahi kuwa na cheo katika nchi hii.....ila kinachohitajika ni kwamba sisi wenyewe watanzania tubadilike na kuamua kujikomboa na jinamizi hili linalotuzunguka......kwani hali sasa ilivyo inatisha kwani hakuna serikali inayokuwa adui na raia wake.....INATISHA MABADILIKO YANAHITAJIKA HARAKA.....
 
mkandala hizo picha zako 2 naona ni za kweli
harafu hana hata wasiwasi baada ya kutoa uhai wa mwenzake
duniani kuna mashetani watu ..
 
Last edited by a moderator:
huyo ni mtu wao,huoni kwenye picha ya pili kanyosha cha moto juu.? Hao ni watu wa upelelezi, nakumbuka enzi za maandamano chuoni tulikuwa tunakutana sana na hao wa kiraia ndo huwa wanatangulia.

Mmh! Haya mauji yalikuwa yamepangwa vilivyo! Walikuwa wanamtaka Slaa!
 
Huu ufedhuri unaofanywa na serikali zisizotii haki za binadamu na sheria, ipo siku zitageuka na kuwa mbegu zinazooteshwa katikati ya ardhi yenye udongo wenye rutuba. Tunampa pole ndugu yetu awe na moyo wa ujasiri, kwani hawa jamaa wameamua kuwaua ndugu zao wenyewe ili kudhoofisha nguvu ya umma. Lakini hawatashinda. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Slaa alikuwa amekimbia na kuwaacha wanachama wenzake wapigwe na mabomu km yeye kidume angekaa pale mbn kakimbia hahahahahhahahaah CDM bana

tunajadili jambo muhimu ktk taifa letu,tuondolee kwashakoo yako ya akili.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Ninachokiamini ni kwamba hata paka ukimkimbiza akichoka husimama gafla tayari kwa mapambano.sasa nadhan hata watanzania tusishindwa ujanja hata na paka
 
Mmh! Haya mauji yalikuwa yamepangwa vilivyo! Walikuwa wanamtaka Slaa!

Kuna Polisi anadai kuna uwezekano baadhi ya washiriki wa mauaji hayo walitoka green guards na chombo kimoja cha usalama,kwamba walivaa nguo za polisi kutekeleza ujambazi wao.
 
Firstlady,Nadhani sio mtu mmoja ukiangalia katika angle tofautitofauti, ...................... Ukiangaliia background ya hizo picha unagundua kuwa zilipigwa katika maeneo tofauti kabisa, hiyo yenye mauaji inaonekana kuna nyumba za matofali ya kuchomwa na hata roof ni tofauti na hiyo inayomwonyesha askari huyo mwenye damu.................................. Ukiwaangalia hao askari wawili wana onekana wana tofauti ya kimaumbile, hiyo ya kwanza anaonekana ni Askari mwembamba na ya pili inaonekana ni Askari mwenye Nyama kumzidi yule anayemwelekeza bunduki marehemu..........................................................., na hata hiyo Damu inayoonekana kwenye uso wa Jamaa kama ingekuwa ni damu ya Marehemu basi ingekuwa pia kwenye nguo za huyo Askari, maana zinaonekana kwa wingi usoni, kwenye Kofia na kwenye mAwani......................................Huyo askari anayemwekelekezea bunduki Marehemu anaonekana hana safety glass, wakati huyu mwenye Damu anaonekana ana hizo gogles na zina Damu, hope ni watu tofauti na labda pia ni matukio tofauti
 
huyo ni mtu wao,huoni kwenye picha ya pili kanyosha cha moto juu.? Hao ni watu wa upelelezi, nakumbuka enzi za maandamano chuoni tulikuwa tunakutana sana na hao wa kiraia ndo huwa wanatangulia.

Akili ya kawaida tu inakuonyesha kuwa huyo jamaa ni askari kanzu(plain cloth policeman). Haingewezekana mwana-CDM awe very close na hao polisi vichaa waliokuwa wamekula cigar(sigara kubwa au Bangi).Kwa hiyo uwepo wake pale hausaidii chochote isipokuwa atakachofanya ni kupindisha ukweli halisi wa tukio husika!
 
Mimi nimetoa ushahidi wa kisayansi. Wewe unachofanya ni kusema tu mimi nipo OFF TARGET bila kutoa hoja. Nikuulize swali?

Unaelezeaje huyo askari kuwa na damu hapo katikati ya paji la uso wake. Yaani hata kifuani hana?

Nataka ujifanye wewe ndo ulikuwa unamchomeka marehemu kitu kinachosababisha damu iruke

Kama damu imekurukia hapo katikati ya paji la uso maana yake ulikuwa umesimama upande gani wa marehemu. Na je uliinama au ulikuwa umenyooka?

Rafiki, angalia vizuri jamaa anayo matone ya damu kifuani.
 
Back
Top Bottom