Mauaji ya mtanzania Wisconsin US miaka ya 90

Mauaji ya mtanzania Wisconsin US miaka ya 90

Ngwathra

Platinum Member
Joined
Jul 11, 2007
Posts
6,122
Reaction score
11,761
Ni miaka mingi imepita tangu hili tukio limetokea kwa kaka kumuua dada yake na kufungwa maisha jela hata baada ya rufaa adhabu haikupungua na hadi sasa anatumikia kifungo.

Kwa ufupi mauaji yanahusu kisa cha kusikitisha cha mwaka 1999 ambapo Mwivano Mwambashi Kupaza, mwanafunzi wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 25, aliuawa na binamu yake, Peter T. Kupaza, huko Madison, Wisconsin, Marekani.

Mwivano Kupaza alihamia Wisconsin mwaka 1997 kutoka Tanzania kwa ajili ya masomo na aliishi kwa kaka yake na mkewe wa kizungu ambaye baadaye ndoa ya kaka yake ilivunjika wakabaki wawili kwenye apartment.

Mnamo Julai 1999, mabaki ya mwili wa Mwivano yaliyokatwakatwa yalipatikana kwenye mifuko ya plastiki kando ya Mto Wisconsin. Muuaji alikuwa ameondoa ngozi ya uso na kichwa cha mwathiriwa ili kuzuia asitambulike.

Iliwachukua miezi sita polisi kumtambua marehemu. Na walimpata utambuzi baada ya mke wa zamani wa Peter Kupaza kutambua picha iliyochorwa na polisi kutokana na kumodel fuvu la kichwa cha Mwivano lilopatikana kwa udongo maalum na kulipiga picha, hii ilikuwa mara ya kwanza teknolojia ya uchapishaji wa 3D kutumika kutambua mwathiriwa.

Waendesha mashtaka walidai kuwa Mwivano alikuwa amewaambia marafiki zake kuwa Peter alikuwa akimnyanyasa kijinsia, na ilisemekana huenda alimpa mimba na Mwivano akakataa kuitoa jambo ambalo Peter aliona lingekuwa fedheha kubwa sana kama familia ya jamii yake nyumbani Tanzania ingejua, kwa sababu ni yeye aliyemleta Marekani kwa kumuombea ruhusa kwa baba mzazi wa marehemu.

Peter Kupaza alikamatwa mapema mwaka 2000 na kupatikana na hatia ya mauaji ya makusudi na kuficha maiti na hatimaye akahukumiwa kifungo cha maisha jela.

Peter alikata rufaa mara kadhaa na zote hazikuweza kuwashawishi majaji kubadilisha hukumu kwa kuwa zote ziliegemea kwenye ushahidi wa mbwa wa kunusa (cadaver dog) uliotolewa na Sarah Anderson, ambaye alipoteza sifa na kushitakiwa kwa kupandikiza ushahidi katika kesi nyingine, so akajua kumdiscredit huyu mama kutaifanya mahakama iamue kuchunguza upya kwamba huenda alipika ushahidi kwa kesi yake pia.

Hata hivyo, mahakama za Wisconsin zilikazia hukumu ya Kupaza, kwa kuwa kulikua na ushahidi mwingine ikiwemo vitu vya marehemu vilivyokutwa nyumbani kwa Peter na mifuko ya plastiki ya shopping iliyokutwa nymbani kwake iliyolingana iliyotumika kuhifadhi vipande vya mwili wa dada yake vilivyokutwa ndani ya mto na ulikuwa wa kutosha kumtia hatiani bila hata ya ushahidi huo wa mbwa walisema jury na majaji.

Kwa wanaojua kimombo kesi hii ipo online na hapa naweka link ya hukumu ya rufaa ya mwisho

Lilikuwa somo, masikitiko na fadhaa kubwa kwa kijana wa kitanzania (kwa wakati huo) kupoteza kila mpango wake wa maisha kisa tu ni ngono ambayo hadi sasa tunaipa kipaumbele sana

Karibuni kwa maoni wadau


Hii ni picha ya huyo dada

Picha ya Mwivano.jpg


Na hizi ni sample za udongo zilizoundwa na kupigwa picha na wataalam wa forensic sciences

1999_Sauk_County_Jane_Doe.webp
Mwivano_Kupaza_recon_long_hair.webp
Mwivano_Kupaza_recon.webp
Kupaza_side_recon.webp
Mwivano_Kupaza_recon_short_hair_color.webp
 
Duh Wazungu kwa sasa wako mbali sana kwenye haya mambo ya teknolojia ya kuwabaini wahalifu. Huku Bongo ni ujinga tu. Imagine Lissu alipigwa risasi 32 saa saba mchana, na bado watuhumiwa hawakukamatwa! Mc Pilipili naye wauaji waungwana walimpigia ndugu yake na kwenda kumkabidhi akiwa anakaribia kukata moto, na bado mpaka leo eti hawajakamatwa!! Yaani wauaji walipiga mpaka simu, na bado hawajulikani!

All in all, huyu jamaa anastahili kabisa hicho kifungo alichopewa, kutokana na ukatili wake alioufanya kwa ndugu yake.
 
Duh Wazungu kwa sasa wako mbali sana kwenye haya mambo ya teknolojia ya kuwabaini wahalifu. Huku Bongo ni ujinga tu. Imagine Lissu alipigwa risasi 32 saa saba mchana, na bado watuhumiwa hawakukamatwa! Mc Pilipili naye wauaji waungwana walimpigia ndugu yake na kwenda kumkabidhi, na bado mpaka leo eti hawajakamatwa!!

All in all, huyu jamaa anastahili kabisa hicho kifungo alichopewa, kutokana na ukatili wake alioufanya kwa ndugu yake.

Inasikitisha sana nchi yetu haina hata tech za miaka ya 60 acha ya 90, wakati wa baba wa taifa nakumbuka kulikuwa na wataalam wa alama za vidole leo hii huwezi kusikia kama wapo na wanafanya nini! Tulisikia kwenye kesi za Mbowe na Lissu kwamba kuna maabara ya kitaalamu lakini walipokuja wataalamu wenyewe kutoa ushahidi duh, ilikuwa maajabu yani utaalamu wa kibongo ni uchafu tu wa kusikitisha kuna nini tupo nacho seriuos unakosa😛😛😛
 
Nakumbuka hii kesi walishawahi kuileta humu zamani na waliidadavua wajuzi.

Inawezekana kweli wakati JF ilikuwa JF nimesearch sijaiona lakini so nikaona tukumbushane, nilikuwa kijana ndio naanza kazi za umma miaka hiyo.

Vijana genzee hawajui hizi kesi so wanajifunza tunapokumbusha
 
Mke wake wa kizungu aliachana nae baada ya kujua amempa mimba dada yake
Hii ya kusema binamu, alitunga tu isionekane ni incest

Yawezekana kabisa! Wamarekani waligharamia wazazi wote wa Peter na dada yake kuja Marekani kuhudhuria kesi na kuona namna haki inavyotendeka na mhalifu anavyohukumiwa bila kujali hali
 
Back
Top Bottom